Kijana Mkimbizi Raia wa Liberia, Aliyejipatia Elimu Marekani, na kisha Kuamua Kurudi ‘Nyumbani’

Jefferson Krua fled Liberia as a refugee at age 5, and eventually settled in Boston, MA. Recently, he's moved back to Liberia to help with re-building the country's infrastructure. Credit: Heidi Shin

Jefferson Krua aliondoka nchini Liberia akiwa na miaka mitano, na kisha kupata makazi ya kudumu huko Boston, MA. Hivi karibuni alirejea nchini Liberia kwa ajili ya kusaidia kwenye ujenzi mpya wa nchi yake. Picha kwa hisani ya Heidi Shin

Makala haya yaliyoandikwa na Heidi Shin kwa mara ya kwanza yalichapishwa PRI.org mnamo tarehe 12 Julai 2016 na yanachapishwa tena hapa kwa makubaliano ya kushirikiana maudhui.

Mercy Krua na mtoto wake Jefferson wanashindwa kuafikiana. Sababu kuu ni ikiwa ni sahihi kwa Jefferson kurudi nyumbani.

Tunakaa kwenye kochi la chumba anachoishi huko Boston, na kisha anakuwa na mshawasha wa kutuonesha picha za utoto wake. Picha hii ni ya wakati wa mahafali, nah ii ni ya wakati nikiwa kwenye kambi za wakimbizi nchini Ghana. Anakumbushia maisha yalivyokuwa kabla ya kutoka nchi Liberia, kipindi ambacho vita ya wenyewe kwa wenyewe ilipokuwa imeshamiri.

Kwa wakati huo, Jefferson alikuwa bado ni kijana mdogo, na pale alipopatwa na njaa au kuchoka, mama yake hakuweza kumpatia hata kifungua kinywa. Machozi yalikuwa yakimtoka, na alikuwa mwenye hofu kuu kwa kuwa angeweza kugundulika: “Kwa hiyo inakupasa kuhakikisha kuwa mtoto halii, ni kama vile kumfahamisha kuwa kulikuwa na watu au raia katika eneo lile. Hii ni kwa sababu watu wale hawakuwa wanajali, walikuwa wakimuua kila mmoja. Kwa kweli, ilikuwa hali tete sana, iliogopesha haswa.”

Hata hivyo, Jefferson ana kumbukumbu ya tofauti. Wakati wanaondoka, yeye alikuwa na miaka mitano tu, na yeye alijisikia kama vile ni safari ya mapumziko. Kujificha nyuma ya gari la misaada ya chakula la Umoja wa Mataifa (UN) ili kupata mwanya wa kuondoka Liberia kupitia kwenye misitu ya Ivory Coast na kabla ya kufikia kwenye kambi za wakimbizi nchini Ghana, ambapo waliishi kwa miaka saba.

Jefferson anasema kuwa, mara baada ya kuwasili nchini Marekani, ndipo alipogundua kuwa maisha haya kuwa yakimwendea vizuri hapo awali. Hii ilikuwa ni kwenye miaka ya 1990, ambapo alikuwa karibu kuanza shule ya sekondari.
Ananichukua hadi kwenye miradi ya nyumba huko Boston mahali ambapo aliishi kwa kipindi chote cha ujana wake. Ananikumbusha kufunga mlango wa gari na kisha kunionesha kwenye kona ya barabara, mahali ambapo yeye na mpwa wake walishambuliwa huku mlinzi wa shule akishuhudia. Tunasikia sauti nyembamba za bembea, na watoto wanapiga kelele kwa lafudhi za kikepverde na lafudhi ya waafrika waliozaliwa Marekani. Kiasi kwamba wanaweza kusikika hata kwenye sauti ya juu ya ving’ora vya polisi na vya magari ya wagonjwa yanayopita karibu.

Jefferson alipokuwa mtoto, alikuwa akiruhusiwa kutoka tu nyumbani na kenda shule na kanisani, basi. Alizingatia sana kwenye masomo hadi akafanikiwa kufika chuo-Chuo Kikuu cha Cornell, ambapo alikutana na Waafrika wengine ambao hawakuwa wakimbizi, lakini wanafunzi wa kutoka mataifa mengine. Hapa alijisikia kuwa ilikuwa fahari kuwa Mwafrika. Chuo hiki kilikuwa na mkusanyiko wa majarida adhimu, ambapo katika majirida haya aliweza kujisomea mambo anuai kuhusu Liberia.

Anaukubali utani wa kuja Marekani, kwenye maeneo ya ndani kama ya Ithaca, New York, ili kujifunza kuhusu chimbuko la familia yake. Alijiufnza tena kuzungumza lugha ya kwao, alisomea uandisi wa majengo huku akitafakari kuhusu kurudi Liberia. Alipata habari za vijana wengine wa kiafrika-ambao walisoma nchi za nje-na kisha kurejea barani Afrika.

Kwa hiyo, wakati wa kipindi cha kiangazi kilichopita, Jefferson alirejea nchini Liberia, mara tu baada ya kutokomezwa kwa ugonjwa wa Ebola. Ananakumbuka halia aliyokuw anayo wakati wa kuwasili. “Ndugu, nilitamani kuibusu ardhi. Nilistaajabishwa sana,” anasema. “ Ni kama vile kila mmoja anaongea kama unapokuwa kwako, ni hisia nzuri sana kutokujisikia vinginevyo.”

Jefferson launched a digital news outlet in Liberia called the Bush Chicken. Here is a photo he took while on assignment, covering a student protest against proposed tuition hikes at the University of Liberia. Credit: Photo courtesy of Jefferson Krua

Jefferson alizindua chombo cha habari cha kidigitali nchini Liberia alichokipa jina la Bush Chicken. Hii ni picha aliyoichukua wakati akiwa kwenye ukusanyaji wa taarifa, alipokuwa akikusanya habari kuhusu mgomo wa wanafunzi dhidi ya pendekezo la ongezeko la ada ya Chuo Kikuu cha Liberia. Picha kwa hisani ya Jefferson Krua

Alizindua chombo cha habari cha kidigitali kinachofahamika kwa jina la Bush Chicken, ambacho kinatoa mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu namna ya kuripoti habari kwa usahihi. which trains journalists to report with accuracy. Pia anatazamia kuanzisha mradi wa kushirikiana baiskeli katika jiji la Monrovia, ambapo utawasaidia watoto kutumia mda mchache kufika shuleni.

Hata hivyo, mama yake ana hofu kuhusu usalama wa mtoto Jefferson’s, kiasi kwamba anasema anachoweza kufanya ni kumuomba tu Mungu. Hawana tena ndugu wa kumuangalia Jefferson huko Liberia, na hata miti ya matunda, waliyokuwa wakiitegemea kwa maembe na machungwa — haipo tena. Ardhi ile siyo ya kwao tena, hata na kwake, nyumbani pia kumepotea.

Kwa mtazamo wa Mercy, mama yake na Jefferson, Marekani ndiyo sehemu iliyompatia mafanikio. Kwenye kambi za wakimbizi, hakukuwa na kazi yayote ya kufanya. Lakini, hapa Marekani, siku nzima anafanya kazi ya kuwatunza watoto, kuwa mwangalizi wa watoto wa watu wengine, kwa hiyo, anaweza kupata kiasi cha fedha cha kuwaangali na watoto wake. Aliweza kutumia fedha zake vizuri na kusomea uuguzi, na kwa sasa anafany kazi kama muuguzi aliyesajiliwa.

“Bila hiana, mimi ni raia kutoka Liberia,” anasema. “Lakini kwa hapa nilipo sasa ndipo ninapopaona kama nyumbani. Popote ulipo, panapokupatia riziki yako, kwa maoni yangu, ndipo ninapopachukulia kuwa ni nyumbani.”

Mercy Krua, and her son Jefferson Krua, on her living room couch in Boston, MA. Credit: Heidi Shin

Mercy Krua akiwa na mtoto wake Jefferson Krua, wakiwa wamekaa kwenye kochi la chumba chake huko Boston, MA. Picha kwa hisani ya Heidi Shin

Hapendi tena kuzuizungumzia Liberia kabisa — kumbukumbu alizonazo zinamfanya ajisikie vvibaya sana. Kinyume chake, ananionesha picha ya Rais wa Marekani, barack Obama na ya Mwanaharakati wa masuala ya kijamii hayati Martin Luther King, Jr ambazo amezitundika kwenye ukuta wa chumba chake cha kulala kwenye nyumba anayoimiliki.

Pamoja na haya, Jefferson ananisimmulia habari ya purukushani aliyokabiliana nayo na polisi, mbele ya nyumba ya mama yake huko Boston, pale alipomtembelea siku za hivi karibuni.

“Wananiuliza maswali, lakini mmoja wao anakuwa mkali kweli kweli,” anasema Jefferson. Askari anamfokea wakati Jefferson akiendelea kutafuta leseni yake: “Kwa nini unachukua muda mrefu hivyo?, Hufahamu kuwa kuna baridi kali sana?”

Jefferson anakiri, “Nikijiangalia kuwa mimi ni mtu mweusi nchini Marekani, ninaogopa sana.”

Anaendelea, “kwa hiyo, kwa mambo kama haya, ni vigumu sana kusema Marekani ni nyumbani. Bila kujali ni kiasi gani cha fedha ninakipata katika nchi hii, kwa vyovyote, nitaendelea kuw amtu mweusi nchini Marekani.”

Lakini nchini Liberia, Jefferson ni asilimia moja tu. Alinionesha picha za maeneo mbalimbali aliyoyatembelea, kitambulisho cha uandishi wa habari alichokuwa akikionesha na kupata ruhusa. Angaliweza pia kutumia lafudhi ya kimarekani kama angependa— kitu ambacho kinaweza kukupa kutaminiwa nchini Liberia. Ana ndoto ya kuwa Waziri wa Uchukuzi na anapendelea kutokuwa raia wa Marekani, ili ajiahakikishie kuingia kwenye siasa huko Liberia.

“Ndoto zangu zote, kila kitu, mikakati yangu yote kwenye maisha, inailenga Liberia,” anasema Jefferson. Anaendelea kusema, “huwa ninakuwa na ndoto za majinamizi, yani ninaamka na kujikuta ninatokwa jasho, kwamba Liberia imeangukia kwenye vita kwa mara nyingine. Hii ndio hofu kubwa niliyonayo, kwa kuwa sijui nitafanya nini.”

Lakini, kwa sasa anajivunia kwa neema ambazo anazipata awapo kwenye makazi yake mapya, na pia anawajibika kuijenga upya nchi yake, na hapa anasema, “mambo kama ya vita sidhani kama yatatokea tena.”

Habari hii iliandaliwa kwa ushirikiano na Kongamano la Uponyaji na Masimulizi la Picha na Sauti za Matumaini.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.