Ayatollah Khomeini Alifariki Miaka 27 Iliyopita, Lakini Msaidizi wa Trump Anamtaka Alaani Shambulio la Nice Hivi Karibuni

Retired Lt. General Michael T. Flynn appears on Fox News. Image: YouTube

Luteni Jenerali Mstaafu Michael T. Flynn akionekana kwenye Kituo cha Fox News. Picha: YouTube

Kampeni ya Urais ya Donald Trump imekuwa ikipigania “kuchukuliwa kwa hatua kali dhidi ya Iran,” lakini propaganda imeenea juma lililopita, kudai kuwa Luteni Jenerali Mstaafu Michael T. Flynn, mmoja wa washauri wakuu wa Trump wa masuala ya kijeshi na mkurugenzi wa zamani wa Shirika la Upelelezi wa Kiusalam (DIA), alimtoa wito kwa Ayatollah Khomeini—mtu ambaye alifariki zaidi ya robo karne iliyopita—kulaani shambulio lililofanyika Julai 14, mjini Nice, nchini Ufaransa.

Michael Flynn, mkurugenzi wa zamani wa Shirika la Upelelezi wa Kusalam, alitoa wito kwa mtu aliyekufa miaka 27 iliyopita kulaani msimamo mkali wa kidini

Akiongea kwenye Kituo cha Televisheni cha Fox News akiwa na Megyn Kelly, Flynn alisema kwa hasira, “Ninamtaka Imam, au Khomeini, atoke hadharani na kuzungumzia itikadi hii kali ya kidini isiyojitenga na damu na nasaba za dini yao.”

Ayatollah Sayyid Ruhollah Khomeini alikufa 1989 baada ya kuasisi Taifa ya Kiislamu la Iran, nchi ya kwanza ya kidini, kufuatia Mapinduzi ya Kiislam mwaka 1979.

Inaonekana Flynn ama alichanganya jina “Khomeini” na jina la Kiongozi Mkuu wa sasa, Ayatollah Sayyed Ali Hosseini Khamenei, au basi hakuwa anafahamu kuwa Ayatollah Khomeini alikufa miaka 27 iliyopita. Iwe kwamba kosa hilo limetokana na kuchanganya mambo au basi tu kutokujua, Flynn alionekana Fox News kwa mara nyingine kesho yake, mnamo Julai 15, na kumtaka Khomeini, akisisitiza kwamba mtu huyo aliyefariki zamani alaani mashambulio ya mjini Nice.

Watumiaji wa mtandao wa Intaneti nchini Irani na Marekani walisema machache kuhusiana na shauku hiyo ya Flynn kwa “Imam Khomeini.” Mtumiaji wa Twita Ameneh Mousavi alitwiti:

Watu wenye hekima, hivi hili linaweza kuwa sawa? Jenerali Michael Flynn, mshauri wa jeshi wa Donald Trump anamtaka “Ayatollah Khomeini,” kiongozi wa Iran, kulaani mashambulio ya kigaidi ya Nice.

Mwandishi wa ki-Iran mwenye asili ya Marekani Saman Arbabi aliandika:

Kuhusu sera ya mamabo ya nje, timu ya Trump inamfanya timu Bush ionekane kama mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel

Watumiaji wa mtandao wa intaneti walitazama suala kuu la habari hiyo, kadhalika, baada ya  Huffington Post kuliandika suala hilo:

Maneno ya Flynn kuwahusisha viongozi wa Kiislam hayana maana kwa sababu anayemtaja amekufa miaka 30 iliyopita

Sawa, eti tuwape madaraka watu ambao hawawezi hata kutofautisha watu waliokufa na wale walio hai

Akaunti ya mashabiki wanaomkejeli waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Urusi, Sergei Lavrov, ilikuwa na maoni yafuatayo:

Inawezekana huyu jamaa anajua Gorbachev bado ni rais wa Urusi. Mshauri wa Trump anamtaka Khomeini alaani shambulio la kigaidi la Nice

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.