Watu Wasiopungua 42 Wafariki Dunia Kufuatia Shambulio la Uwanja wa Ndege Istanbul

Ataturk Airport wikipedia image.

Uwanja wa Ndege wa Ataturk. Picha: wikipedia.

Watu wasiopungua 42 wamepoteza maisha kufuatia mashambulizi ya risasi na mabomu matatu ya kujitoa muhanga kwenye uwanja wa ndege wa Ataturk, Istanbul, ambao ni moja wapo ya viwanja vyenye shughuli nyingi zaidi barani Ulaya na kituo cha usalama wa anga duniani.

Mashambulizi hayo yaliyofanywa na wakimbizi wasiopungua watatu yalifanywa mnamo Juni 29 na Waziri Mkuu wa Uturuki Binali Yildirim anayahusisha mashambulizi hayo na kikundi cha magaidi wa ISIS.

Kwamba shambulio hilo lilifanyika katika uwanja wenye shughuli nyingi zaidi duniani kulimaanisha kwamba habari hizo zilisambaa kwa haraka kupitia vyombo vikuu vya habari duniani kote sambamba na vyombo vya habari za kiraia:

Picha ya kwanza ya uwanja wa ndege wa Ataturk jijini Instabul ambapo mabomu mawili makubwa yalilipuka kwenye sehemu mbili za kuingilia au kutokea abiria wa kimataifa, na kusababisha majeruhi wengi

UTURUKI – Watoto na ndugu wakikumbatiana wakati wakiondoka kwenye uwanja wa ndege wa Ataturk baada ya shambulio la kujitoa muhanga la Instabul

Kama ambavyo imekuwa kawaida nchini Uturuki wakati wa matukio ya majanga, mamlaka za nchi hiyo zilikimbilia kutafuta zuio la kimahakama kuzuia watu kuacha kujadili tukio hilo na hivyo kufungia mitandao ya Facebook na Twita ambayo awali ilikuwa ikipatikana mpaka jioni ya Jumatano.

Tangazo la kuzuia majadiliano ya tukio la shambulio la Istanbul Ataturk limetolewa na Waziri Mkuu

Mwandishi wa Global Voices Efe Kerem Sozeri alichambua jaribio la serikali kufungia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kwenye mtandao wa Vocativ, akisisitiza kwamba serikali ilikuwa imezuia watu kupata habari muhimu kwa wakati.

Wakati madereva teksi walitumia janga hilo kujipatia kipato kwa kudai nauli zaidi ya kawaida, mahoteli kwenye miji yote mikubwa nchini Uturuki pamoja na jiji la Instanbul ziliwakaribisha wasafiri wa mataifa yote waliokuwa wamekwama bila kuwatoza gharama zozote.

Wageni 16 wamepumzika kwenye vyumba vyao. Tuna chumba kimoja kimebaki!

Inasisimua: Mwanafunzi wa Uturuki anayeishi karibu na uwanja wa ndege amewakaribisha wasafiri waliokuwa wamekwama kulala nyumbani kwake

Mashambulio yanayofanyika kwenye viwanja wa ndege yanatukumbusha kile ambacho wachambuzi wa mambo wamekuwa wakiita ‘hali ya kawaida’ ya Uturuki —kwa maana ya mzunguko ule ule wa mashambulio yanayowalenga raia waliokuwa wakionekana kuwa na amani miaka miwili iliyopita.

Mashambulio makubwa ya hivi karibuni…na mgogoro wa Kusini Mashariki ya Uturuki …mamia…mamia wamekufa

Mashambulio yametokea miaka miwili kamili baada ya kiongozi wa magaidi wa ISIS Abu Bakr al-Baghdadi kutangaza kuushikilia mjini wa Mosul nchini Iraq, ingawa kikudni hicho mpaka sasa bado hakijatangaza kuhusika na shambulio hizo.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.