Mwishoni mwa Februari 2016, Mamlaka ya Takwimu ya nchini Japan ilitangaza kuwa idadi ya watu nchini humo imepungua kwa kiasi kikubwa, huku ididi kubwa ya watu wakipoteza maisha kuliko wanaozaliwa, hali inayojitokeza kwa mara ya kwanza tangu 1920, mwaka ambao nchi hii ilianza kuweka kumbukumbu hizi
Habari hizi zinakuja wakati ambao regular news reports in Western media that raia wa Japan wanajamiiana kwa kiasi kidogo kuliko wakati mwingine wowote . Baadhi ya waandishi wa nchi za Magharibi wanafikia mahali pa kuuliza ni kwa nini vijana wa Japan wameacha kujamiiana .
Hata hivyo, ni kwa kiasi gani wajapani wanajamiiana, na pia, kujamiiana ndio kutasaidia kuongeza kiwango cha kuzaliana?
Ni rasmi kuwa idadi ya watu nchini Japan inashuka
Kwanza, hetu tutupie jicho kushuka kwa idadi ya watu nchini Japan. Kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita, (Japan huwa inafanya sensa kamili za idadi ya watu mara moja kila baada ya miaka kumi, na sensa ya wastani kila baada ya miaka mitano ), Idadi ya watu nchini Japan imepungua kwa takribani watu 950,000 (kwa kiasi cha asilimia 0.7) hadi kufikia watu milioni 127.1. Takribani theluthi moja ya raia wa Japan walikuwa na zaidi ya miaka 65 mwaka 2015. Hadi kufikia mwaka 2050, asilimia 40 ya raia wa Japan watakuwa na umri wa zaidi ya miaka 65.
Hali ya idadi ya Raia nchini Japan inaonekana kuwa mbaya zaidi kwani kiwango cha uwezo wa kuzaa kimekuwa cha wastani wa uzao wa 1.41 kwa kila mwanamke, hali inayoiweka Japan kuwa chini ya “wastani wa kuleta kizazi kipya” cha 2.1 (Wastani wa idadi ya watoto wanaozaliwa na mwanamke mmoja ili kuweza kuleta kizazi kipya kwa takribani miaka arobaini tangu miaka ya 1970).
Tangazo la Mamlaka ya Takwimu la mezi huu kuhusu kushuka kwa idadi ya watu nchini japan, lilishatabiriwa mapema sana
Japan siyo nchi pekee duniani inayoshuhudia hali hii. Nchini Ujerumani, uwezo wa kuzaa umeendelea kuwa chini ya kiwango cha watoto 1.5 kwa kila mwanamke tangu mwaka 1975, huku Benki ya Dunia ikiweka bayana kuwa Asia ya Mashariki na eneo la Pasifiki yakiwa na kiwango kikubwa cha watu wanaozeeka haraka sana kuliko eneo jingine lolote lile. Kwa maneno mengine, hali ya “uzee” ya taifa hili ni ya kidunia na siyo ya kipekee kwa nchi ya Japan.
Serikali ya Abe ana malengo ya “kuimarisha” idadi ya watu nchini Japan na kufikia watu milioni 100 kwa kuwahamashisha wanawake (angalao) kuwa na watoto wengi zaidi na hivyo kuongeza kiwango cha ongezeko la idadi ya watu.
Tatizo kubwa (kwa utashi wa kuzaliwa, kwa kiwango chochotesays conventional wisdom, at any rate) ni kuwa raia wa Japan hawana tena ari ya kujamiiana.
“Hali ya useja” ya raia wa Japan: Ni halisi au inadhaniwa tu na vyombo vya habari vya kigeni?
badala ya kuwalinganisha Wajapani na wenzao wa nchi kama Ujerumani, raia wa Japani mara nyingi wanahusishwa na dhana kuwa raia wa japan hawana mazoea ya kujamiiana. Inaonekana kuwa kuna jina linalobeba dhana hii nchini Japan: “dhana ya Useja” (セックスしない症候群). Katika hali ya kufurahisha, matokeo ya Wikipedia ya maneno haya yanaonekana kwenye makala ya gazeti la Guardian ya mwaka 2013 inaonekana ndio chanzo cha awali cha neno hili.
Makala katika lugha ya kijapani kuhusu”dhana ya useja” inaanza kwa Kurejea video ya BBC ya mwaka 2013 iliyokuwa na jina “Hakuna kujamiiana, Tafadhali, Sisi ni WajapaniPlease.” Nyingi ya matokeo ya utafutaji wa “セックスしない症候群” yameonekana kufikia karibu 2013, na makala za vyombo vya habari vya kigeni kama vile Huffington Post na China's People's Daily Online vina matokeo ya juu ya utafutaji kwa lugha ya kijapani.
2006/07 Utafiti wa Durex bado Unashawishi
Kuna uwezekano kuwa suala hili liliibuliwa na utafiti wa kina kuhusu kujamiiana uliofahamika kama Utafiti wa kimataifa wa Afya ya Kujamiiana . Utafiti uliofanywa na kampuni ya kutengeneza kondomu ya Durex kati ya mwaka 2006 na 2007, utafiti uliofanyika takribani miaka kumi iliyopita kw kuwahoji watu 26,000 walio na umri wa miaka 16 na kuendelea kutoka mataifa 26 toafuti duniani kuhusiana na mtazamo wao kuhusu kujamiiana.
Pmaoja na kuwa imepita miaka 10 tangu kutangazwa kwa matokeo ya utafiti huo, matokeo ya utafiti wa Durex yameendelea kusambazwa na vyombo vya habari vya Magharibi pamoja na vile vya Japan.
Kwa mfano, kwenye makala ya mwaka 2014 ya toleo la mtandaoni la jarida la Toyo Kezai, Sechiyama Kaku, Profesa wa Chuo Kikuu cha Tokyo, arejelea utafiti wa Durex wa mwaka 2006/07 na kuweka bayana kuwa “Japan ndio nchi iliyo na kiwango kidogo kabisa cha mazoea ya kujamiiana duniani”. (Kwenye utafiti wa Durex, Raia wa Japan walionesha kujamiana mara 45 kwa mwaka, idadi ambayo ni ndogo kabisa miongoni mwa nchi zote 41 zilizoshiriki utafiti huo .)
Wakati haya yakisemwa, na kufahamika kwa kiasi kidogo, matokeo ya utafiti wa kampuni ya wajapani ya hivi karibuni inaonekana kuthibitisha matokeo ya Durex kuhusu hali ya ashiki ya raia wa Japan. Hali ya mambo ni kuwa, Sagami, kampuni maarufu ya kutengeneza kondomu ya Japan ilifanya utafiti wake yenyewe mwaka 2013 kuhusu kujamiiana nchini Japan. Mwanablogu Yuta Aoki alichapisha tathmini yake hapa ya matokeo ya utafiti wa Sagami kwa lugha ya Kiingereza. Aoki anasema kuwa, matokeo ya hivi karibuni ya Sagami yanaonekana kushabihiana na hitimisho la utafiti wa Durex: Raia wa Japani wanaonesha hawajihusishi sana kwenye tendo la kujamiiana.
“Ndoa za Japan Zisizoshiriki Tendo la Kujamiana”
Aoki anasema kuwa matokeo ya utafiti wa Sagami yanaonesha kuwa raia wa Japan walio kwenye mahusiano ya kimapenzi (durex ilimhusisha kila mtu aliyekuwa na hamasa ya mahusiano ya kimapenzi) wanaweza kujamiana kwa mara zisizozidi 45 kwa mwaka. Utafiti wa mwaka 2006 uliofanywa na Bayer uligundua kuwa kwa wastani watu wa japani waliokuwa kwenye ndoa walifanya tendo la ndoa mara 17 kwa kipindi chote cha mwaka.
Kwa kuongeza, utafiti wa Sagami uligundua kuwa asilimia 55.2 ya wanaondoa wasema kuwa hawakuwa wakifanya tendo la ndoa . ” Ndoa zisizoshiriki tendo la ndoa” imekuwa gumzo kubwa nchini Japan kwa miaka ya hivi karibuni.
Kwenye utafiti wa aiana yake Chama cha Uzazi wa Mpango cha Japan kiligundua kuwa wanaume wengi waliokuwa wameoa walijishughulisha zaidi na kazi au walionesha kuchoka kiasi cha kushindwa kufanya tendo la ndoa. Wanawake wa kijapani walisema kuwa kujamiana ni “kunafadhaisha sana.”
Hata hivyo, jambo la kufurahisha kuhusu utafiti wa Sagami, Aoki anabainisha kuwa, kwa ujumla, raia wa Japan wanapenda kushiriki tendo la kujamiiana:asilimia 83 ya wanaume na asilimia 58 ya wanawake ambao hawapo kwenye mahusiano ya kimapenzi katika umri wa miaka 20 na 30 wanasema kuwa wanatamani kujamiiana .
Wakati kunaweza kuwepo sababu anuai zanazowafanya baadhi ya watu nchini Japan hawajuhusishi na tendo la kujamiiana, kuchukia tendo la kujamiiana inaonekana siyo moja ya sababu hizo
Japanese Men May Be Having Sex, Just Not Always With Their Partners
Ni muhimu kufahamu kuwa, katika muktadha wa utafiti wa Sagami, watu ambao waliokuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na waliosema kuwa walikuwa sehemu ya “ndoa isiyoshiriki tendo la ndoa” waliweka bayana kama walikuwa wakishiriki tendo la ndoa na wenza wao au hawakuwa wakishiriki nao.
Kile ambacho hakitolewi ufafanuzi ni Kujamiana nje ya ndoa, na kujamiana kama namna ya kujipatia kipato.
Kwa mujibu wa tafiti anuai, kati ya asilimia 10 na 20 ya wanaume wa kijapani wanakiri kujamiana nje ya ndoa (不倫, furin) na wanawake nusu ya idadi hiyo. Kwa hiyo, hata kama raia wengi wa Japan wapo kwenye ndoa ambazo hazishiriki tendo la ndoa, siyo lazima iwe sahihi kusema kuwa hawafanyi tendo la kujamiiana.
Pamoja na hilo, wanaume wengi wa Japan walio kwenye ndoa wanasidia kuchangia kiasi cha dola za kimarekani bilioni 5 (5兆6,884億 円) kwenye biashara ya kujiuza. Hata hivyo, ni kiasi kidogo sana cha wanaume wa kijapani wanaojihusisha na mahusiano ya kimapenzi na wanawake tofauti wanapendelea kulipia ili kufanya ngono.
Wanaume Wacheache Sana wa Kijapani ndio Wanaoweza Kulipia ili Kufanya Ngono
Kwa mujibu wa Mamlaka ya Polisi ya Taifa la Japan (NPA), kwa mwaka 2011 kulikuwa na zaidi ya biashara 29,000 zilizohusihwa na biashara ya ngono (性風俗関連特殊営業, seifuzokukanrentokushueigyo)— biashara 10,000 zaidi ya zile zilizokuwepo miaka minne iliyopita tangu 2007.
Biashara ya ngono nchini Japan inajumuisha majengo kadhaa na makampuni ikiwa ni pamoja na madanguro (“soaplands”), massage parlors, mawakala wa kutafuta wapenzi, pamoja na huduma za “kulipia” za kutafutia wenza.
Kwenye utafiti mmoja uliofanywa na MiW (jumuia iliyojitolea kusaidia na kutoa ushauri kwa watu ambao wenza wao walibainika kufanya uzinzi), asilimia 23 ya wanaume waliopo kwenye ndoa walihojiwa huko Tokyo na kubainisha kuwa walitoa fedha ili kufanya ngono.
Utafiti mwingine uliofanywa na Kituo cha Elimu ya wanawake cha Japan kiligundua kuwa asilimia 40 ya wanaume wa kijapani walitoa fedha ili kufanya ngono.
Kwa hiyo, wakati “dhana ya useja” inaweza kuwepo, inaweza kuwa ni miongoni mwa wanaondoa wa muda mrefu wanaofanya ngono nje ya ndoa
Hali hii Inaiweka wapi Japan Kuhusu Kuzorota kwa Kiwango cha Kuzaliana?
Shukrani ziiendee serikali ya Abe, wanawake wa Japan wanawekwa kwenye majukumu ya aina mbili- au hata matatu: Wanawake wa Japan wanahamasishwa kuwa na watoto wengi ili kuongeza kiwango cha Japan cha kuzaliana na kupunguza kiwango cha kushuka kwa idadi ya watu. Wakati huo huo, wanawake wa Japan wanahamasishwa “kujituma” na kushiriki kwa wingi kwenye shughuli mbalimbali. Hata hivyo, wanawake watatakiwa kuwajibika kuwatunza watoto, na pia kuwatunza ndugu wao waliozeeka.
Kwa hiyo, hata kama kujamiiana sana kutamaanisha kuongezeka kwa kiwango cha kuzaliana, kwa wanawake wa kijapani, kwao itakuwa ni jukumu mojawapo, na pia kuwa na muda mchache zaidi kuliko walionao kwa wakati huu.
Sambamba na Utafifi wa Masae Okabayashi.