Unataka Kuuona Mji Huru wa Kwanza wa Kiafrika Barani Amerika? Nenda nchini Mexico

Statue of Gaspar Yanga. Photo by Erasmo Vasquez Lendechy via Wikipedia. Used under a Creative Commons license

Sanamu ya Gaspar Yanga. Picha na Erasmo Vasquez Lendechy kupitia Wikipedia. Imetumiwa kwa makubaliano ya Hati miliki ya Creative Commons

Makala hii kwa mara ya kwanza ilichapishwa kwenye blogu ya Lupitanews.

Inaitwa Yanga. Katikati ya uoto uliofungamana huko Kaskazini mwa Veracruz, jimbo linalopakana na  Ghuba ya Mexico, mji wa Yanga ni kiashiria cha uwepo wa makazi ya Waafrika huko Mexico.

Tukiwa tunaelekea  kwenye bandari ya Veracruz, tulisimama mjini Yanga ambapo tuliona mashamba ya kilimo yaliyosheheni caña pamoja na mahindi kila mahali, pia yalionekana mashamba makubwa ya kahawa; hali ya hewa ya kitropiki inakufanya uendelee kukaa nje ili kuliota jua.

Yanga inaaminika kuwa ndio mji huru wa kwanza wa Waafrika huko Amerika ulioanzihwa rasmi Oktoba 3, 1631. Waafrika-Wa-Kimexico wanajivunia kuwa sehemu ya simulizi ya “El Yanga,” aliyejulikana dhahiri kama Mfalme aliyekuwa mateka kutoka katika kabila la Yang-Bara la Gabon, ambaye aliwasaidia watumwa kuwa huru kutoka kwa  Waspaniola kwenye miaka ya 1570.

Moja ya eneo la soko imewekwa sanamu yake, inamtambulisha El Yanga kama mmoja wa watu wajasiri na wa kujivunia.

Masoko makuu,  malango pamoja na kanisa kuu hufafana kabisa na yale yaliyopo kwenye miji mingine ya Mexico na ambayo huleta hamasa ya utulivu na matembezi ya raha yasiyo na bugudha. Mji wa Yanga ni wa amani na unatoa imani kwa ustawi mkubwa wa wakazi. Karne nyingi na watu wengi wameishi na wameshakufa wakiwa hapo, Many centuries and people have lived and died there, pengine hii ikiwa ni dhahiri katika historia, lakini bado wao wenyewe wanaendelea kuweka historia.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.