Picha za Kusikitisha za Watoto wa Kifilipino Wanaofanya Kazi Migodini

child labor sacadaHali ya utumikishaji wa watoto nchini Ufilipino inazidi kushamiri. Mwaka 2011, Ofisi ya Takwimu ya Ufilipino ilitaarifu kuwa kulikuwa na watoto milioni 5.5 waliokuwa wakitu mikishwa, miongoni mwao, milioni 2.9 walikuwa wakifanya kazi kwenye viwanda vilivyo hatari kwa afya yao kama vile vya migodi na mashamba makubwa. Taasisi hii ya serikali iliongeza kuwa, watoto 900,000 walisitisha msomo kwa ajili ya kwenda kufanya kazi.

Idadi hii inaashiria hali tete inayowakabili watoto wengi wa Ufilipino, ambao wanakosa mahitaji muhimu ya kijamii pamoja na kukosa kuthaminiwa.

Ufilipino ni moja ya nchi iliyoingia mkataba wa Makubaliano kuhusu Haki za Mtoto pamoja na kwenye t mashirika mengie ya kimataifa yaliyo na malengo ya kulinda mustakabali wa watoto. Pia, kuna mkakati maarufu wa kuwa na serikali inayowajali watoto, husani kwa maeneo ya vijijini. Hata hivyo, sheria hizi pamoja na mikakati hii bado haijafanikiwa kutokomeza aina mbalimbali za uonevu, umasikini na hali ya kukosa malazi na chakula kunakowakabili watoto wengi.

Mwezi uliopita, Taasisi ya Kidini ya Tafiti za Elimu ya Ajira(EILER) ilitoa taarifa ya utafiti msingi ambao ulithibitisha kuendelea kuwepo kwa utumikishwaji wa watoto migodini pamoja na kwenye mashamba makubwa katika maeneo mbalimbali nchini Ufilipino. Kwenye jamii za watu wanaohusika na mahsmba makubwa, takribani asilimia 22.5 ya makazi ya watu yana watoto wanaofanya kazi katika mashamba hayo. Kwenye maeneo ya migodi, matukio ya watoto kufanyishwa kazi yalionekana kwa asilimia 14.

Kwenye mashamba ya miti ya mafuta ya michikichi, mara nyingi watoto hufanyishwa kazi za kupanda, kuvuna, kupakua, kupakia pamoja na kung’oa mimea. Kwa upande mwingine, watoto wanaotumikishwa katika mashamba ya miwa hufanya kazi za palizi, kuvuna pamoja na kuchota maji.

child labor hacienda

child labor plantation

child labor negros

Kwenye migodi, watoto hutumikiswa kwenye kazi kama vile za kuchota maji, kubeba viroba vya udongo, au kukusanya magogo manene kwa ajili ya kuimarisha njia za ardhini, au wanaweza kuwa wajakazi wa wafanyakazi wazoefu wa mgodini. Pia, watoto huwa ni wafanyakazi wa ziada na “wapokezi” hususani pale wachimbaji madini wa kudumu hawatafika kazini. Watoto wa kike kwenye migodi hufanya kazi ya kuchambua dhahabu au kutoa huduma anuai kwa wachimbaji madini kama vile kuwafulia nguo au kuwapikia chakula.

child labor mining

child labor bicol

child labor gold mining

EILER iligundua kuwa, watoto wanaotumikishwa hufanyishwa kazi kwenye hali mbaya ya hewa, kufanya kazi kwa muda mrefu sana na kwenye mazingira magumu huku wakitumia zana na vifaa vya kufanyia kazi ambavyo ni duni.

Kwenye mashamba makubwa, magari huwachukua watoto kutoka majumbani kwao na kuwapeleka kujenga mahema karibu na maeneo ya miji na kasha huishi humo wakifanya kazi kwa vipindi vya kati ya wiki mbili hadi mwezi mmoja na bila ya kuwa na wazazi wao.  Kwwa kuwa mashamba mengi makubwa hutumia viuatilifu, watoto wanaofanya kazi katika mashamba haya huwa katika hatari kubwa ya kuathiriwa na viuatilifu hivi.

Wenzao wanaofanya kazi kwenye migodi, wakati huo huo, huwa wanatumia vifaa ambavyo ni hatari na wanafanyishwa kazi kwa muda mrefu na bila ya kuwa na vitu vya kuwakinga na hatari mbalimbali. Matumizi ya vitu hatarishi kwa jamii kama vile madawa ya kulevya ya kuwafanya watoto waingie migodini   na kufanya kazi kwa muda mrefu ni mambo ya kawaida kwenye migodi.

Pitang holding a placard which reads: "I am a child laborer". Photo from Facebook page of Jhona Ignilan Stokes

Mtoto akiwa amebeba bango linalosomeka: “Mimi ni mtoto inayefanyiPitang holding a placard which reads: “I am a child labourer”. Picha kutoka Ukurasa wa Facebook wa Jhona Ignilan Stokes

Pitang, kutoka Mindanao, ambaye ni mmoja wa watoto waliokuwa wakitumikishwa aelezea uzoefu wake wa kufanya kazi kwenye mashamba makubwa wakati wa mijadala ya wazi iliyoandaliwa na EILER:

Niliacha kwenda shule nikiwa na umri wa miaka 10. Nilishapoteza tumaini la kuwa siku moja nitarudi tena shuleni, na nilifikiri kuwa mwimbaji badala yake. Mara nyingi huwa napenda kuimba kama namna ya kukabiliana na kusahau hisia za maumivu na uchovu niliokuwa nikiupata katika mashamba makubwa. Ni miaka mine sasa imepita tangu nilipoacha shule. Niliweza kufika darasa la sita peke yake na hapo nililazimiaka kuachana na masomo ili nikafanye kazi.

Kwa bahati nzuri, yamekuwepo makundi kama vile EILER yanayoendesha kampeni ya kukemea aina mbalimbali za utumikishwaji wa watoto nchini Philippenes. Moja ya miradi yao ni Balik-Eskuwela (Rudi shuleni) ambao una lengo la kuwarudisha mashuleni watoto wanaotumikishwa. Umoja wa Ulaya ni moja ya  washirika  wa EILER katika mradi huu.

Child workers return to school. Photo from Facebook page of Balik-eskuwela

Watoto wanaofatumikishwa kazi warudi shuleni. Picha kutoka ukurasa wa Facebook wa Balik-eskuwela

*Picha zote kutoka EILER, na zimetumiwa kwa ruhusa

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.