Hadithi ya Mapenzi Kibera

Hii ni hadithi ya kusisimua ya mapenzi kati ya Sam, anayetoka Kibera, makazi ya masikini kwenye jiji la Nairobi, Kenya, na Alissa, anayetoka Minnesota, Marekani:

Bila shaka, hii ni hadithi ya mapenzi isiyo na kifani mwaka huu!!! Alissa anatoka Minnesota, huko Sam alizaliwa na kulelewa Kibera. Ilikuwaje ‘njiwa hawa wa mapenzi’ wakakutana?

Alissa alikuwa amekuja Kenya, na kwa muda wa miezi kadhaa, alikuwa anafanya kazi na watu wanaoishi Kibera. Kwa miezi kadhaa, akitumia Matatu (usafiri wa umma) kurudi nyumbani, alimwona Sam, kijana mwenye kipaji, aliyekuwa na kibanda cha ‘vito’ vya kiafrika pembeni mwa barabara. Siku moja, Sam alipokuwa akila ndizi pembeni mwa duka lake, akamwona msichana mrembo mzungu amekaa kulia mwa Matatu. Alishangazwa na kile alichokiona na akaamua kutumia shilingi tano zilizokuwa zimebaki mfukoni kumnunulia ndizi pia. Kwa hivyo akamwomba dada aliyekuwa kibandani ampe ndizi nyingine, nia yake ikiwa kumpatia mrembo yule mzungu ndizi hiyo. Bahati haikuwa yake, kwa sababu alipokaribia dirisha la upande ambapo msichana alikuwa amekaa, matatu ikaondoka kwa kasi. Akaikimbilia, lakini tayari alikuwa amechelewa. Matatu iliondoka ikiwa imembeba msichana wa ndoto zake.

17 maoni

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.