Uchambuzi zaidi Kuhusu Muswada wa Kupinga Ushoga Nchini Uganda

Kristoff Titeca anaangalia mbali zaidi ya sababu moja kuhusiana na muswada wa kupinga ushoga nchini Uganda:

Pointi muhimu ni kuwa Rais Museveni hajawahi kuwa shabiki mkubwa wa muswada huu na badala yake amekuwa mtu wa kuutilia mashaka: alikuwa anafahamu matokeo mabaya kimataifa. Katika majibu yake ya wazi kwa mara ya kwanza baada ya muswada huu kuletwa, alisema muswada huu “haukuwakilisha sehemu ya msimamo wa serikali” na namna “Uganda isivyoweza kuwa tayari kuhatarisha sera yake ya mambo ya nje kwa kuruhusu muswada huu kupia ukiwa katika sura iliyopo”. Mwaka unaofuata, muswada ulififia na ukawekwa kapuni, (mwaka 2009, 2011 na 2013), mpaka ulipoonekana tena Desemba 20, 2013, ulipopitishwa na bunge.

Baada ya kupitishwa, Museveni aliendelea kuwa na msimamo usioeleweka: alidai imekuwaje muswada upitishwe bila yeye kujulishwa, na kwa haraka kiasi kile, tena na idadi ndogo ya wabunge wakiongozwa na spika Kadaga. Kufanya hivyo kulimlazimu kulitazama suala hili kwa kina zaidi. Katika mahojiano yake pamoja na matamko, Museveni mara zote alikuwa amejikita katika masuala mawili: Kwenye ufundishaji wa watu kuwa mashoga (na linalofanana na hili, ni, wale wanaofundishwa, wale ambao wanageuka kuwa mashoga kwa sababu za kibiashara) na pili, kuonyesha hadharani tabia ya ushoga. Katika kufanya hivyo, aliacha upenyo, kuwa kuna uwezekano wa kuwa watu fulani wanazaliwa mashoga (…) tabia zisizo za kawaida kwa binadamu na zinazotokea mara chache. Katika kufanya hivyo, angeweza kuwaridhisha wananchi wake wa ndani -aliwakosoa mashoga – lakini na watu wa nje, kwa kuacha upenyo wazi. Kwa mfano, hata baada ya kutangaza kwamba ataenda kusaini muswada huo, kama majibu baada ya Obama kumkosoa, Museveni alidai kuwa anaiomba Marekani utoe ushahidi kuwa kuna watu wanazaliwa mashoga, hatua ambayo ingemwezesha kuipitia upya sheria hiyo.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.