Namna Shambulizi la Westgate Jijini Nairobi Lilivyojadiliwa Kupitia Mitandao ya Kijamii

Shurufu ni mwandishi wa Kitanzania anayeishi jijini Dar es Salaam. Anatwiti kupitia@shurufu. Unaweza kusoma posti yake Mwandishi wa Global Voices Awakumbuka Marafiki Waliouawa Kwenye Shambulio la Westgate.

Kwa muda mfupi, kila kitu kilibadilika. Tarehe 21 Septemba, 2013, kikundi cha wanajeshi wenye silaha walivamia kituo cha biashara jijini Nairobi, mji mkuu wa Kenya, walimimina risasi, wakiua watu wanaosemekana kufikia 69 na kujeruhi mamia.

Mtandao twita ulikuwa na taarifa za shambulio hilo katika muda halisi tangu watumiaji walivyoripoti awali kile walichodhani ni mlipuko. Baada ya saa za mchana kupita, habari zilianza kuenea kupitia mitandao ya kijamii kwamba hali ilikuwa mbaya sana kwenye kituo cha kibiashara cha Westgate, eneo moja wapo maarufu kwa wageni na wa-Kenya wa tabaka la kati.

Ma Bradley (@NyamburaMumbi) alitwiti:

mlipuko kwenye maduka ya westgate…. inasikitisha namna gani?

Ndani ya dakika chache baada ya habari kusambaa, hata hivyo, haikuwa imejulikana wazi, kwa hakika, nini hasa kilikuwa kimetokea. Naporneon Pornaparte (@aCreole) alitafakari hali hii ya kutokuwa na uhakika wa mambo kupitia twiti yake ifuatayo:

Mlipuko au ni risasi? “@NyamburaMumbi: mlipuko kwenye maduka ya westgate….inasikitisha namna gani?

Kwa baadhi, eneo hasa la tukio hilo lililoripotiwa, halikuwa bayana. Ramsy Ama Ramah (@ramjanja) alidhani kuwa taarifa za mwanzo zinazodai kuwa mlipuko umetokea eneo la Westgate zilikosewa:

mlipuko umetokea Mathare na sio Westgate

Baada ya muda mchache, hata hivyo, ilikuwa bayana kuwa kuna jambo lisilo la kawaida linaendelea kwenye kituo kicho cha kibiashara cha Westgate. Uthibitisho wa hali hii ulikuwa baada ya Wizara ya Mambo ya Ndani kutwiti habari hii mpya:

Tunawasihi wa-Kenya kukaa mbali na kituo cha Westgate kilichopo Westlands mpaka itakapotangazwa vinginevyo

Kilichokuwa kinaanza kuwa wazi katika mtandao wa twita ni kwamba watu wenye silaha walikuwa wameingia ndani ya majengo ya Westgate, mwandishi wa habari

KAENI MBALI na Jengo la Westgate -watu wenye silaha kali wanapiga risasi hovyo ndani. Wafahamishe wanafamilia na marafiki zako kutokufika kwenye eneo hilo.

Inspekta Jenerali wa Polisi David Kimaiyo kupitia ukurasa wake wa twita(

Tafadhali msisogelee eneo la Westgate, Westland. Polisi wamelizingira eneo hilo.

Pamoja na habari hizi mpya kutoka kwenye vyombo vya dola, kile hasa walichokuwa wakikishughulikia kilibaki kuwa utata, hata kwao, angalau kupitia kile walichokuwa wakikisema hadharani, kama ilivyowekwa wazi na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani Mutea Iringo kupitiakauli yake kwa waandishi:

Tumefanya upepelezi wa anga. Tumethibitisha kuwa kuna wahalifu wenye silaha lakini hatujaweza kuthibitisha ni akina nani hasa. Tuwape nafasi @PoliceKE wafanye kazi yao

Lakini vyanzo vingine ndani ya polisi ya Kenya vilianza kugundua kuwa walichokuwa wakipambana nacho ni zaidi ya ujambazi wa kutumia silaha. Hapa ni Robert Alai (@RobertAlai), mmoja wa watu wa mwanzo kuarifu kwamba kulikuwa na kitu cha ajabu kinaendelea:

Raia wengi wa kigeni na wenyeji wengi wameuawa kwa kupigwa risasi kwenye Shambulio la Westgate. Huu sio ujambazi wa kutumia silaha [kama ilivyodhaniwa] -Chanzo kilichomo ndani ya Jeshi la Polisi

Baada ya picha kamahizi zilipoanza kusambaa mtandaoni, ilikuwa wazi kwamba kilichokuwa kinaendelea Westgate ni kitendo cha kigaidi:

Usizitazame kama usingependa kufanya hivyo

Nani yuko nyuma ya shambulizi la Westgate?

Ilipotimu saa 5 usiku, Rais Uhuru Kenyatta alilihutubia taifa na kuthibitisha kwamba kilichokuwa kinaendelea huko Westgate, kilikuwa, kwa hakika, ni shambulio la kigaidi. Kupitia kituo cha televisheni cha KTN:

Bw. Kenyatta alionekana mwenye uso wa huzuni nyingi naaliwafahamisha watu wake uovu wa kile ambacho Kenya ilikuwa inakumbana nacho:

Asubuhi ya leo, kikundi cha magaidi wenye silaha waliingia kwa nguvu kwenye kituo cha kibiashara cha Westgate kwenye eneo la Parkland, jijini Nairobi na kusababisha ghasia zisizo za kiungwana kwa wateja na wafanyakazi. Wameua watu wasio na hatia wapatao 39 na kujeruhi zaidi ya watu 150. Kwa niaba ya taifa lote, ninaungana na familia za wale waliopoteza maisha yao na kuwapa rambirambi za kila raia wa Kenya kwa kilichotokea.

Baadae, iliripotiwa kwamba naye pia alikuwa miongoni mwa waliopoteza wapendwa wao:

Kwa mujibu wa taarifa, mpwa wa rais, Mbugua na mchumba wake Wahito, waliuawa kwa risasi wakati wa shambulio hilo na kwa maelezo ya walioshuhudia tukio hilo, Mbugua alikuwa amefanikiwa kutoka kwenye jengo hilo na baadae aligundua kuwa mchumba wake alikuwa bado yumo kwenye jengo. Alirudi haraka kwenye jengo kumchukua ndipo alipopigwa risasi akiwa na mchumba wake.

Pamoja na uthibitisho kuwa shambulio la Westgate lilikuwa la kigaidi, haikuwa bayana nani hasa alilipanga.

Katika tamko lake kwa taifa, Rais Kenyatta hakutaja kuhusika kwa kikundi chochote. Lakini baadae, anuani ya twita inayoaminiwa kuendeshwa na Al-Shabaab, kikundi cha Kiislam cha Kisomali, kilidai kuhsuika na shambulio hilo. Anuania hiyo imesimamishwa tangu wakati huo, lakini madai yao yamewekwa kwenye habari za Storify za mtandao wa Canoe News. Robert Alai aliweza kupata picha ya ukurasa huo unaodaiwa kumilikiwa na Al-Shabaab kabla haujaondolewa:

#AlShabaab sasa wanasema kwamba wataweka video ya Shambulio la Westgate

Ni kweli, masaa kadhaa baadae, kipande cha video kwenye mtandao wa YouTube kinachodaiwa kuwekwa na Al-Shabaab kiliwekwa mtandaoni. Video hiyo iliyokuwa na maneno makali na ya kidini, ilikuwa na ujumbe ulikuwa wazi:

Baadae, kikundi cha Wanazuoni wa Kiislamu walijibu kwa hasira madai hayo ya wanamgambo wa Al-Shabaab kwamba matendo yao yalifanywa kwa kutumia jina la Uislam. Jukwaa maarufu la mtandaoni la Naijeria, Nairaland, lilimnukuu Sheikh Abu Eesa Niamatullah, akipinga kile alichokiita kuifanya damu ya raia wasio na hatia kuwa bidhaa ya bure. Aliendelea kwa kusema,

Hamjawahi kugusa chochote isipokuwa kukiharibu, hamjawahi kulitumikia kusudi halali isipokuwa kulighoshi, hamjawahi kudhamini upekee wa maisha ya mwanadamu isipokuwa kuyakatisha, hamjawahi kufanya kitu kwa jina la Uislamu isipokuwa kuuchafua.

Kwa hiyo ni kwa nini wakati huo, Al-Shabaab?

Ujasiri wa shambulizi hizi umefanya baadhi ya watu kudhani linaweza kutengeneza sura mpya kwa wa-Islamu wa Kisomali.

Mwezi Agosti mwaka huu, mchambuzi Abdihakim Ainte (@Abdikhakim) anayeandikia tovuti ya Al-Monitor alidhani kuwa kuzidiwa nguvu kwa kikundi hicho nchini Somalia na majeshi ya Uganda na Kenya kumekilazimu kubuni mbinu mpya ya kigaidi kufanya vita. Anasema:

Katikaujumbe wa sauti wa hivi karibuni, Ahmed Godane, kiongozi mkuu wa operesheni za al-Shabab, aliweka wazi kwamba alikuwa amekusudia kubadili mbinu za operesheni zake. Hiyo ilikuwa ni pamoja, kama anavyosema yeye, na mipango ya kuingiza kizazi kipya kinachoweza kuendana na vita vya Jihad vinayobadilika kwa kasi. Tofauti na al-Shabab 1.0, al-Shabab mpya inaweza kuwa na wapinganaji wapi -hasa vijana, chini ya miaka 30, ambao wanayafahamu vyema mataifa ya Magharibi na wanafahamu vyema lugha za kigeni, kuweza kusukuma mbele mapambano hayo kwa vizazi vijavyo. Hili linaonekana kuwa bayana katika video mpya iliyotolewa na al-Shabab ikiwaonyesha vijana watatu wa ki-Somali waliouawa wakati wa vita. Video hiyo iliyopewa jina la “Njia ya kwenda Ahera: Kutoka Majiji Pacha kwenda Nchi ya Kuhamia” ni sehemu ya ujumbe wa propaganda zinazokubalika na Al-Qeda kushawishi kizazi kipya.

Wakati huo huo, Ken Menkhaus katika tovuti ya Think Progress alikubali kwamba Al-Shabab imedhoofishwa kwa hakika. Menkhaus aliendelea kusihi kwamba karata hii ya hivi karibuni iliyochezwa na kikundi hicho ilikuwa ni jaribio la kutengeneza upya vigezo na masharti ya mgogoro unaoendelea Somalia:

Shambulio la Westgate ni dalili ya hivi karibuni ya udhaifu wa kikundi hicho. Ilikuwa ni karata ya kukata tamaa, isiyo na uhakika iliyochezwa na Al-Shabaab kujaribu kurudi kwenye malengo yake. Kama shambulio hilo baya litafanikiwa kuibua vurugu baina ya raia wa Kenya au hatua nzito za serikali dhidi ya wa-Somali, basi Al-Shabaab itakuwa na nafasi ya kujitengenezea picha ya kikundi cha kijeshi kinachowalinda wa-Somali na maadui wa nje. Kikundi hicho kinahitaji kutengeneza upya sura ya mgogoro wa Somalia kama vita ya wa-Somali na wageni, na sio wa-Somali wanaotafuta amani na kurudi kwenye maisha ya kawaida didi ya harakati za kikatili za Jihad.

Kwenye mtandnao wa twita, Charles Onyango Obbo (@coboo3) hakukubaliana na hilo, akisema kwamba shambulizi hilo linaonyesha kukua kwa kikundi hicho cha Al-Shabaab:

Nimependa mawazo yako, ingawa kwa mtazamo wangu ni kwamba Al-Shabaab inapanuka na kuwa kikundi cha kigaidi katika eneo hili la Afrika, na wala sio kusambaratika.

Namna nyingine ya mtazamo huu ilisikika katika uchambuzi wa tovuti ya Somalia Newsroom, ilisema kwamba shambulio la Westgate lilikuwa ni shambuli la kisasi lisilokwepeka kufuatia operesheni ya Kenya inayoendelea Somalia. Kwa nyongeza, walibainisha kuwa, kutokuwepo kwa mpango mkakati wa muda mrefu wa namna ya kupambana na ugaidi nchini Kenya unaweza kueleza sababu ya kuendelea kwa nguvu ya Al-Shabaab:

Serikali ya Kenya inaweza kupata mafanikio katika kupambana na ushawishi wa Al-Shabaab na wanaowaunga mkono kwa kujenga daraja kati ya jamii na sio kutafuta mchawi, kutoa misaada kwa jamii zisizopata msaada ili kuwatumikia vijana na familia, na kuchukua hatua mpya makini na uwajibikaji kwa vitendo vinavyofanywa na vikosi vya kijeshi kwa raia wa kawaida.

Wakati mbinu za sasa za Kenya kuwadhibiti al-Shabaab zimekuwa na mafanikio kadhaa, hata hivyo zimesababisha hali ya tahayaruki kwa wa-Somali na zimeacha mapungufu mengi yasiyoshughulikiwa huko nyumbani. Badala ya kushuhulikia shambulizi la Westgate kwa hasira za kipofu, Kenya lazima itafakari na kujibu kwa upole maswali halisi yanayoikabili katika kujaribu kuongeza hali ya usalama nyumbani na nje ya mipaka.

Hakuna mashaka kwamba, kadri muda unavyoendelea, tafakuri na chambuzi zaidi zinafuatia katika kujaribu kutafakari matukio ya kutisha ya Septemba 21.

Soma pia: Mwandishi wa Global Voices Akumbuka Kuuawa kwa Marafiki katika Shambulio la Westgate.

1 maoni

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.