Mnamo Machi 27, mjadala mkali uliibuka kwenye mitandao ya kijamii ya Kenya juu ya matamshi yaliyotolewa hewani na watangazaji wa redio tatu wakati wa kipindi cha asubuhi “Breakfast Show”. Watangazaji walikuwa wakijadili kesi inayoendelea ya kortini inayomshirikisha Eunice Wangari, mwanamke ambaye alisukumwa nje ya jengo la ghorofa 12 na mwanamume ambaye alikuwa na mahusiano naye.
Kwenye mtandao wa Twitter, Wakenya wenye hasira waliwaghadhabisha watangazaji Shaffie Weru, Joseph Munoru, na Neville Muysa kwa matamshi yao juu ya kesi ya madai ya unyanyasaji wa kijinsia, na kuwaita watangazaji hao wahanga-wa-kulaumu.
Shaffie is insinuating that the lady who was pushed from the 12th floor of a building in Nairobi CBD after she said no to a man's advancements was because she was too loose & very available hence putting herself is such a situation. Homeboyz yawa. What the actual hell! ?
— BRAVIN YURI (@BravinYuri) March 25, 2021
Shaffie anasisitiza kwamba mwanamke huyo alisukumwa kutoka gorofa ya 12 ya jengo jijini Nairobi baada ya kusema hapana kwa mwanamume ni kwa sababu alijiachia sana na kuwa huru kwa hivyo kujiweka mwenyewe katika hali kama hiyo. Homeboyz yawa. Je! Ni kuzimu gani!
Kesi hii imegawanya watumiaji wa mitandao kwani kuna baadhi yao wanakubaliana na watangazaji hao. Ingawa watatu hao walifukuzwa kazi na kituo hicho cha redio, ilileta wazi jinsi uhasama wa nafasi mkondoni ya Kenya imekua kwa wanawake.
Kuna takribani watumiaji 21.75 milioni wa mitandao nchini Kenya, au asilimia 40 ya idadi ya watu nchini kulingana na utafiti wa data uliofanywa na kampuni ya DataReportal mwaka 2021. Karibu watu milioni 11 ni watumiaji ya mitandao ya kijamii, ongezeko la asilimia 2.2 ukilinganisha na mwaka 2020.
Kutokana na ripoti nyingine ya Mfumo wa kimataifa wa mawasiliano ya simu (GSMA), idadi ya umiliki wa simu za mikononi ni karibu sawa kwa wanawake na wanaume ikiwa na tofauti ya asilimia tano zaidi kwa wanaume wanaomiliki au wenye uwezo wa kupata vyombo vya mawasiliano ukilinganisha na wanawake, kwenye watumiaji watatu wa mitandao nchini Kenya mmoja wao ni mwanamke.
Kama wachache mkondoni, mara nyingi wanawake nchini Kenya wamekua lengo la uonevu wa kimtandao. Na ingawa mwaka 2018 sheria dhidi ya unyanyasaji wa kimtandao ilipitishwa nchini – ambayo hufafanua tabia kama kushirikiana na wengine kwa njia ambayo “inaweza kusababisha… wasiwasi au hofu ya vurugu kwao au uharibifu au upotezaji wa mali ya watu hao”… kwa adhabu ya hadi miaka 10 jela, bado uonevu wa watu wengi mtandaoni bado imekithiri sana.
Hapa chini tutaeleza matukio mwengine maarufu mawili iliyojitokeza mizi 12 iliyopita ambayo mitandao ya kijamii imetumika kama jukwaa la kunyanyasa wanawake nchini Kenya.
Mgonjwa wa COVID-19
Mnamo Machi 2020, Brenda Iyv Cherotich alikua mgonjwa wa kwanza wa COVID -19 nchini Kenya. Baada ya kupona alikuja na kuelezea juu ya safari yake wakati ulimwengu ulipoanza kuelewa kuhusu kirusi hiki kipya.
Lakini Cherotich hakupokelewa kwa uchangamfu kama alivyotarajia. Baada ya kufanya mahojianona vyombo vya habari mwezi April 2020, alikabiliwa na unyanyasaji na usumbufu mtandaoni kutoka kwa “Kenyan On Twitter” (maarufu kama #KOT neno linalotumika mara nyingi kuelezea watumiaji hai wa mtandao wa twitter nchini Kenya wanaoshiriki kwenye mijadala mbalibali au haiba kwenye mtandao huo) ambao walitafuta kudhalilisha na kuuliza ukweli kuhusu hadithi yake.
Wanyanyasaji wengine wa mtandaoni waliingilia maisha yake binafsi, mazungumzo yake binafsi na picha zake zilisambaa sana mtandaoni, pengine baada ya kuvujishwa na rafiki yake au mtu wake wa karibu.
her hairstyle looks like Corona itself ????#brenda @indukusy pic.twitter.com/q3HsQxkcfw
— this is me?? (@mykdjmaliq) April 1, 2020
Mtindo wa nywele zake zinaonekana kama Corona yenyewe
Baada ya kukasirishwa kwa hili, waziri wa afya wa Kenya Mutahi Kagwe alijitokeza kumtetea Brenda, kutoa wito wa kukamatwa kwa wanyanyasaji hao na kuwataja kama “jitihada za aibu zinazodhoofisha juhudi za serikali za kupambana na COVID-19.”
Health CS Mutahi Kagwe tells police to arrest social media users for bullying Brenda pic.twitter.com/YkI5EMfeaM
— Nairobi News (@Nairobi_News) April 3, 2020
Waziri wa afya Mutahi Kagwe akiwaambia polisi kuwatia hatiani watumiaji wa mitandao ya kijamii kwa kumnyanyasa Brenda
Na hiyo haikuwa mwisho wake, mwathirika mwingine hivi karibuni alianguka kwenye shambulizi la #KOT: Mtangazaji wa runinga Vyonne Okwara alilengwa baada ya kumtetea Brenda na kumuunga mkono hoja ya waziri ya kuwatia hatiani wanyanyasaji wa mitandao.
I strongly disagree with Yvonne Okwara. Your statement is not objective. It is emotional and stinks to high heavens. Speaking of which where was your voice when your fellow women stripped a MAN (Lonyangapuo) naked and shared his nude photos? This is toxic
pic.twitter.com/mqXDt0GkAK— Lord Abraham Mutai (@ItsMutai) April 3, 2020
Sikubaliani kabisa na Yvonne Okwara. Taarifa yako haina tija. Ni ya kihemko na yenye kunuka hadi mbingu za juu. Sauti yako ilikuwa wapi wakati wanawake wenzako walimvua MWANAUME (Lonyangapuo) uchi na kushiriki picha zake za uchi? Hii ni sumu
Okwara aliwakosoa wanyanyasaji kwa kulenga wanawake. Alisema kuwa Brian Orinda, mwathirika watatu wa COVID-19, aliekuwepo alipotoa safari yake ya kupona pamoja na Brenda, hakupata muitikio sawa. Hii ilichochea vidole vya wapambanaji wa kibodi kuwasha ambao walikuwa na siku yao kwenye mtandao wa Twitter wakimshambulia Okwara.
Playing gender card everytime. Women should safeguard their dignity in the first place. Posing for such photos and sharing the same is equally immoral
— Saadiq-Al Amin (@Saadiq77) April 3, 2020
Utumiaji wa kadi ya kijinsia muda wote. Wanawake wanatakiwa kulinda heshima wao kwanza. Kupiga picha kama hizi na kuzishiriki vile vile ni ukosefu wa maadili.
Kind of shallow and idiotic take from Okwara. So shallow, you wonder if Corona ate the brain.
Nudes of men were online juzi. She suddenly has selective amnesia over that.
— Robert Alai, HSC (@RobertAlai) April 3, 2020
Hali hiyo duni na ya kijinga kutoka Okwara. Kwa hivyo duni, unashangaa kama Corona alikula ubongo.
Uchi wa wanaume ulikuwa mtandaoni juzi. Yeye ghafla amepata usahaulifu kwa kuchagua juu ya hiyo.
Mwanzoni mwa mwaka, msemaji mkuu wa Ikulu Kanze Dena pia aliathirika na unyanyasaji wa kimtandoa wa Kenya. Alipokua akitoa mkutano na waandishi wa habari kwenye hafla, wanyanyasaji wa mtandao waliudhalilisha mwili wake kutokana na uzito wake.
Kwa haraka ikawa mjadala kwenye mitandao ya kijamii, na sehemu ya Wakenya na haiba ya media wakimtetea Dena.
She’s too fat, tall,short! Who set standards for how women should look like?Why is it our problem that @KanzeDena has added some weight? Well, she’s a new mother, but, she owes no one an explanation! #HerBodyHerChoices! Give her a break please! This is a new low we must reject ? pic.twitter.com/x7qP3nuPeS— Patience Nyange (@NyangePatience) January 29, 2021
Yeye ni mnene sana, mrefu, mfupi! Ni nani aliyeweka viwango vya jinsi wanawake wanavyopaswa kuonekana? Kwa nini ni shida yetu kwamba @KanzeDena ameongeza uzito? Kweli, yeye ni mama mpya, lakini, hana deni kwa mtu yeyote! #HerBodyHerChoices! Mpeni pumziko tafadhali! Hii ni chini mpya lazima tuyakatae
View this post on Instagram
Makala ya The Elephant, moja ya chapisho kuu la kidijitali nchini Kenya, ilibaini kuwa nyanja za mtandao wa kijamii mkondoni nchini Kenya na ulimwenguni zimegeuka kuwa mipaka ya maneno yenye sumu na unyanyasaji.
There is no gainsaying that social media has become an important tool for social and professional advancement, more so for women. Many women have built their businesses online and, in the process, have learned how to connect with others. Many find clients to buy and sell their products online. Others find platforms to incubate ideas, leading to hundreds if not millions of social enterprises that not only spur economic growth but directly empower young men and women economically. They have also learned how to improve their entrepreneurship skills online. No doubt then, social media has emerged as a great space to do business. This is important for women’s economic empowerment and visibility. – Source: The Elephant
“Hakuna ubishi kwamba mitandao ya kijamii imekuwa nyenzo muhimu kwa maendeleo ya kijamii na kitaalam, zaidi kwa wanawake. Wanawake wengi wamejenga biashara zao mkondoni na, katika mchakato huo, wamejifunza jinsi ya kuungana na wengine. Wengi hupata wateja wa kununua na kuuza bidhaa zao mkondoni. Wengine hupata majukwaa ya kuwezesha maoni, na kusababisha mamia kama sio mamilioni ya biashara za kijamii ambazo sio tu zinazochochea ukuaji wa uchumi lakini zinawawezesha moja kwa moja wanaume na wanawake wadogo kiuchumi. Wamejifunza pia jinsi ya kuboresha ujuzi wao wa ujasiriamali mkondoni. Bila shaka basi, mitandao ya kijamii imeibuka kama nafasi nzuri ya kufanya biashara. Hii ni muhimu kwa uwezeshaji kiuchumi na kujulikana kwa wanawake” – Chanzo, The Elephant.
Inaonekana kwamba kwa wanawake kushiriki mazungumzo ya maana mkondoni juu ya mada zinazoathiri moja kwa moja maisha yao, mtandao lazima uwe mahali salama zaidi kuliko ilivyo sasa.