Rais Robert Mugabe ameshinda uchaguzi wa Rais nchini Zimbabwe ulifanyika Jumamosi ya Julai 31, 2013, akimbwaga mshindani wake wa karibu, waziri mkuu wa zamani katika serikali ya umoja wa kitaifa Morgan Tsvangirai.
Uchaguzi huo umekuwa wa amani kwa mara ya kwanza tangu kuanzishw akwa serikali ya pamoja kati ya chama cha Zanu PF cha Mugabe na chama kikuu cha upinzani kinachoongozwa na Tsvangirai kiitwacho Movement for Democratic Change (MDC). Serikali ya pamoja ilianzishwa kufuatia uchaguzi uliopita wa mwaka 2008 ulisemekana kuvurugwa mno na kusababisha umwagaji wa damu.
Mugabe, mwenye umri wa miaka 89 na ambaye amekuwa madarakani kwa miaka 33, ataendelea kuitawala nchi hiyo kwa miaka mingine mitano. Waangalizi wa uchaguzi huo kutoka Umoja wa Afrika (AU) na Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Afrika ya Kusini (SADC) wameunga mkono uchaguzi wa Mugabe pamoja na madai ya udanganyifu mkubwa yanayotolewa na upinzani.
Botswana, hata hivyo, ni nchi pekee ya Afrika iliyotoa wito wa ukaguzi huru wa uchaguzi huo. Baadhi ya wnaachama wa SADC wamethibitisha kuyaunga mkono matokeo hayo kwa kudai kuwa uchaguzi ulikuwa huru “lakini si lazima uwe wa haki.”

Rais Robert Mugabe ni mtawala mzee kuliko wote barani Afrika. Picha imeruhusiwa kutumiwa na umma na serikali ya Marekani.
Uchaguzi ulifanyika pamoja na maandamano kutoka kwa washirika wa muungano wa Mugabe na raia wa Zimbabwe baada ya *Mugabe) kujitangazia mwenyewe kuwa Julai 31, 2013 ndiyo tarehe ya uchaguzi. Mahakama ya Katiba ilimwamuru Robert Mugabe kuitisha uchaguzi tarehe 31 Julai kufuatia kufanikiwa kwa maombi ya Jealousy Mawarire, mkurugenzi wa Kituo cha Uchaguzi na Demokrasia kwa eneo la Afrika ya Kusini (CEDSA).
Kwa kutumia alama habari #ZimElections, #ZimbabweDecides, #ZimDecides na #ZimbabweElections, watumiaji wa Twita kutoka sehemu mbalimbali za dunia walitoa maoni yao kuhusiana na ushindi wa Mugabe.
Mzambia anayeishi Uingereza na mwanzilishi wa CrossFire Radio, Mueti Moomba (@Muweight) alishangaa nani alimpigia kura mtawala huyo mzee wa miaka 89:
Kabla sijalala ninawaomba #wazimbabwe wote, ambao kwa akili zao timamu walimpigia kura mzee anayechungulia kaburi? #zimbabwedecides my foot
— mueti moomba (@Muweight) August 3, 2013
Mjasiria mali wa kijamii wa Zimbabwe Sir Nigel (@SirNige) hakukata tamaa:
Nilikumbushwa kwa mara nyingine tena kwmaba yapo mambo ninayo/tunayoweza kufanya baada #Uchaguzi wa Zimbabwe yaani kushiriki kwenye mchakacho kuanzia SASA #263Chat #Twimbos
— Sir Nigel (@SirNige) August 6, 2013
Andiva (@AndyAndiva) kutoka Kenya anakilaumu chama cha upinzani cha MDC kwa kushiriki uchaguzi uliovurugwa:
kwa nini MDC walishiriki kwneye uchaguzi huo wakijua kuwa ulikuwa umevurugwa tangu mwanzo? #Zimbabwedecides
— Andiva (@AndyAndiva) August 3, 2013
mwandishi wa Afrika Kusini na mshauri wa matangazo Thebe Ikafaleng (@ThebeIkafaleng) alimnukuu Tendai Biti, Katibu Mkuu wa MDC, aliwakejeli wale waliokuwa wakihoji uwepo wa watu milioni mbili waliokwisha kufa katika daftari la wapiga kura haukuathiri upinzani:
“Wanakiri kuwa kuwa watu milioni mbili waliokufa katika daftari la wapiga kura, lakini ‘kwa sababu wamekufa, hawawezi kupiga kura’.” Tendai Biti. #ZimbabweDecides.
— Thebe Ikalafeng (@ThebeIkalafeng) July 31, 2013
Uchaguzi wa Zimbabwe (@ZimElections) umeonyesha ukubwa wa tatizo la wapiga kura mfu:
asilimia 75 ya vitambulishi vya mpiga kura vilivyogunduliwa katika vituo vya kupigia kura kwenye mji wa Chegutu tangu Jumatano ya wiki iliyopita ni vya watu waliokwisha kufa siku nyingi. #ZimElections
— ZimElections2013 (@Zimelections13) August 6, 2013
rakim allah (@LDaviano) alitoa maoni kwenye suala hilo hilo la “wapiga kura wafu”:
Inaweza kushangaza sana kuwa na watu wengi waliokufa wakipiga kura zaidi ya wale walio hai
— rakim allah (@LDaviano) August 6, 2013
Azad Essa wa Al Jazeera(@azadessa) alihoji tathmini ya Umoja wa Afrika kwa uchaguzi huo:
Kuna vituo 9700 vya kupigia kura. AU [Umoja wa Afrika] walitembelea vituo 350. Je, hiyo ni sampuli inayokubalika kufanya uamuzi? #zimelections
— Azad Essa (@azadessa) August 3, 2013
Mwandishi wa Habari za Uchunguzi na Mtengenezaji wa filamu Stanley Kwenda (@stanleykwanda) alibainisha kuwa ushiriki wa polisi inawezekana uliwatisha wapiga kura wasio na uelewa:
#Zimbabwedecides kuhusishw akwa polisi kama & maafisa wa uchaguzi katika kuwasaidia wapiga kura wasio na uelewa inawezekana kuliwatisha wapiga kura hao
— stanley kwenda (@stanleykwenda) August 2, 2013
mfanya biashara wa Afrika Kusini Another_craig (@@Another_craig) alitwiti kuhusu taarifa ya mwanajeshi mwenye miaka 135 “aliyepiga kura” katika uchaguzi huo:
Kwa hiyo, inawezekana, mwanajeshi mzee wa miaka 135 kweli akapiga kura kwenye uchaguzi huo wiki iliyopita. Oh, ndio faida ya zoezi hili huru.
— Craig (@Another_craig) August 6, 2013
Akimjibu @Another_craig, mjasiria mali wa Afrika Kusini Sello Rabele (@sellorabs) alindaika kwamba anatamani kuwa mwanajeshi akikua:
@Another_craig @chrishartZA #Zimelections Ninataka kuwa mwanajeshi nikikua, yaani nikifikisha miaka 130
— Sello Rabele (@sellorabs) August 6, 2013
arnold chamunogwa (@chamunogwa) hakuonyesha kushangaa kuwa chama tawala kimeiba kura. Alishangazwa na suala jingine kabisa:
Haishangazi kwamba ZPF kiliiba kura lakini inashangaza kwamba MDC ndiyo imeshangazwa na kiwango cha wizi wa kura katika uchaguzi huo #Zimbabwedecides
— arnold chamunogwa (@chamunogwa) August 2, 2013
Akuzike Polela (@Mulengi) kutoka Zambia alibainisha kwamba Morgan Tsvangirai ana rafiki mmoja wa ki-Afrika:
Botswana inaongea neno tofauti kuhusu uchaguzi wa Zimbabwe. Morgan ana rafiki MMOJA wa Kiafrika mpaka sasa.
— Akuzike Polela (@Mulengi) August 6, 2013
Zimbabwean Kudzai (@shuestrait) ningependa kuwaona wa-Zimbabwe wanaoishi nchini humo wakiamua kile kilicho chema kwa ajili ya nchi yao:
Ni wa-Zimbabwe pekee wanaojua kile kilichochema kwa wa-Zimbabwe..Wakaazi wa Zimbabwe na sio watu wanaoishi nje na baadhi ya mawaziri kutoka Marekani au Uingereza..#ZimDecides
— kudzai (@shuestrait) August 5, 2013
Mkenya David Ogara (@david_ogara) alifanya hitimisho chungu kuhusu uchaguzi wa Afrika:
Kwa hiyo MUGABE mwenye miaka 89 ni Rais mteule wa Zimbabwe…..uchaguzi wa Rais hauna maana yoyote kwa Afrika……
— David Ogara (@david_ogara) August 2, 2013
1 maoni