Cairoobserver atoa wito [ar] kwa wakaazi wa Misri kupitia mtandao wa Facebook na Twita [ar] kufanya maandamano mbele ya majengo ya serikali, yanayohusika na mipango miji, kote nchini Misri kudai kusitishwa kwa kuharibiwa na kupotezwa kwa sura halisi ya kihistoria katika miji.
Jiji lenye minara elfu sasa ni jiji lenye nguzo elfu! Mji wa kihistoria ambao uliorodheshwa kama urithi wa dunia katika miaka ya 70 sasa unakabiliwa na uharibifu na kubadilika kila sifa yake na viongozi wanaishughulikia hali hii kama jiji lisilo rasmi lisilodhibitika tena
[…]Jiunge nasi Jumatano Juni 19, 2013, saa 05:00 ( Masaa ya Cairo) katika Maandamano mbele ya ofisi la Gavana wa Cairo