Washindi wa Tuzo za Kwanza za Uandishi wa Kiraia Nchini Ghana

Tumepata matokeo ya Tuzo za kwanza kabisa za Uandishi wa Kiraia nchini Ghana.

Mashirika na watu binafsi kumi na tatu walitunukiwa tuzo hizo tarehe 23, Machi 2013 kwa matumizi yao bora ya vyombo vya habari za kiraia kuandika maudhui na kutangaza kazi zao wakati washerehe za utoaji wa tuzo hizo nchini Ghana, ambazo zilihudhuriwa na Balozi wa Marekani nchini humo Gene A. Cretz. Mashindano hayo yalitayarishwa na Blogging Ghana, kikundi cha wanablogu na watumiaji wa zana za uandishi wa habari za kiraia wanaoandika habari za Ghana au kuhusu tajiriba (mambo wanayokutana nayo) nchini Ghana.

Tovuti ya Blogging Ghana inaonyesha wafuatao kama ndio washindi wa makundi mbalimbali kama yalivyoorodheshwa:

 1. Blogu bora ya Biashara na Uchumi-  eStock Analysis.
 2. Blogu bora ya Teknolojia – Techy-Africa.
 3. Blogu bora ya Shirika  –  AccraDotAlt.
 4. Blogu bora ya Burudani  – AmeyawDebrah.com
 5. Blogu Bora ya Uanaharakati – Adventures from the Bedrooms of African Women
 6. Blogu Bora ya Uandishi wa Habariza Kiraia – Circumspect
 7. Blogu Bora ya Masuala ya kimaisha – Ganyobinaa.com
 8. Blogu Bora ya Ubunifu, Fasisi, Hadithi Fupi, Ushairi  – Ganyobinaa.com
 9. Blogu Bora ya Picha – Dirisha la Ghana na Afrika – Nana Kofi Acquah
 10. Tuzo ya Mtu Maarufu anayeonekana zaidi kwenye Mitandao ya Kijamii – @mutomboDaPoet
 11. Tuzo ya Maudhui Bora Halisi - Kodjo Deynoo Poetry
 12. Blogu Bora- Adventures from the Bedrooms of African Women
 13. Tuzo ya Heshima kwa Kuwa Mfano wa Harakati Bora za Kiraia Mtandaoni – Ghana Decides

Kwa mujibu wa tovuti ya Blogging Ghana, mapendekezo yalitoka kwa watu 314, hiyo ikifanya mapendekezo kuwa 1,128 katika makundi zaidi ya 13. Idadi hiyo inafanya wastani wa mapendekezo yanayofikia 87 kwa kila kundi shindanishi.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

 • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.