Kenya: Kilimo cha Bustani Mijini Chashika Kasi

Nchini Kenya, wakazi wa mijini wameanza kujifunza mbinu anuai za kulima chakula kwa ajili ya matumizi yao na kuuza hata katika eneo dogo. Kwa watu wenye kipato cha chini au wale wasio nacho kabisa, kilimo cha bustani mijini chaweza kuwa sehemu ya suluhisho la kuwa na chakula cha hakika. Video hizi zinaonyesha namna ya kuotesha na kukuza mimea ya chakula kwenye vifaa vya kawaida kabisa tena kwa kutumia eneo na raslimali ndogo.

Kutoka kwenye filamu ya maisha halisi iitwayo God save the green(Mungu okoa kijani) iliyotayarishwa na Michele Mellara na Alessandro Rossi chini ya kampuni ya utengenezaji filamu ya Mammut Film Production unakutana na kipande hiki kifupi kinachohusu bustani za mifuko zinazowasaidia walima bustani wa mijini hususani jijini Nairobi kulima mboga mboga zinazotosha familia za watu sita katika meta moja tu ya eneo, kwa kwenda juu:

Kuwa Baraka Leo kwenye mtandao wa YouTube amepandisha mfululizo wa video zinazofundisha mbinu mbalimbali za kilimo cha mjini kwa kutumia uzoefu wa bustanini kwake nchini Kenya. Moja ya mbinu hizo ni ile ya awali ya
kutumia mifuko, , ikiwa na maboresho yanayorahisisha zaidi zoezi la umwagiliaji:

Mbinu mbili zaidi zinazofundishwa na chaneli hiyo ni ile ya kulima matuta marefu na kulima kwa ngazi , zote hizo zikiwa na faida ya kutumia vyema nafasi ndogo kwa ajili ya bustani, kwa kutengeneza matuta marefu ambaye hayamlazimishi mkulima kuinama ili kuvuna au kulima, na kumsaidia kulima kwenye maeneo yenye udongo wa kichanga na au penye udongo mgumu.

Mbinu nyingine kama hizo zinazowasaidia watu wanaolima mahali penye nafasi finyu zinaelezwa na watu wengine kwenye mtandao wa YouTube kutoka sehemu mbalimbali duniani. Kwa mfano, mbinu hii bora ya kutumia chupa za za maji plastiki zilizotupwa kwa ajili ya kutengeneza bustani ya kuelekea juu:

Mbinu hii hutumika kuotesha mimea kwa juu au chini ya chombo cha plastiki kilichotengenezwa kutokana na chupa kubwa za maji zilizotupwa:

Video hii nyingine video inatuonyesha njia nyingine ambapo matairi yalitupwa yanaweza kutumika kama vifaa vya kulimia bustani:

Picha ya kuotesha mbegu ni ya Chrisseee kwenye mtandao wa Flickr, inalindwa kwa hatimiliki ya Creative Commons Attribution License.

1 maoni

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.