Kundi la Harakati kwa ajili ya Amani, Haki na Utu [es] linaloongozwa na mtunzi wa mashairi wa zamaniJavier Sicilia lilisherehekea mwaka mmoja mnamo tarehe 28 Machi, 2012 tangu kuundwa kwake; kwa maneno mengine, mwaka tayari umekatika tangu kuuwawa kwa mtoto wake wa kiume Juan Francisco Sicilia ambaye mwili wake ulikutwa miongoni mwa wahanga wa vurugu za nchini Mexico katika jamii ya Las Brisas huko Temixco, Morelos.
Magazeti ya kitaifa kama vile Milenio [es] yalichapisha habari kuhusu shughuli zilizofanyika katika kumbukumbu hizo:
Con la asistencia de unas cien personas, cantidad mucho menor a la que lo acompañó hace un año, Javier Sicilia, Julián LeBarón y familiares de otras víctimas de la delincuencia iniciaron la jornada de 12 horas para conmemorar el aniversario de la muerte del hijo del poeta y de otros seis jóvenes, cuyos cuerpos fueron hallados en el fraccionamiento Las Brisas, en Temixco, Morelos.
En la fuente de la Paloma de la Paz, Sicilia señaló que la ausencia de más acompañantes en este aniversario se debe a que la sociedad ya aprendió a tolerar lo intolerable y que, de cara a los comicios electorales, quien en realidad pierde, consideró, es la sociedad.
A un año del multihomicidio, Sicilia declaró que no hay justicia en este caso porque hasta ahora no hay ninguna persona sentenciada.
Huku kukiwa na washiriki wapatao mia moja, ambayo ni idadi ndogo kuliko wale waliokuwa pamoja naye mwaka jana, Javier Sicilia, Julián LeBarón na wanafamilia wengine walianza saa 12 za ratiba ya kukumbuka kifo cha mwana wa mtunzi huyu wa mashairi na vijana wengine sita ambao miili yao ilipatikana huko Las Brisas, in Temixco, Morelos.
Katika eneo la mnara wa maji unaojulikana kama Peace Dove (Njiwa wa Amani), Sicilia alieleza kwamba kupungua kwa idadi ya washiriki kulidhihirisha kwamba watu wamejifunza kuvumilia yasiyovumilika na kwamba kwa kuwa ni mwaka wa uchaguzi, basi jamii yenyewe ndiyo iliyokuwa katika hali ya kupata hasara zaidi.
Mwaka mmoja baada ya mauaji hayo, Sicilia aliutangazia umma kwamba mpaka wakati huo haki ilikuwa bado haijapatikana kwa sababu hadi sasa hakuna aliyekuwa amepatikana na hatia au kuhukumiwa.
Karina González anakumbuka jinsi harakati za kundi hilo zilivyoanza:
Kundi hili la MPJD lilianza kufuatia barua iliyoandikwa na mtunzi wa mashairi Javier Sicilia, wakati alipompoteza mwanaye mwenye umri wa miaka 24, Jaunelo, kwa sababu vya vurugu ya vita. Kwa kupiga mbija ya “Estamos hasta la madre!” (“Tumechoka!”), maelfu ya raia wa Mexico waliishinda hofu yao na kumiminika mitaani kupinga vita hivyo. Mwaka mmoja uliopita, harakati hizo zilizoanza kule Morelos ziliwatia moyo maelfu ya raia wa Mexico kushutumu madhara ya vita na kutunza kumbukumbu hai za maisha ya wahanga.
Kama sehemu ya kumbukumbu hii, blogu inayoitwa Raia wa Mexico nchini Uswisi Wapenda Amani [es] ilieneza barua ifuatayo ili kutafuta uungwaji mkono:
Nosotros, Mexicanos viviendo en Suiza; Manifestamos con fuerza que la distancia que nos separa fisicamente de nuestro país, es nada cuando nuestros corazones se quedaron en México. Amamos, respetamos y sufrimos de igual manera que ustedes. El clima de violencia por el cual atraviesa nuestro país nos duele profundamente y nos indigna.
Por eso queremos decirles que desde Suiza estamos con ustedes en la lucha, Aún así, estando a miles de kilómetros. Porque como dice el escritor alemán Bertolot Brecht : « Quien lucha, puede perder. Quien no lucha, ya ha perdido.”
Con ustedes luchando por un México en paz.
Sisi, raia wa Mexico tunaoishi Uswisi tunataka kuonyesha kwamba umbali mkubwa unaotutenganisha sisi na nchi yetu hauna maana kwa kuwa mioyo yetu bado ipo nchini Mexico. Tunaipenda, tunaiheshimu na tunateseka kwa ajili yake sawasawa na ninyi mlio huko. Nyakati hizi za vurugu nchini mwetu zinatuumiza sana na kutukasirisha mno.
Ndiyo sababu tunataka kuwaambia kuwa kutokea huku Uswisi sisi tupo pamoja nanyi katika mapambano haya. Ingawa tunatenganishwa nanyi kwa maelfu ya kilometa. Hiyo ni kwa sababu, kama alivyoandika mwandishi wa Kijerumani Bertolot Brecht akisema: “Wale wanaopambana wanaweza kupoteza. Lakini wale ambao hata hawapambani, tayari wamekwishapoteza”.
Tupo nanyi katika kupigania Mexico yenye amani.
Kundi la Animal Político [es] lilikusanya baadhi ya matamshi ya Sicilia kuhusu kifo cha mwanae, hasa kuhusu mapenzi yake kwenye soka na kwa ajili ya timu fulani:
“Mi hijo Juan tenía una sola falla –se lamenta Javier Sicilia–: era americanista, en eso nunca lo pudimos corregir”. El poeta mira a su costado, donde su compadre, Francisco, corrobora sus palabras con un gesto afirmativo de la cabeza.
“Mwanangu Juan alikuwa na kosa moja tu – anasikitika Javier Sicilia-: alikuwa shabiki mkubwa wa Klabu ya Amerika, hatukuweza kurekebisha jambo hilo”. Kisha mtunzi huyo anatazama kando, upande alipo rafiki yake Francisco ambaye kwa ishara anaunga mkono maneno hayo.
Kupitia Twita, aliyewahi kugombea nafasi ya Urais Josefina Vázquez (@JosefinaVM) [es] hakutaka kupoteza fursa hiyo pale alipotuma ujumbe kwa Javier Sicilia:
Un abrazo solidario a Javier Sicilia, Gaby Cadena y los padres de los jóvenes asesinados hace un año. Su lucha no es en vano.
Ninampa Javier Sicilia kumbatio la mshikamano, vilevile Gaby Cadena na wazazi wengine waliopoteza watoto wao kwenye mauaji hayo. Mapambano yao hayatapita bure.
Kwa upande wake mwandishi wa habari Katia D'Artigues (@kdartigues) [es] naye alifanya tafakari kuhusu kifo cha mwana wa Sicilia:
Hace un año, hoy, Javier Sicilia estaba a unas horas de que le cambiara su vida.
Mwaka mmoja uliopita, siku kama ya leo, Javier Sicilia alikuwa saa kadhaa kabla ya kuanzisha kundi la harakati lenye lengo la kubadilisha maisha.
Mtumiaji twita mwanamama @lafalconielsa [es] alieleza hisia zake kuhusu mwanaharakati huyu:
Dirán lo que quieran, pero yo amo a Javier Sicilia
Vyovyote mtakakavyosema, ninampenda Javier Sicilia
Mtumiaji Twita mwingine @roblesmaloof [es] hakutaka kujiwekea mipaka kwa kuizungumzia familia ya Sicilia peke yake, alitunuku twiti yake kwa mhanga mmoja anayewakilishwa na Kundi la Harakati kwa ajili ya Amani, Haki na Utu:
Hoy como todos los días, pensamos en don #Nepomuceno Moreno, quien como muchas madres y padres, fue asesinado por buscar a su hijo #MPJD
Leo, kama ilivyo kila siku, tunamkumbuka Bw. #Nepomuceno Moreno, ambaye kama ilivyo kwa akina mama na baba wengi, aliuwawa kwa jitihada zake za kumtafuta mtoto wake #MPJD
Unaweza kusoma maoni zaidi na taarifa kuhusu kumbukumbu hizi kwa kufuata ishara-unganishi hizi #MPJD, #hastalamadre (fed up), #AniversarioMPJD. Zaidi ya hayo, anwani rasmi ya Twita ya Kundi hili la Harakati (@MxLaPazMx) [es] liliwafahamisha wafuasi wake kuhusu shughuli ambazo zilifanyika katika siku hiyo ya kumbukumbu.
Kama Global Voices ilivyoripoti tangu Agosti 2011, Harakati na vuguvugu ambalo Sicilia anaongoza yamesababisha maoni na miitiko tofauti kwenye mtandao wa Intaneti kuashiria kwamba licha ya kuwepo tofauti za maoni, kuna matumaini ya pamoja kwamba huenda hali ya vurugu inayotawala kwenye nchi hii iliyo Amerika ya Kaskazini inaweza kubadilika kwa manufaa ya raia wote wa Mexico.