Nchi za Balkani: Ufanano Baina ya Facebook na Chama cha Kikomunisti cha Yugoslavia

Kwa desturi yake ya ucheshi, Sead Dzigal ametoa orodha [MKD] ya Ufanano baina ya Facebook na Chama cha Kikomunisti cha Yugoslavia (CPY):

 • Facebook – ni mtandao wa wanajamii
  CPY – ni mtandao wa wajamaa
 • Kama sio mwanachama wa Facebook – Huna maana kwao
  Kama si mwanachama wa CPY – Huna maana kwao
 • Kila mtu kwenye Facebook ni rafiki yako, japo kuwa huwajui nusu yao.
  Kila mwana CPY ni swahiba wako,* japo huwajui zaidi ya nusu yao.
 • Katika Facebook unashabikia matukio mbalimbali bila hata kuinua kidole chako.
  Katika CPY we ni mjumbe wa kamati na makusanyiko lukuki bila hata ya kunyanyua kidole chako.
 • Kwenye Facebook kuna mchezo wa mashamba,
  katika CPY kuna zadrugas [namna fulani ya kolkhoz] na sera mpya ya ardhi.
 • kwenye Facebook utajipatia “Like,” (naipenda)
  kwenye CPY unajipatia “Long live comrade…!!!” (maisha marefu swahiba)
 • Facebook – mara nyingi huingilia faragha yako,
  CPY – mara nyingi huingilia faragha yako.
 • .aNTI alichangia kwa kutoa maoni [MKD], akitumia usema uliotumiwa mara nyingi na raisi wa kwanza wa jamhuri ya Czech Vaclav Havel:

  Makala hii imejaa maoni yaliyozoeleka na ni propaganda za wapinga ukomunisti. Kitu pekee kibaya katika hili ni kwamba wakomunisti wenyewe ni wapinga ukomunisti.

  Recenzent anakubali na anajaribu kuonesha jinsi wapinga ukomunisti wa sasa walivyo na mtazamo usio sahihi kwajinsi mabadiliko yanayojitokeza, anakumbusha [MKD]:

 • Vyombo vya habari vilikuwa vikimilikiwa na vyama vya siasa. Siku hizi vinaweza kuwa kwa niaba ya Serikali au vipinga Serikali, lakini bado vinamailikiwa na vyama vya siasa.
 • Utapata kazi kirahisi zaidi ilimradi tu ni mwanachama wa chama cha siasa , haialishi chama hicho ni CPY, SDSM or VMRO-DPMNE.
 • Pia amejuza kuwa huu msimamo usio wazi wa vyama vya siasa katika mambo mbalambali umebaki kuwa ni msingi wa vyama hivyo sasa. Vyama pia hupigana na waandishi kwa nadharia za kihasidi.

  * maneno swahiba na rafiki yamekuwa na maana sawa katika lugha za kislavik, kama Kimasedonia, Kiserbia, Kikroashia, Kiboznia…..

  Anza mazungumzo

  Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

  Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.