Moroko: Je, Wakristu Wako Hatarini?

Mapema mwezi Machi mwaka huu, watazamaji walishuhudia jumla ya wafanyakazi wa muda mrefu katika kituo cha Kikristo cha kulelea watoto yatima wapatao 20 wakifukuzwa kutoka katika nchi ambayo wanaiona kama nyumbani. Tukio hilo pamoja na mengine kadhaa yaliyofuatia yamezusha mjadala kuhusiana na imani ya Kikristu katika ufalme huo.

Takwimu rasmi za kiserikali nchini Moroko zinaeleza kwamba asilimia kati ya 98.7 – 99 za jumla ya watu nchini humo ni Waislamu (waliobaki ni kama asilimia 1 ambayo ni Wakristo na asilimia 0.2 ambao ni Wayahudi), takwimu hizo zinajumuisha pia Wazungu wanaoishi Moroko. Kuinjilisha ni kosa kama ilivyo kwa mtu kuacha Uislamu na kuingia katika dini nyingine. Hata hivyo, wageni wanaruhusiwa kuishi imani yao kwa uhuru, na kuna makanisa kadhaa bado, yaliyo mengi ni yale yaliyojengwa enzi za ukoloni wa Wafaransa. Kwa kulinganisha na kundi hilo lililopita, Wayahudi wa nchi hiyo ni wale walio wenyeji kabisa wa hapo, hawa nao wanaruhusiwa kuishi imani yao kwa uhuru.

Pamoja na kutoa uhuru huo, inaonekana kwamba siku za karibuni serikali inachukua hatua kali dhidi ya uinjilishaji, uwe ule wa waziwazi au unaodhaniwa kufanyika. The Moroccan Dispatches inatukumbusha tukio moja la hivi karibuni la kule Misri ambapo Padre mmoja Mkatoliki alifukuzwa kutoka katika nchi hiyo:

Wainjilisti wamekuwa wakifanya kazi kwa miaka mingi nchini Moroko na lengo lao kubwa limekuwa ni kuwaongoa Waislamu. Wakatoliki wamekuwepo kwa muda mrefu zaidi, lakini kwa makusudi kabisa hawakutaka kujihusisha na uinjilishaji wa moja kwa moja. Kwa hiyo lilikuwa tukio la kushangaza kwamba Padre Mkatoliki alikamatwa na kisha kufukuziwa mbali na tukio la hivi karibuni la ushughulikiaji wanaoinjilisha.

Mwanablogu anatutumia ujumbe aliopokea kutoka kwa padri wa Kikatoliki anayefanya kazi Moroko:

Mnamo Jumapili tarehe 7 mwezi Machi, dakika tano kabla ya kuanza misa; askari polisi wa jiji la Larache waliingia kwenye nyumba yetu ya watawa na kumkamata mmoja wa watawa, Rami Zaki, ambaye ni raia wa Misri na ambaye bado yuko katika hatua zake za awali za malezi na aliyekuwa anaishi na sisi kwa mwaka mmoja. Aliamriwa kuondoka na polisi wale, wala hakupewa fursa ya kuchukua chochote, wala hakuelezwa kwa nini alikuwa akikamatwa …

…Pale Rami alipopakiwa kwenye ndege, alinyang'anywa pasi yake ya kusafiria ambayo ilikabidhiwa kwa rubani ambaye naye aliikabidhi pamoja na Rami kwa polisi kule jiji la Kairo. Alishikiliwa na polisi wa Kairo kwa muda wa saa saba kabla hajaruhusiwa kupiga simu kwenye nyumba ya watawa wenzake. Tangu Jumapili asubuhi alipokamatwa mpaka mchana wa Jumanne alipoachiwa – jumla ya saa 50 – Rami alinyimwa haki zake za kimsingi kama binadamu na askari polisi wa Moroko na wale wa Misri.

Katika makala nyingine, mwanablogu anaeleza kwamba umma nao umejiunga katika msako huo, akitoa mfano wa tukio la hivi karibuni ambapo msalaba uling'olewa kutoka katika eneo ambapo umekuwa kwa miaka mingi sana:

Hapa ndipo ambapo msalaba ulikuwepo huko Meknés

Hapa ndipo ambapo msalaba ulikuwepo huko Meknés


Hapa ndipo ambapo msalamu ulikuwepo huko Meknes’ medina. Wakatoliki wanaofundisha raia wa Moroko lugha na stadi nyingine za kazi katika jengo hili hawashughuliki na uinjilishaji lakini nao wamenaswa na chuki hizi dhidi ya Ukristo kufuatia kufukuzwa kwa Wakristo kadhaa hivi karibuni. Wiki iliyopita, msalaba uling'olewa na kuvunjwavunjwa vipande vidogovidogo. Katika hatua inayoonekana kuwa ya pekee, raia wa Moroko ambao wamekuwa wakinufaika na kazi za watawa hawa, wamejitolea kuujenga upya msalaba huo.

Kwenye makala yake ya hivi karibuni, mwanablogu huyo anatathmini makala ya TelQuel kuhusiana na matukio hayo, na anaeleza hivi:

Katika makala kuu, inaonyesha kwamba raia wengi wa Moroko huongokea Ukristo zaidi kwa sababu ya vyombo vya habari vya Kiarabu kuliko shughuli za wamisionari wageni. Jambo hili linaendana na yale ambayo nimewahi kuyashuhudia: raia wengi wa Moroko wamewahi kufanya mazungumzo kuhusu duni na wamisionari Wakristo lakini hakuna walioongoka. Wapo walioutetea Uislamu huku wakivuta bangi ili mradi tu wawaponde Wakristo, uzoefu huu unaokupa picha kuhusu namna gani raia wa Moroko wanavyoelewa Uislamu wao. Mtazamo huu kuhusu wamisionari wageni, bila shaka, unaondolewa mbali msingi wa hoja za matukio ya hivi karibuni ya kuwafukuza wageni wengi.

Ili kuhitimsha, mwanablogu anaeleza kuhusu namna vyombo vya habari vilivyoathiriwa na usakaji huo na anaomboleza:

Baadhi ya vyombo vya habari vinavyoikosoa serikali vimefungiwa. Jambo kama hilo linaweza kutokea kwa Tel Quel pia. Lakini, kadiri vitakavyoendelea kuwepo ndiyo kadiri hiyohiyo ambapo kutakuwa na mijadala ya kutafakarisha kuhusu matukio ya hivi karibuni.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.