Angola: Gharama za Juu za Maisha Mjini Luanda

Mji mkuu wa Angola, Luanda, ni mji aghali sana. Kwa wote, Waangola na wageni. Kama upo hapa, basi unafahamu fika. Mahitaji ya msingi, kama chakula, elimu na nyumba yana bei sawa na baadhi ya nchi za Ulaya. Tofauti kubwa ni kuwa mishahara nchini Angola inachekesha ikilinganishwa nay a wenzao wa Ulaya, jambo ambalo linapelekea mapambnano ya kila siku ili kupata mahitaji ya msingi.

Ni wazi mapambano haya hayafanywi na wale wenye pesa ambao, kwa sababu zisizoeleweka au la, wanalindwa na akaunti za benki ambazo zinaweza kuwafanya viumbe wa kawaida kupata wivu. Kwa mujibu wa tafiti iliyofanywa mwezi wa Pili na kampuni ya Kiingereza, ECA International – Mji wa Luanda ni wa kwanza kati ya miji ghali kupita yote duniani.

Katika blogu yake, Mundo da Verdade [pt], Miguel Caxias anaandika:

“Só para terem uma ideia, o custo por noite no hotel em que estou é de 170 USD (quarto individual, com casa de banho e pequeno-almoço mesmo muito sofrível). Estamos a falar de um hotel que deve ter se tanto, duas estrelas. Para um europeu, não só por costumes alimentícios mas também por costumes de segurança, não se arrisca a comer em qualquer botequim de esquina, obviamente. No restaurante onde temos feito as nossas refeições, o custo médio de uma dose é de 30USD (junte-se a isso bebida, sobremesa, entradas e o preço salta logo para 40/45 USD de despesa individual).

Luanda está numa fase de construção massiva. Junto à Marginal existem apartamentos a 1 milhão de USD. Estão todos vendidos!!!”

“Ili kukupa picha tu, gharama za usiku mmoja katika hoteli ninayokaa ni $170 dola za Kimarekani (chumba cha kitandanda kimoja na bafu, pamoja na staftahi ndogo isiyokidhi). Tunaongelea hoteli yenye hadhi ya nyota mbili. Kwa mtu wa Ulaya, siyo tu kwa sababu ya desturi za maakuli/chakula, bali piakwa sababu za kiusalama, hatuthubutu kujitia hatarini na kula chakula cha kwenye kona, ni wazi. Tunakwenda kwenye mgahawa, gharama za wastani za chakula ni $30 dola za Kimarekani (ongeza na kinywaji, vitafunwa vitamu na vyakula vya mwanzo na bei inapanda haraka kufikia $40/45 kwa mtu mmoja).

Ujenzi mkubwa unafanywa katika mji wa Luanda. Karibu na ukingo [eneo la mbele ya ghuba], kuna nyumba za dola milioni moja zimeorodheshwa. Na zote zimeshauzwa!!!”

Gharama kubwa za maisha nchini hazina mantiki, kwani haziwiani na kiwango bora cha maisha, walau sio kwa wale walio vibaya kiuchumi. Angola inaorodhesha vilekezo vya juu vya maendeleo ambavyo, kwa bahati mbaya, havishabihiani na hali ya kifedha ya raia walio wengi nchini Angola. Mahitaji yanapita kiasi yanayoambatana na uhaba wa ugavi unafanya mambo yawe kiasi magumu.

Mwandishi wa Kibrazil wa blogu ya Diário de África [pt] anatoa uchambuzi wa haraka juu ya nini kinachotokea Angola.

“Não são apenas os alugueres (habitação) que custam caro. Tudo é caríssimo. Um quilo de tomate pode sair por 20 USD. Uma bandeja de uvas pode custar 30 USD o quilo. Um bife com batatas fritas pode custar facilmente, 50 dólares. Um cano furado pode sair por 1000.000 USD. Tapar um pequeno furo na tubulação do ar-condicionado do carro e colocar o gás para enfrentarmos o calor luandense custa 200 USD.

Precisa de electricista? Ele não vai sair da sua casa sem ter tirado pelo menos 100 USD de você. Mesmo que só tenha trocado uma lâmpada. Porque é tudo tão caro?”

“Siyo kodi ya nyumba pekee ambayo ghali. Kila kitu ni ghali sana. Kilo ya nyanya inawezaa kuuzwa kwa $20 dola za Kimarekani. Sinia ya zabibu inaweza kugharimu $30 dola za Kimarekani kwa kilo. Kipande cha nyama na chipsi kwa urahisi vinaweza kugharimu $50 za Kimarekani. Bomba liliotoboka linaweza kukurudisha nyuma kwa kiasi cha $1000.00. kuziba tobo dogo kwenye bomba la kiyoyozi cha kwenye gari na kujaza gesi ili kukabili joto la Luanda kunaweza kugharimu $200.

Unahitaji fundi umeme? Hawezi kuondoka nyumbani kwake bila ya kupata angalau $100.00 toka kwako. Hata kama ni kubadilisha taa ya umeme tu. Kwa nini kila kitu ni ghali sana?”

Kwa mujibu wa mwanablogu huyu, jibu ni rahisi, na, kwa mara nyingine tena, linasikika kutokea kwenye vita ambavyo viliipokonya nchi miaka zaidi ya 30 ya maendeleo.

“O atabalhoado processo de independência e a guerra acabaram com tudo. Primeiro, a independência. Em 1975, pelo menos 300 mil portugueses abandonaram Angola. Médicos, dentistas, advogados, empresários, encanadores, mecânicos, burocratas, professores. Em questão de meses, Angola ficou sem quadros. Não havia quem soubesse gerenciar as finanças do país. Depois a guerra. O esforço de guerra sugou o dinheiro que deveria ser investido na saúde, na educação, nas infra-estruturas do país. Agora multiplique essa situação por 30 anos. O resultado chama-se Luanda.

Com a alta no preço do petróleo nos últimos anos, os fretes subiram e por tabela, o de todos os produtos. Chegou-se a uma situação tal que mesmo os itens produzidos em Angola podem custar mais que os importados. Porquê? Os economistas que me corrijam, mas parece ter algo a ver com a tal lei da oferta e da procura. Quem quer agora, tem de pagar mais.”

O país não tem indústrias. Tudo é importado. Vem de navio. No porto, não há espaço. Os navios ficam dois, três meses atracados em alto-mar, aguardando autorização para descarregar. Só agora é que a agricultura começa a dar os primeiros passos. Mas só nas áreas em que não há minas terrestres. O último número que ouvi era de que mais da metade das terras cultiváveis do país estava cheia de minas. Enquanto o terreno não estiver limpo, nada feito. Portanto, até a comida precisar ser importada.

“Mapambano magumu ya uhuru yaliyofuatiwa na vita yalipoteza kila kitu. Kwanza, uhuru, mwaka 1975, kwa uchache raia wa Ureno wapatao 300, 000 waliiacha Angola. Madaktari, Waganga wa meno, wanasheria, wafanyabiashara, mafundi bomba, mafundi wa mashine, watumishi wa serikali, maprofesa. Katika muda wa miezi, Angola iliachwa bila wafanyakazi waliofuzu.Hapakuwa na mtu aliyefahamu jinsi ya kudhibiti fedha za nchi. Pili, vita. Jitihada za vita zilinyonya pesa zote ambazo zilipaswa kuwekezwa kwenye afya, elimu na miundombinu ya nchi. Sasa zidisha hali hiyo kwa miaka 30, na utapata Luanda.

pamoja na bei ya juu ya mafuta katika miaka ya hivi karibuni, gharama za usafiri nazo zimepanda na, kwa mpigo, bei ya bidhaa nyingine pia. Hali imeondokea kuwa hata bidhaa zinazozalishwa Angola zinaweza kugharimu zaidi ya zile zinazoagizwa kutoka nje. Kwa nini? Wanauchumi tafadhali nisahihisheni, lakini hali hii inaelekea kuwa na jambo Fulani lenye kuhusiana na kanuni za ugavi na mahitaji. Kama unataka sasa hivi, inabidi ulipie zaidi.

Nchi haina viwanda. Kila kitu kinaagizwa. Kinasafirishwa kwa meli, na hakuna nafasi bandarini. Meli zinaegeshwa kwa miezi miwili mpaka mitatu kwenye bahari kuu, zikisubiri ruhusa ya kupakua bidhaa. Ni hivi sasa kilimo kimeanza kupiga hatua hatua zake za kwanza, lakini ni katika sehemu zile ambazo hazina mabomu ya ardhini. Takwimu mpya nilizozisikia ni kuwa nusu ya ardhi yenye rutuba imejaa mabomu. Na kama ardhi haijasafishwa, hakuna linaloweza kufanyika. Kwa hiyo hata chakula kinabidi kiagizwe.

Kipande cha nyama ya mbuzi kinagharimu 600 KZ ($7 za Marekani) picha ya Tweetpic na @bethinagava

Kipande cha nyama ya mbuzi kinagharimu 600 KZ ($7 za Marekani) picha ya Tweetpic na @bethinagava

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.