Mauritania: Uchaguzi wenye udanganyifu?

Tarehe 18-07-2009, miezi 11 baada ya mapinduzi ya kijeshi yaliyoongozwa na Jenerali Mohamed Ould Abdel Aziz, Mauritania imemchagua Jenerali huyu kwa Urais, na kusababisha wapinzani wakuu wa Abdel Aziz kuukataa uchaguzi kwamba ni “kiini macho,” kwa mujibu wa Habari za BBC. Pitio la haraka haraka kwenye blogu za nchi za Saheli linaonyesha kwamba wapinzani wako katika ushirika mzuri.

Blogu ya Maghreb inawaelezea wagombea:

Wamauritania wanaelekea kwenye vituo vya kupigia kura leo katika uchaguzi wa Rais wa kihistoria. Mgombea anayepewa nafasi kubwa ya kushinda ni Ould Abdel Aziz, kiongozi wa zamani wa mapinduzi ya kijeshi ambaye anagombea kwa njia ya jukwaa la umaarufu na kwa kuwa mpinga-Israeli. Ould Abdel Aziz pia ameatoa wito wa kukomesha vitendo vya rushwa na kusimika misingi ya utawala bora. Kwa mujibu wa kura za maoni hivi karibuni, Jenerali Ould Abdel Aziz anafuatiwa na Ahmed Ould Dada na Messaoud Ould Boulkheir. Agenda za huyu wa kwanza, Ahmed Dada zinatilia mkazo maadili na misingi ya “haki, usawa, uvumilivu.” Ould Boulkheir anakumbatia nadharia za demokrasia na haki za binadamu, na ameahidi kuunga mkono vyama vya wafanyakazi.

Mwanablogu Moor Next Door, mwenye makao huko Marekani, kwa ujasiri kabisa ameuita ni udanganyifu, kwa kusema:

Kampeni za Ould Daddah na Boulkheir zinaweza kuelezewa kama “zenye taharuki”: idadi ya kura zinazotangazwa tangu upigaji kura ufanyike zinaonyesha watu wengi sana wakimuunga mkono Jenerali Ould Abdel Aziz. Huko Nouadhibou, asilimia sitini na tano wanaonyesha matokeo hayo hayo yenye kumuunga mkono Ould Abdel Aziz. Swali: kwa jinsi gani? Jawabu: Udanganyifu. Mwitikio wao sasa utaonyesha nini kinawezekana kesho na siku zinazofuata.

Mwanablogu huyo anatukumbusha:

Jenerali Ould Abdel Aziz ameitawala Mauritania katika kampeni tatu muhimu: Mapinduzi mazuri (2005), Mapinduzi yaliyokataliwa (2008) na, sasa, mapinduzi ya Kikatiba (2009).

Mwanablogu anayeishi marekani ambaye anayejielezea mwenyewe kuwa mwanablogu wa Kiafrika Bombastic Element analiita beleshi kwa jina lake (au kusema maneno bila kupinda pinda):

BBC inaarifu kuwa kiongozi wa mapinduzi Jenerali Mohamed Ould Abdelaziz, aliachia madaraka na kujigeuza raia kwa minajili ya kugombea uchaguzi wa Jumamosi anakaribia kucheza mchezo wa “Musharraf.”

Wakati wanablogu wanasuburi matokeo yakamilishwe, mmoja –msanii anayeishi Nouakchott, anatoa mchoro huu wa siku ya uchaguzi huko Nouadhibou:

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.