Malawi: Homa Ya Uchaguzi na Kuelea Teknolojia ya Kidijitali

Juma lililopita lilikuwa lenye moto wa kisiasa kwa Wamalawi wengi kwani wameshuhudia wagombea wa viti vya urais na ubunge wakiwasilisha maombi yao kwenye Tume ya Uchaguzi kuelekea Uchaguzi utakaofanyika terehe 19 Mei. Hadi kufikia mwisho wa zoezi hilo wagombea wapatao 10 waliwasilisha maombi yao ya kugombea urais na mamia wengine kwa ajili ya kugombea viti 193 vya bunge.

Mapema, mwanahabari, Kondwani Munthali alieleza maoni yake kuhusu maendeleo ya kisiasa ambayo yanategemewa kwenye ushindani wa ngazi ya urais na kadhalika kwenye ngazi za ubunge. Anaandika kwenye Viva My Country's Democracy:

Ndiyo, nilisema kuwa chama cha DPP hakina muundo wa kujiendesha kwenye hatua za mwanzo za uchaguzi. Nafarijika kuwa mawaziri wawili wamekumbuka majadiliano niliyofanya nao na wamenipigia simu. Kwa chama cha UDF, jinsi watakavyodhibiti hali inayomuhusu Muluzi hilo ni juu yao. Kwa MCP inaonekana wamebadilika kwa hakika, wanaonekana wako makini sana kuweza kupindua meza. Kwa leo hapa ndio inapoishia

Mwanablohu mwingine anayeblogu kwenye Ndagha anakubaliana na Munthali kwamba siasa za Malawi mwaka huu zimeshika moto. Anategemea kwamba washiriki wana moyo wa dhati kwa ajili uya Wamalawi na si kwa ajili ya kuhudumia maslahi yao. Anasema kwamba mwaka huu unatia moyo. Kwa nini?:

Kwangu, mbio za uchaguzi wa wabunge zitakuwa za kusisimua kwani zitaonyesha wagombeea wapya wengi ambao kwa mtazamo wangu wanaweza kutoa mchango muhimu kwa maendeleo ya nchi. Natamani tungekuwa na sura mpya maarufu kwenye uchaguzi wa rais.

Mwanahabari mwingine, Mzati Nkolokosa anakiita kipindi hiki cha siasa nchini Malawi kama kipindi cha uzushi. Anaandika makala ndefu inayomuhusu Brown Mpinganjira ambaye amekitosa chama ambacho alisaidia kukijenga na amejiunga na John Tembo wa Chama cha Malawi Congress kama mgombea mwenza.

Ni sahihi kukiita kipindi hiki kama kipindi cha uzushi. Lakini Brown Mpinganjira ni lazima akubali kwamba ukweli wa kisiasa katika Malawi huanza kama uzushi.

Brown Mpinganjira, mwanasiasa mwerevu zaidi nchini Malawi kwa mujibu wa Jack Mapanje, ni mzuri katika mawasiliano. Anayafahamu maneno yaliyojaa maana, anaongea kishairi, anaweza kuwachanganya wananchi, hata wanahabari, ambao hawamfuatilii kwa makini.

Idara nyingi za umma nchini Malawi zinatumuia tarakilishi. Wakati kuna juhudi za kuboresha (muundo), bado ni changamoto kubwa kwa idara na asasi nyingi. Moja ya ofisi ambazo zinahudumia Wamalawi wengi ni Ofisi ya Serikali ambako pamoja na mambo mengine wateja husaidiwa kwa huduma zinazohusu masuala ya mirathi.

Baada ya kufanya kozi fupi ya uingizaji takwimu, Mwanahabari, Pauline Kalumikiza anaandika juu ya umuhimu wa ofisi kama hizi kutumia teknolojia ya dijitali.

Sababu ni kuwa, inawachukua muda mrefu mrefu kuwahudumia warithi kutokana na uhifadhi kwa kutumia mikono. Nafikiri ni mtindio unaochukua muda mrefu, kwa sababu wanashughulikia mafaili mengi ili kulitoa moja, inachukua muda.
Mara nyingi, watakuambia, ‘Samahani, njoo mwezi ujao, tupe muda wa kulitafuta faili lako’ hebu fikiria mtu anakuja kutoka Nsanje kuja kwa Mwanasheria Mkuu mjini Blantyre; anakuja tena kama alivyoahidiwa na anaambiwa asubiri tena kwa wiki moja nyingine, inaghafirisha, au sivyo?

Naam, teknolojia ina faida zake lakini nafikiri, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu ingeweza kuokoa muda na nishati kwa kutumia teknolojia ya dijitali.
Hatuwezi kuendelea kuongelea teknolojia ya mawasiliano ya kidijitali kuweza kumfikia kila mmoja, kama ofisi zinazohifadhi habari muhimu bado zinatumia mbinu za uhifadhi za mikono. Zisinthe! (Yaache Mambo yabadilike!)

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.