Papa Francis Ataitembelea Makedonia Kaskazini Mwezi Mei, Muda Mfupi Baada ya Uchaguzi wa Rais

Picha za skirini kutoka katika tovuti ya papa.mk, imewekwa na Serikali ya Jamuhuri ya Makedonia Kaskazini wakati Papa alipowatembelea Mei 7, 2019.
Papa Francis ataitembelea Makedonia Kaskazini Mei 2019, kwa siku mbili baada ya raundi ya pili ya uchaguzi wa Rais.
Itakuwa ni mara ya kwanza kwa Papa kutembelea Makedonia Kaskazini. Kutembelewa huko itakuwa ni sehemu ya ziara ya siku tatu katika ukanda huo ambapo pia atatua Bulgaria.
Serikali ya Makedonia Kaskazini imetengeneza tovuti, ya papa.mk kuwezesha ziara hiyo. Kutokana na uwepo wa tamaduni mbalimbali katika nchi, maudhui katika tovuti hizo yanapatikana kwa lugha tatu tofauti ambazo ni Kimakedonia, Kialbania na Kiingereza.
Baadhi ya wananchi wameuliza kuhusu serikali kumiliki tovuti hiyo, wakisema kuwa inaleta utata kwa sababu serikali hiyo haina dini.
Wananchi wa Makedonia wanaweza kuomba tiketi za kuhudhuria Ibada Takatifu itakayoendeshwa na Papa ambapo tiketi hizo zinapatikana bure katika makanisa nchini wakati wageni toka nje ya nchi wanaweza kupata nafasi kwa kupitia tovuti. Ibada hiyo itafanyika katika viwanja vya Mji Mkuu wa Skopje, Mei 7.
Wakatoliki wanwanaf angalau asilimia moja ya watu wote wa Makedonia Kaskazini ambapo asilimia 65 ni Wakristo wa ki-Orthodox na angalau asilimia 33 ni Waislamu. Pamoja na idadi yao ndogo, jamii ya Kikatoliki ina watu mbalimbali kama vile Wamakedonia, Waalbania, Wakroeshia, Waslovenia na Wapoland.
Kwa upande mwingine, nchi hii ina maana kubwa katika ukatoliki kwa sababu mji wake mkuu Skopje ndipo alipozaliwa Mama Theresa (1910-1997), ambaye alitunukiwa kuwa Mtakatifu Teresa wa Calcutta. Mmoja kati ya wamisionari wa karne ya 20 na mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel, alizaliwa katika familia yenye asili ya ki-Albania ambapo nyumba yao ilikuwa pale ambapo kwa sasa ni uwanja mkuu wa mji.
Kipengele cha kisiasa katika ziara hiyo kinafunika umuhimu wake kidini. Kama mkuu wa nchi, Papa amepangiwa kuonana na waziri mkuu na rais anayemaliza muda wake , ambaye madaraka yake yatakoma siku tano baadaye.
Wamakedonia wanaona ziara hii kama ishara ya kutambuliwa na nchi za Magharibi na kuinua jitihada za serikali kuiweka nchi karibu na uanachama wa NATO na Umoja wa Ulaya. Hisia hizi zinapatikana huko twita katika chapisho la jenerali mstaafu wa polisi Stojanche Angelov, ambapo alitoa maoni katika ziara ya maandalizi ya Mkuu wa Taasisi ya Usalama wa Raia ya Makedonia kwa Vatican.
Благодарение на мудрата, храбра и одлучна меѓународна политика на оваа Влада, нашата мала држава со големи чекори оди напред!
Директорот на БЈБ Сашо Тасевски подготвува највисоко ниво на безбедност за престојот на Папата Франциск во Скопје.
Стево за Претседател! pic.twitter.com/zF2m2lvzL3— Stojanche Angelov (@StojanceAngelov) April 17, 2019
Asante kwa siasa za hekima na za kijasiri zilizoamuliwa na serikali hii, nchi yetu ndogo inasonga mbele kwa kasi kubwa. Mkurugenzi wa Taasisi ya Usalama wa Raia, Sasho Tasevski aliandaa usalama wa hali ya juu kwa ajili ya Papa Fransis atakapokuwa hapa Skopje.
Stevo [Pendarovski] kwa urais!
Mwezi mmoja kabla ya safari ya Papa, habari za Vatican mfumo wa habari wa Holy See, waliongeza lugha ya Kimakedonia katika kazi zake. Ni lugha ya 34 inayopatikana katika chombo hicho. Askofu wa Skopje, Askofu Kiro Stojanov alisema “hili ni tunda la awali la ziara ya kitume ya Papa Francis.”
Kabla ya safari ya Kitume ya#PapaFrancis’ kuelekea #MakedoniaKaskazini hapo Mei 7, @VaticanNews waongeza ukurasa unaoandikwa kwa Lugha ya Kimakedonia. https://t.co/2obxroAMcx
— Vatican News (@VaticanNews) April 8, 2019
Septemba, Papa atatembelea Msumbiji, Madagascar na Mauritius. Global Voices imeandika mrejesho kutoka Msumbiji kuhusu ziara hiyo.
Mada za Habari

Anza mazungumzo
Kumbukumbu za Mwezi
- Disemba 2020 1 ujumbe
- Oktoba 2020 4 jumbe
- Septemba 2020 8 jumbe
- Agosti 2020 2 jumbe
- Julai 2020 1 ujumbe
- Juni 2020 1 ujumbe
- Aprili 2020 1 ujumbe
- Februari 2020 2 jumbe
- Oktoba 2019 2 jumbe
- Agosti 2019 2 jumbe
- Juni 2019 3 jumbe
- Mei 2019 10 jumbe
- Aprili 2019 14 jumbe
- Machi 2019 10 jumbe
- Februari 2019 11 jumbe
- Januari 2019 2 jumbe
- Disemba 2018 2 jumbe
- Novemba 2018 1 ujumbe
- Oktoba 2018 1 ujumbe
- Agosti 2018 3 jumbe
- Julai 2018 11 jumbe
- Juni 2018 12 jumbe
- Mei 2018 12 jumbe
- Aprili 2018 6 jumbe
- Januari 2018 2 jumbe
- Disemba 2017 3 jumbe
- Septemba 2017 1 ujumbe
- Agosti 2017 8 jumbe
- Julai 2017 8 jumbe
- Juni 2017 5 jumbe
- Mei 2017 5 jumbe
- Aprili 2017 9 jumbe
- Machi 2017 15 jumbe
- Februari 2017 8 jumbe
- Januari 2017 6 jumbe
- Disemba 2016 2 jumbe
- Novemba 2016 12 jumbe
- Oktoba 2016 16 jumbe
- Septemba 2016 7 jumbe
- Agosti 2016 5 jumbe
- Julai 2016 15 jumbe
- Juni 2016 15 jumbe
- Mei 2016 8 jumbe
- Aprili 2016 8 jumbe
- Machi 2016 10 jumbe
- Februari 2016 8 jumbe
- Januari 2016 1 ujumbe
- Disemba 2015 1 ujumbe
- Novemba 2015 10 jumbe
- Oktoba 2015 7 jumbe
- Septemba 2015 4 jumbe
- Agosti 2015 4 jumbe
- Julai 2015 2 jumbe
- Juni 2015 15 jumbe
- Mei 2015 12 jumbe
- Aprili 2015 30 jumbe
- Machi 2015 3 jumbe
- Februari 2015 25 jumbe
- Januari 2015 5 jumbe
- Novemba 2014 9 jumbe
- Oktoba 2014 21 jumbe
- Septemba 2014 32 jumbe
- Agosti 2014 2 jumbe
- Julai 2014 51 jumbe
- Juni 2014 24 jumbe
- Mei 2014 57 jumbe
- Aprili 2014 60 jumbe
- Machi 2014 67 jumbe
- Februari 2014 43 jumbe
- Januari 2014 12 jumbe
- Disemba 2013 29 jumbe
- Novemba 2013 50 jumbe
- Oktoba 2013 32 jumbe
- Septemba 2013 25 jumbe
- Agosti 2013 9 jumbe
- Julai 2013 34 jumbe
- Juni 2013 33 jumbe
- Mei 2013 28 jumbe
- Aprili 2013 18 jumbe
- Machi 2013 3 jumbe
- Februari 2013 12 jumbe
- Januari 2013 20 jumbe
- Disemba 2012 16 jumbe
- Novemba 2012 8 jumbe
- Oktoba 2012 21 jumbe
- Septemba 2012 13 jumbe
- Agosti 2012 16 jumbe
- Julai 2012 26 jumbe
- Juni 2012 21 jumbe
- Mei 2012 3 jumbe
- Aprili 2012 19 jumbe
- Machi 2012 10 jumbe
- Februari 2012 2 jumbe
- Januari 2012 10 jumbe
- Disemba 2011 16 jumbe
- Mei 2011 10 jumbe
- Aprili 2011 22 jumbe
- Februari 2011 4 jumbe
- Januari 2011 10 jumbe
- Disemba 2010 4 jumbe
- Novemba 2010 7 jumbe
- Oktoba 2010 6 jumbe
- Septemba 2010 10 jumbe
- Agosti 2010 13 jumbe
- Julai 2010 20 jumbe
- Mei 2010 2 jumbe
- Aprili 2010 16 jumbe
- Machi 2010 22 jumbe
- Februari 2010 22 jumbe
- Januari 2010 41 jumbe
- Disemba 2009 47 jumbe
- Novemba 2009 56 jumbe
- Oktoba 2009 29 jumbe
- Septemba 2009 3 jumbe
- Agosti 2009 6 jumbe
- Julai 2009 10 jumbe
- Juni 2009 11 jumbe
- Mei 2009 5 jumbe
- Aprili 2009 7 jumbe
- Machi 2009 3 jumbe
- Februari 2009 18 jumbe
- Januari 2009 12 jumbe
- Novemba 2008 3 jumbe
- Oktoba 2008 9 jumbe
- Septemba 2008 12 jumbe
- Agosti 2008 9 jumbe