Wanaharakati wa Mazingira wa Bulgaria Wapata Ushindi Muhimu wa Mahakama Kufuatia Kampeni yao ya #SaidiaHifadhiyataifayaPirin

Map, Pirin National Park, Pirin, Bulgaria, raised-relief map, wall, skis

Ramani ya eneo la Mlima wa Pirin kwenye ukuta wa Borovets, Bulgaria. Picha ya Global Voices, CC-BY.

Wanaharakati wa mazingira walifurahia pale mapema Aprili 26 mahakama kuu ya Nchini Bulgaria ilipofikia uamuzi kuwa Serikali haina budi kusitisha mpango wake wa kiruhusu ujenzi mpya karika hifadhi ya Taifa ya Purinmu, ambayo ni eneo la urithi wa Dunia la UNESCO, bila ya kufanya tathimini ya makakati wa mazingira.

Muungano ulioitishwa kwa ajili ya Mazingira ulianzisha sheria na na kuunga mkono uamuzi wa mahakama ikiwa ni moja ya hatua zao muhimu kwenye kupigania kulinda sehemu ya eneo lenye thamani kubwa.

Kwa mujibu wa WWF-Bulgaria, mmoja wa watu wa muungano huu:

Serikali imepanga kutoa kibali cha ujenzi kwenye eneo la ukubwa wa mara 12.5 zaidi ya eneo lililoruhususiwa kwa sasa, hali inayoweza kupelekea kudorora kwa uchumi, hali inayotarajiwa kuathiri karibu asilimia 60 ya hifadhi (kwa sasa hakuna shughuli yoyote ya kiuchumi inauoruhisiwa kwenye eneo la hifadhi). Utekelezaji wa mpango huu umefadhiliwa na Umoja wa Ulaya.

Hali ya hatari dhidi ya hifadhi ya Pirin ilipelekea maandamano ya miezi mitano mfululizo katika maeneo mbalimbali ya Bulgaria na nje ya nchi. Maandamano ya hivi karibuni yalifanyika huko Sofia, Blagoevgrad, Plovdiv, Sliven na London mapema Aprili 26, ambapo waandamanaji walitoa pia wito wa kulindwa kwa urithi.wa asili wa eneo la Bahari Nyeusi.

Maamuzi ya mahakama yalioindua maamuzi ya Wizara ya Mazingira na Maji ya nchini Bulgaria ya kukubali mpango wa usimamizi wa Hifadhi ya Purin kwa kipindi cha mwaka 2014-2020 bila ya kufanyika kwa tathmini ya kimkakati ya mazingira, ili kuruhusu ujenzi wa miundombinu mipya ya mchezo wa kuteleza kwenye theluji karibu na mji wa Bansko.

Wanaharakati waliofungua kesi mahakamani wanasema ujenzi kama huu utahatarisha hifadhi nzima na ni ukiukwaji wa agizo la Umoja wa Ulaya la 2001/42/EO, linalobainisha kuwa tathmini ya mazingira lazima ifanyike kwenye mambo yanayohusu utalii, sekta ya misitu na bayoanuai.

Mahakamailijenga hoja kuwa bila ya kufanya upembuzi yakinifu wa mazingira, “Wizara haikuwa na ushahidi wowote wa awali wa kufanya makadirio yoyote ikiwa utekelezaji wa maazimio kwenye mpango ulioandaliwa ungeweza kuwa na manufaa kwenye mazingira au la.”Jopo la majaji watatu liliweka bayana kuwa tathmini ya aina hii inapaswa kuzingatia vigezo vya Kanuni ya Upembuzi Yakinifu wa Mazingira, ambayo haijazingatiwa hadi sasa.
Pamoja na kuwa kwa kiasi fulani walisherehekea maamuzi ya Mahakama Kuu ya nchini Bulgaria, wanaharakati wa mazingira wa nchini humo wanachukua tahadhari na kuona kuwa huu sio mwisho wa jitihada zao za #kuokoaPirin, kwani wanatambua kuwa hila za matajiri wakubwa zinaweza bado kulitwaa eneo hill kwa ajili ya miradi ya kitalii. Kisheria, wizara inazo wiki mbili za kukata rufaa, ambayo itawasilishwa kwenye jopo la mawakili watano.

Vyombo vikuu vya habari nchini Bulgaria kwa kiasi kikubwa vinaendeshwa kwa mfumo kandamizi na hivyo kutokutangaza inavyotakiwa matukio haya, kolichofanyika ni ama kuonesha kuwa maandamano hayakuwa na madhara yoyoye na kwa uchache sana yalitiliwa maanani. Kwa mfano makala moja ya hivi karibuni inawaita wanaharakati hawa “wapokea hongo wa kijani” (Bul. зелени рушветчии).

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.