Kupiga Marufuku Wasichana Waliozaa Kurejea Masomoni, Inaweza Isiwe Suluhisho la Mimba Mashuleni.

Picha: PesaCheck.org

Makala hii ilichapwa hapo awali na PesaCheck.org, Nradi wa kwanza Afrika Mashariki kwa ajili ya kuthibitisha taarifa.

Rais wa Tanzania  Mheshimiwa John Magufuli amepiga marufuku wanafunzi wa kike kuendelea na masomo mara baada ya kujifungua.

Akiongea katika mkutano wa hadhara huko Chalinze, mji mdogo Mashariki ya Pwani, Rais Magufuli aliyakemea mashirika yasiyo ya kiserikali Tanzania kwa harakati zao za kutaka wasichana wanaopata mimba katika umri mdogo kuendelea na masomo baada ya uzazi: Akikiri kwamba kitendo hiki kinaliangamiza taifa na kuchangia mmomonyoko wa maadili

Kama msichana akipata mimba, iwe ni makusudi au kwa bahati mbaya, akazaa na akarui tena shuleni, atawafundisha na wengine. Halafu akipata mimba ya pili, azae na arudi tena shuleni. na tena kwa awamu ya tatu. Je, tunasomesha wazazi?

Sambamba na hilo, Mheshimiwa Raisi alipiga marufuku wanafunzi watakaozaa kabla hawajamaliza elimu ya sekondari kuendelea na masomo:

Nataka niwaambie, na hayo mashirika yasio ya kiserikali wasikie kwamba, katika kipindi hichi cha utawala wangu, hakuna msichana atakaezaa na kupewa nafasi ya kurudi shuleni kwa awamu ya pili.

Akishauri kwamba yapo mambo mengi ya kufanya ukiacha shule, kama vyuo vya ufundi na stadi za maisha, au hata kilimo.

Tamko hili la Rais lilienea katika mitandao ya kijamii, na idadi kubwa ya Watanzania wakitumia alama habari ya   #ArudiShule kupinga wazo hilo, ukizingatia idadi kubwa ya wasichana wa Kitanzania wapatao 8,000  wanaositisha masomo yao kwa sababu ya ujauzito kulingana n ripoti ya haki za binadamu.

Je, ni  kweli wanafunzi waliozaa wanaweza kuathiri tabia za wengine pindi wanaporejea mshuleni?

PesaCheck imefanya utafiti juu ya swala hili, kwa kuanzisha chombo cha kujitegemea  kwa wananchi kiitwacho Twaweza, na kugundua kwamba tamko la Mheshimiwa Raisi linakiuka yafuatayo:

Sababu za mimba za utotoni

Kufuatana na tafiti za Shirika la Afya na Makazi mwaka  (THDS) 2015–16  idadi ya mimba za utotoni Tanzania bara imeongezeka kwa asilimia 27. Je, ni sababu zipi zimechangia ongezeko hili?

Makala ya HakiElimu  baada ya kupitia mawazo ya wananchi juu ya hili iligundua kwamba miongoni mwa sababu ya ongezeko hilo ni kipato duni cha mwananchi. Makala hiyo inasema kwamba asilimia 31 ya wahusika (wakiwemo wazazi na mabinti wenye ummri wa kubalehe) wamefikiri kwamba sabu ni umaskini, hali ngumu ya uchumi imepelekea wazazi kuwaozesha mabinti zao  kwa sababu wameshindwa kuwatimizia mahitaji yao muhimu.

Ripoti ya  THDS inaonyesha kwamba idadi ya watoto wanaozaliwa hubadilika kutegemeana na ngazi za kiuchumi, hupungua pale uchumi wa watu unapoongezeka. Wenye uchumi wa juu huwa na umri mkubwa pale wanapopata wazawa wao kwa kwanza, ni dhahiri kwamba mama masikini huwa na umri mdogo pengine umri ambao wangetakiwa wawe wanajiendeleza kimasomo.

Sambamba na hilo, ripoti ya UNICEF inaonesha kwamba moja kati ya wasichana sita wa Kitanzania wenye umri kati ya miaka 15 hadi 19 ameolewa. Wasichana hawa wanaathirika kisaikolojia , yaani wengi wao huwa hawpti nafasi za kujiendeleza kimasomo bada ya haya.

Sababu nyingine iliyotolewa na makala ya HakiElimu  ni “malezi mabaya ya hawa wasichana kitendo kinachosababisha wasichana kushindwa kujizuia katika hali ya matamanio yao.” Wakigundua kwamba wazazi wengi hawana muda wa kuzungumza na kufuatilia maadili ya watoto wao pale wanapofikia umri wa kupevuka. Kuna pia suala la kukosekana kwa elimu ya uzazi. “Wazazi wengi huwa hawazungumzi na mabinti zao wanapovunja ungo.” Takwimu za TDHS 2015 zinaonyesha kwamba nusu ya wasichana hushiriki ngono chini ya umri wa miaka 16.

Ripoti hiyo ya HakiElimu ilisema kwamba mtazamo wa jamii pia juu ya thamani ya mtoto wa kike kuwa yeye ni mtu wa kuolewa tu, kuzaa na kuwa mama ilichangia kwa namna moja au nyingine katika hili.

Ripoti ya TDHS 2015–16 imeonyesha kwamba ongezeko la watoto wanaozaliwa linategemeana sana na kiwango cha elimu ikimaanisha kwamba wanawake ambao hawajaenda shule wana uwezekano wa kuwa na watoto mara 3.3 ikilinganishwa na wale walioko shule. Wanawake ambao hawana  elimu wana uwezekano wa kuzaa mara tano zaaidi ya wale waliohitimi masomo ya sekondari au elimu ya juu. TDHS mwaka 2010 sambamba na ripoti ya UNICEF  (p.12) iligundua kwamba kundi kubwa la wasichana huzaa wakiwa bado na umri mdogo huwa hawapo mashuleni.

Je, wasichana hawa ndio kichocheo cha mimba mashuleni?

Kulingana na THDS, Zanzibar inaongoza kwa kuwa na asilimia ndogo ya mimba za utotoni ukilinganisha na asilimia 8 bara. Zanzibar ilianzisha kauli mbiu ya arejee shuleni mwaka 2010 kama hili. Kenya iko kati ya Tanzania bara na Zanzibar kwa asilimia 18% ya mimba za utotoni. Na katika maeneo yote husika wanafunzi wnaojifungua hurejea mashuleni na bado hawajtufiki katika hili l kuongoza kutoa wasichn wengi wenye mimba za utotoni.

Kwa hivyo kusema kwamba kitendo cha kuwarejesha mashuleni ni kuchochea mimba za utotoni ni upotoshaji. Tafiti zimefanyika na sababu kuu za mimba za utotoni ni uchumi mbovu na kukosekana kwa malezi bora na uwajibikaji wa wazazi kwa mabinti zetu.

Je unahitaji kuthibitisha habari zilizosemwa na mwanasiasa au kiongozi yeyote wa uma kuhusu masuala ya fedha? Jaza fomu hii, au wasiliana nasi kwa kutumia mawasiliano haya hapa chini, na tutahakikisha hukatishwi tamaa.

Ripoti hii iliandikwa na Mshirika wa PesaCheck Mwegelo Kapinga, mshauri mwelekezi wa maendeleo, mtafiti na mwandishi. Mwegelo amefanya kazi na Twaweza Afrika Mashariki kama mchambuzi wa tafiti. Picha ya takwimu imetengenezwa na Mshirika kwa PesaCheckBrian Wachanga, ambaye ni mwanateknolojia ya kiraia wa Kenya anayependa kutengeneza takwimu zionekane vyema kwa macho. Ripoti hii ilihaririwa na Mhariri Mtendaji wa PesaCheck Eric Mugendi.

PesaCheck, iliyoanzishwa na Catherine Gicheru, ni mradi kwanza Afrika Mashariki unaothibitisha taarifa. Lengo lake ni kuwasaidia wananchi kupambanua ukweli na hisia kutokana kutangazwa kwa takwimu zinazoathiri dunia yetu, uzito ukiwa kwenye matangazo yanayohusu fedha za umma zinazoathiri utekelezajiwa kile kinachoitwa “Malengo Endelevu ya Milenia” au huduma za umma za SDG, kama vile afya, maendeleo vijijini na upatikanaji wa maji. Pesachecki pia inatafiti umakini wa habari zinazotangazwa na vyombo vya habari. Kufahamu zaidi kuhusu mradi huu, tembelea pesacheck.org.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.