Kubaki au Kuondoka Hakutoi Mustakabali wa Wakazi wa Al-Waer Nchini Syria

Mtoto akiwa amebeba taji la maua huku akiwa amejiinamia kwenye moja ya mabasi yanayotumiaka kuwahamisha wakazi wa Al-Waer. Madinat al-Maared Square, Al-Waer, Homs. Picha ilipigwa Machi 27, 2017. Chanzo: Maher Al-Khaled/SyriaUntold.

Makala haya yaliandaliwa kwa ajili ya Syria Untold na Jood Mahbani, mwandishi wa habari aliyeko huko Homs na mwanaharakati wa Kiraia, na kisha kutafsiriwa na . Kwa mara ya kwanza ilichapishwa Mei 8, 2017 na inachapshwa tena hapa kwa awamu mbili kama sehemu ya makubaliano ya kiushrikiano. Ifuatayo ni sehemu ya kwanza, isome.

Idlib, Jarablus, au eneo duni la Kaskazini mwa Homs?”

Hili ni swali ambalo limekuwa likiulizwa mara nyingi na wakazi wa jiji la Al-Waer nchini Syria, Magharibi mwa jiji la Homs na sehemu ya manispaa ya Homs pale wanapotaka kuelewa kila mmoja anapotaka kuelekea. Waasi pamoja na familia zao wanaihamisha ngome yao kutoka kwenye jiji hili lililobatizwa jina la “ Kitovu cha Mapinduzi,” kufuatia kuingiwa kwa makubaliano ya kutafuta amani yanayosimamiwa na Urusi na Uturuki.

Baada ya miaka sita ya vita, ambayo ilianza kama vuguvugu maarufu la kupinga serikali ya Assad,  ambao unaendelea kujihakikisha uwepo wake kwa kusaidiwa na matafia ya Urusi na Iran.

Kwa mujibu wa makubaliano yaliyotiwa saini Machi 13, 2017 na wawakilishi wa serikali pamoja na Kamati ya Ujirani ya Al-Waer, mpango utakaotekelewa kwa awamu, hadi mtu wa mwisho kuhitaji kuondoka mjini hapo, wakati ambao mji huo utakabidhiwa kwa wanajeshi watiifu wa Serikali ya Syria.

Kwa kuwa hakujakuwa na taarifa za uhakika zilizotolewa, wakazi wengi wameamua kuhatarisha maisha yao kwa kwenda “kusikojulikana” badala ya kusubiri “lisiloepukika” kwa mujibu wa Ibtisam Al-Masri, mama wa watoto wannne. (Majina ya kubuni yametumiwa kwenye makala haya kwa sababu za kiusalama.)

Aliwaza kuwa, madhara ya mjini hapo yanaweza kufanana na yale ya Aleppo Mashariki. “Hawataacha chochote kikiwa salama,” aliongeza, kabla hajapanda kwenye moja ya mabasi ambalo linachukua awamu ya tano ya watu wanaohamishwa kuwapeleka kwenye jiji la Jarablus. “Watalipiza visasi kwa kila atakayesalia, ndio maana mimi ninaondoka… hakuna namna ninaweza kubaki na kushuhudia wakituua na kuharibu makazi yetu.”

Kituo cha Habari cha Upinzani kinasisitiza kuwa miji ya Homs ipo kwenye hatari ya kuangukia kwenye mpango maalum wa kuhamisha wakazi unaoratibiwa na serikali ya Syria, kama ilivyokuwa kwenye majiji ya Daraya, Al-Qusayr na Aleppo Mashari, ambapo majiji yote yalizingirwa na majeshi na baadae kukimbiwa na wakazi.

Hatahivyo, hali katika jiji la Al-Waer haieleweki na ni ngumu sana, na haijafahamika wazi ikiwa serikali ipo tayari kuwaondoa wakazi wote kabla ya kuzingira jiji kwa wanajeshi wake.

Kuhamishwa kwa wakazi wa jiji la Al-Waer kumekuwa na upekee wa kuruhusu raia wanaomiliki vitu kuingia kabla ya majeshi ya serikali kufanya hivyo. Pia kulikuwa na uhuru wa wale wanaopenda kubaki tofauti na hali ilivyokuwa huko Aleppo Mashariki kwa mfano, ambapo raia wote waliondolewa kabla ya kuingia kwa majeshi ya serikali.

Hata hivyo, kukosekana kwa imani dhidi ya mkakati wa Urusi wa kuhamisha watu, ambaye ndiye mfadhili mkuu, sambamba na uwepo wa wanajeshi kwenye vijiji vya Shiite vilivyo karibu na Al-Waer (Zarzuriya, Hayek na Mazraa) imesababisha kuenea sana kwa hofu mjini hapo. Kumekuwa na kusambaa kwa tetesi kuwa kuna wanamgambo wa Shiite huko Kwenye kijiji cha Mazraa (kinachopakana na al-Waer) wakisubiri kuondoka kwa kundi la mwisho la waasi ili wawavamie raia watakaokuwa wamesalia pamoja na kuwanyanyasa.

Kutokana na hali hii, raia wamejikuta kwenye mkwamo wa kupotea kwa matarajio ya kuhamishwa na kuangamizwa, kwa namna moja, au wabakie kwenye jiji lisilokuwa na hatma inayoeleweka, kwa upande mwingine, ambapo kwa kila upande, inakuwa ni vigumu sana kufanya maamuzi.

‘Sitaki kuiacha nyumba yangu, vitu vyangu, historia yangu’

Hayyan Al-Siufi (30), mwanaharakati wa kiraia alibainisha kuwa, miaka mitano iliyopita aliyoitumia kwenye janga hili kuwa ni “miaka iliyopotea”

Aliiambia SyriaUntold kuhusu hali tete za milipuko ya mabomu, kuzungukwa na wanajeshi na kuharibiwa kwa miundombinu huku akijutia kosa la kutokuamua kuhama tangu kuanza kwa hali ya sintofahamu ya vita nchini Syria. the harsh conditions of bombardment, besiegement and destruction of infrastructure, admitting his regret for not having decided to emigrate since the beginning of the armed turmoil in Syria. “Sifahamu, kwa nini mambo yalikuwa hivi?” aliongeza kwa mshangao. “Kwa nini tumekuwa kimya? Matokeo yake ni kuhamishwa kwa namna hii na kuacha nyumba zetu na wapendwa wetu?”

Hayyan ni mmoja wa maelfu ya vijana wa Al-Waer walio na sifa ya kujiunga na jeshi au kujiunga na vikosi vya dharura na aliyeamua kubakia kwenye eneo lililozungukwa na waasi tangu mwaka 2011 bila ya kusafiri kwenda ng'ambo. Walikuwa na matumiani kwamba, ipo siku vita vingekuja kumalizika, na hivyo kuondolewa kwenye utumishi jeshini au kuwepo kwenye majina ya vikosi vya dharura.

Hata hivyo, pale uhamishaji wa watu ulipoanza rasmi, na zikiwa zimebaki wiki chache kabla ya kukamilika kwa kundi mwisho, wengi wao waliamua kujiandikisha kwa ajili ya kuondoka. Walikataa kubakia kwa hofu ileile ya utumishi wa walima kwenye majeshi ya serikali ya Syria.

Zaidi, kama wanaume wa miaka chini ya 40 kwa haraka wangeamua kuhamia maeneo yaliyo chini ya umiliki wa upinzani, huu ungekuwa ni uamuzi mgumu sana kwa familia na ndugu zao. Mambo haya yangekuwa ni mjumuiko wa vipaumbele, wajibu, hofu na na matarajio.

Pasipo kujua wafanye nini kati ya kutamani kuendelea kuwepo kwenye asili yao sambamba na kuondoka kwa watoto wao, familia nyingi zimegawanyika kuhusu uamuzi wao, ambapo baadhi yao wakisitisha uamuzi wao kujiandikisha kwa ajili ya kwenda eneo fulani na kuwasilisha tena mara kadhaa.

“Tulijisajili kwa ajili ya kwenda Idlib ili baadae tuelekee Uturuki. Tulikuja kugundua kuwa, kuingia nchi nyingine kinyemela siyo kitu rahisi na si la gharama nafuu, kwa hiyo tuliamu akubadili na kuelekea Jarablus,” alisema Umm Rami, akithibitisha uwepo wake na kundi la wakazi kwenye moja ya vituo vya kujisajili pamoja na kuisha kwa muda wa kuchagua eneo la kwenda.

Wakati alipokuwa anaongea na SyriaUntold, iligundulika kuwa Umm Ramialikuwa ni mwajiriwa serikalini, na pia mume wake alishazidi umri unaohitajika kwa ajili ya kufanya kazi kama mwanajeshi wa dharura. Hata hivyo, waliamua kuondoka na watoto wao watatu bila kujali.

“Mkubwa kabisa na umri wa miaka 26, na anhitajika kama mwanajeshi wa dharura, wa kati ana umri wa miaka 20 na anahitajika kwa ajili ya utumishi wa lazima, na wa mwisho ana umri wa miaka 15, ikiwa na maana kwamba anakaribia umri wa kujiunga na jeshi”

Akifunika shingo yake kwa viganja vyake kama namna ya kukabiliana na hali ya hofu, aliongeza kwa sauti ya ukali: “Nina hofu ya kushindwa. Sipendi kuiacha nyumba yangu, vitu vyangu, lakini pia siwezi kuwaacha watoto wangu katika umri huu.”

Kwenye vituo kwa ajili ya kwenda kwenye vituo walivyopangiwa watu (Idlib, Jarablus, Homs northern countryside), watu wanashauriana na kupeana taarifa zilizopatikana na wale waliokwishatangulia kwenye moja ya maeneo wnayopaswa kwenda.

Baadhi ya kauli za kutia moyo, zimekuwa zikisemwa zaidi ya mara moja na watu kadhaa zenye kuchukua sura ya maneno matakatifu katika tahajudi zimekuwa zikisambaa maeneo ya jirani kama taarifa za kisayansi. “Idlib ina nyumba za kupanga za bei nafuu,” “Tatizo la Idlib nin kwamba ni mji wa hatari na kuna mashaka ya kulipuliwa,” “Wale wanaochagua Idlib ni kama vile wamechagua kwenda Uturuki kwa kutumia njia haramu,” “Majeshi ya serikali yatawashikilia wote watakaokuwa maeneo ya jirani” “Jarabulus ni salama, ila ni vigumu kujihakikishia kuishi,” “ Kama uliweza kuishi kwenye hema basi unaweza kwenda Jarablus,” “Maeneo ya Kaskazini mwa vijijini hivi punde yatakabiliwa na janga lililoikuta Al-Waer.”

Umm Rami anang'aka kutoka kwenye kundi la wanawake wanateta, anawaacha wanawake hawa nyuma yake ili waendelee na maongezi yao. Anaivuta miguu yake kwa shida, anayazuia machozi yake lakini hata hivyo yanatiririka kutoka machoni kwake. “Haya yote hayana maana,” aliliambia SyriaUntold. “Tunajazwa taarifa na kufurahishwa kwa taarifa za sehemu ipi ni nzuri za kule tunapokwenda, Idlib au Jarablus… lakini tunakosa kitu cha muhimu: Kote ni sawa tu! Tunaondoka!”

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.