‘Kwa nini Siwezi Kumbusu Mpenzi wangu wa Kike Hadharani?’ Simulizi ya Mwanamke Basha wa Armenia

Picha: Anna Nikoghosyan kwa ajili ya OC Media. Picha zote zimetumiwa kwa ruhusa.

Lifuatalo ni toleo la makala ya ubia  iliyoandikwa na na kuchapishwa kwa mara ya kwanza kwenye tovuti ya OC Media.

Nilikuwa na umri wa miaka 19 ndipo nilipokutana na msichana msagaji aliyetokea kunipenda. Nilimueleza kuwa sikuwa miongoni “mwao” lakini, bila kutarajia, nilimbusu. Nilikuwa naye na hapo ndipo kwa mara ya kwanza nikafahamu nini maana ya upendo.

Eva (ambalo si jina lake halisi), mwenye miaka 24, ni mwanamke msagaji anayeishi Yerevan. Alipitia hatua nyingi katika kutambua jinsia yake. Kwanza, ilikuwa ni jambo la kawaida sana kujitambulisha kama mwanamke wa kupenda kufanya ngono na mtu wa jinsia tofauti na yake, ambapo, hata hivyonayo baadae alijiweka kwenye kundi la mwanamke wa kupenda ngono ya jinsia zote mbili. Alipogundua mahaba yake kuwa yalikuwa kwa watu wasioweza kuitambulisha jinsia zao, hapo alijiona kuwa kumbe alikuwa mwanamke asiyekuwa na jinsia mahususi. Kwa sasa, hapendelei tena kujihusisha na aina yoyote ya jinsia au kutafuta namna yoyote ya kuelezea jinsia yake.

“Mimi ni mtu ninayempenda mtu mwingine; Mimi ni basha,” anasema.

Parandzem na Taguhi. Picha: Anna Nikoghosyan kwa matumizi ya OC Media

‘Parandzem na Taguhi walikuwa wakifanya mapenzi usiku kucha’

Kwenye uso wa jengo kuu lililopo katikati ya jiji la Yerevan, kuna mchoro unaosomeka, ‘Parandzem na Taguhi [majina mawili ya wanawake wa Armenia] wamekuwa wakifanya mapenzi usiku kucha’. Michoro huu unaohamasisha nafasi ya mwanamke katika eneo la jiji linalotawaliwa zaidi na wanaume, kimsingi ni utaratibu wa kinguvu unaojulikana sana wa kueneza msemo toka enzi za kale toka enzi za kale: ‘Parandzem na Taguhi wamekuwa wakipika tambi usiku kucha’.

“Kwa hakika, hii inawahamasisha watu,” Eva anasema,lakini bila ya kuweka bayana ni nani aliyeandika maneno haya.

Mabasha ni miongoni mwa makundi ya watu wanaotengwa sana na kunyanyaswa nchini Armenia. Utafiti wa mwaka 2016 uliokuwa na kichwa cha habari ‘ Jinai za Chuki na Matukio mengine yanayoshadiwa na chuki thidi ya watu wa LGBT nchini Armenia’ uligundua kuwa kati ya watu 200 mabasha waliohojiwa kwenye utafiti huo, 198 walikuwa wahanga au walishuhudia makosa ya jinai yaliyosababishwa na chuki au matukio ya makosa mengine yaliyochochewa na chuki.

Kwea kutambua umuhimu wa kusitisha machafuko na chuki dhidi ya mabasha, wanaharakati lukuki na waangalizi wa haki za binadamu nchini Armenia wameanzish harakati za kulinda haki za mabasha, usawa pamoja na kukomesha unyanyasaji. Hata hivyo, wakati harakati za kutafuta haki za mabasha zikiendelea, sauti za wasagaji, watu wanaovutiwa na jinsia zote na wanawake na wanawake walio na tabia za kiume bado hazijasikiwa vya kutosha.

“Kwa ujumla, kwa namna hali wanayoishuhudia wanawake walio wengi, simulizi za wanawake wa LBT bado hazijawekwa bayana,” Eva anasema.

Kwa maoni yake, katika jamii ambayo karibu wanawake wote wanakabiliana na vikwazo katika kusemea mambo yao, ni vigumu hata wa wanawake walio na mtazamo wa kuvutiwa na watu wa jinsia tofauti na wao kujadili hali zao.

“Kila kitu tunakifanya kwa usiri”

Wanawake mabasha nchini Armenia, kwa wakati mmoja wanakabiliana na ukandamizaji wa kila namna unaolenga jinsia na utambulisho wao wa kijinsia. Kwa kuwa hakuna bahati ya kupata fursa ya kuelezea changamoto zao, wanawake mabasha wana hatari kubwa ya kuathirika kisaikolojia na pia pia kushindwa kuweka bayana hisia zao kwa jamii.

Mashinikizo kama haya wakati mwingine hupelekea hali ya kufadhaika na kuingiwa na kukumbwa na hofu kubwa.

“Tunafanya kila kitu kwa usiri. Kuna sehemu ndogo sana ya jamii ambazo ninaweza kujisikia mwenye amani, lakini niwapo nyumbani, na miongoni mwa marafiki na ndugu zangu, siwezi kuonesha uhalisia wangu” anasema Eva.

Kutengwa pamoja na matatizo ya kihisia ni moja ya changamoto wanazokabiliana nazo wanawake mabasha nchini Armenia. Eva anasema kuwa ikiwa haiba ya ujinsia wa basha itawekwa bayana, mtu wa namna hiyo anaweza kukabiliana na “jaribio la kuhitajika kimapenzi na mtu wa jinsia tofauti” pale wanaume wa mapenzi ya jinsia tofauti wanapojaribu kuonesha “uhalisia” wao kwa mhanga.

Polisi hawezi kuwa na msaada

Hatari za kiusalama dhidi ya wanawake mabasha ni jambo la kawaida sana nchini Armenia. Eva anaelezea ni kwa kiasi gani, mara baada ya kutoka kumbi za starehe au mgahawani, au pale anapotembea mtaani akiwa na mpenzi wake wa kike, amekuwa akifuatwa na wanaume mara kwa mara.

“Huwa ninaogopa sana kwani sifahamu ni jambo ganni linaweza kunikuta. Mwanaume yupo ndani ya gari, na akiwa na nguvu kuliko mimi. Anaweza kufanya lolote atakalo bila hata ya mtu yeyote kujali.”

Eva haamini kama polisi wanaweza kumsaidia kwani hata akienda kwao kwa ajili ya kuhitaji ulinzi, polisi watamdhihaki kwa sababu ya utambulisho wake wa kijinsia na pia kuumuliza maswali ambayo yatamfanya asijisikie vizuri. Hili limetokea mara nyingi sana kwa marafiki zake wasagaji, anasema Eva.

Kuna wakati Eva na rafiki yake wa kike walishambuliwa na wanaume wakiwa sehemu ya mapumziko, ambapo watu hao waliwapiga na kuwatukana. Wanaume wengine waliokuwepo eneo la tukio, badala ya kusaidia kuwazuia wahalifu hao, wao walishinikiza akina Eva kuacha kufanya laana kwani katika eneo lile walikuwepo pia wanawake kama wao. “Kwa hiyo, ilikuwa sawa kabisa kwa wao kutupiga, hata ivyo, walipaswa kufanya hivyo kimya kimya, sawasawa kabisa na namna wanavyowapiga wanawake wao majumbani” anasema Eva.

‘Unapaswa kujaribu na mwanaume ili ufahamu mapenzi ya kweli ni yapi’

Wakati bado kukiwa na mwendelezo wa vitisho na ukatili dhidi ya wanawake mabasha, uhusiano wa wanawake wasagaji bado pia haujatiliwa maanani. Matamko kama vile “yeye ni msagaji kwa kuwa bado hajampata mwanaume wa kweli” na “unapaswa kujaribu mapenzi na mwanaume ili ufahamu ‘mapenzi ya kweli’ ni yapi’ yamekuwa mambo ya kawaida kabisa.

Wanawake wasagaji wanaonekana kama vitu kwa wanaume. Kwa walio wengi, msagaji ni mwanamke wa mapenzi kutoka kwenye video za mapenzi aliyepo kwa ajili ya wanaume kujichagulia na kutmiza matakwa yao ya kimapenzi.

“Mara nyingi wanaumee walikuwa wakinijia mimi na rafiki yangu wa kike na kutuomba tufanye nao mapenzi. Pale tulipowakatalia, waliomba ikiwa angalao tungeweza kufanya mapenzi mbele yao,” anasema Eva.

Mashinikizo kutoka kwenye Familia

Changamoto wanazokabiliana nazo wanawake mabasha nchini Armenia hazitokani tu na jamii inayowazunguka. Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Pink Armenia na Socioscope, mabasha mara kwa mara wamekuwa wakikabiliwa unyanyaswaji wa aina tofauti tofauti kutoka kwenye familia zao kama namna ya kuwaanya waachane na utambulisho “usio sahihi” wa jinsia zao.

Wazazi wa Eva hawafahamu kuhusu hali ya jinsia ya mtoto wao. Hata hivyo, kwa mujibu wake, anajisikia mwenye bahati, kwani hakuna chuki yoyote katika familia yake dhidi ya kundi lolote.

“Wengi wa marafiki wangu wa LGBT wanakuja katika nyumba yetu. Hata wapenzi wangu wa kike wanakuja. Sote tunakunywa kahawa na mama yangu. Kwa kweli anawafurahia sana.”

Kuna wakati mama yake Eva alimuuliza ikiwa Eva alikuwa msagaji. Hata hivyo, Eva hakuwa tayari kumwambia ukweli mama yake na kwa hivyo, alimdanganya. Baadae alijuta sana kwa uamuzi wake, kwani kutoka kwake ilimuwia vigumu sana.

Pamoja na uvumilivu kutoka kwa ndugu wa familia yake, Eva bado anakabiliana na changamoto ya kisaikolojia kutoka kw ndugu zake. Bibi yake Eva anamuona Eva kuwa ni mwanamke aliyekosa mume. Kuna wakati mama yake Eva alimuuliza ni kwa nini haolewi, Eva naye alimuuliza mama yake swali kama hilo.

“Nilisema, ‘sikuombi uwe na mtoto ili nimpate mdogo wangu, ninafanya hivyo? kwa nini basi nawe unanilazimisha nikuzalie mjukuu na niwe na mume? Baada ya majibzano haya, hawakuwahi tena kuwa na maongezi ya namna hii na mimi.”

Kuna kosa gani kumbusu hadharani umpendaye?

Kwa upande mwingine, Eva haogopi kuweka bayana kuhusu uhalisia wa jinsia yake. Hata pale ma rafiki zake wa zamani wanapowazungumzia mabasha kama namna ya chuki kwa kusema kuwa wanapaswa kuchomwa moto na kuuawa.

Eva alisema kuwa aliwaambia wamchome moto au wamuue, kwani naye alikuwa msagaji– miongoni ‘mwao’ –pia. Eva alisema kuwa kauli yake iliwafanya marafiki zake watafakari upya kuhusu tabia yao ya kuddhalilisha na ujinga walio nao.

Kwa upande wa rafiki yake na Eva, ambaye anatokea nchi nyingine, namna watu wanavyomtazama yeye na mpenzi wake wa kike pale wanapotoka pamoja, ni jambo linalomshangaza. Kila mara wanapokuwa kwenye kituo cha basi, mpenz wa Eva humsogelea na kumbusu kabla hawajaingia kwenye basi. Hata hivyo, Eva hujisikia kukataa, lakini kwa upande mwingine anajiuliza kuna kosa gani kumbusu hadharani mpenzi wake.

Eva anaamini kwamba hasingekabiliana na changamoto kama hivi kama angekuwa kwenye uhusiano wa jinsia tofauti. Anakumbushia enzi za miaka ya mwanzo ya ujana wake, pale alipokuwa kwenye mahusiano na mvulana mdogo.

“Tuliweza kutembea kwa uhuru, tukiwa tueshikana mikono, na hakuna hata mmoja aliyetufuatilia. Kinyeme chake, kwenye mahusiano ya jinsia moja, anasema Eva, maisha yamekuwa ya hofu na kudanganya kwingi; maisha yasiyoeleweka ambayo kila mara yanahitaji kufikiri kupita kiasi.

‘Nipo kwenye mahusiano ya kimapenzi, na ninahitaji kuwa na uwezo wa kulisemea hili’

“Sijui ni kwa nini ninalazimika kumdanganya mama yangu.Nina mtu ninayempenda, nina mapenzi ya dhati kabisa kwake, kua jambo gani litakalozidi hili? Nipo kwenye mahusiano ya kimapenzi na ninahitaji kuweza kuongea na watu wengine kuhusu hili. Tunaishi maisha ya upendo baina yetu, tunatoka pamoja, tunakwenda mighawani, tunacheza, na tunavuta sigara pamoja. Hivi kwani haya siyo mambo mazuri? Watu wanapaswa kutuheshimu, au siyo? Lakini hapana, hakuna aliye na furaha; watu wanachotaka kufanya ni kutaka kutuua tu” Anasema Eva huku sauti yake ikianza kuwa iliyojawa na hofu.

Kila mara Eva anafikiria kuihama nchi yake.  Utafiti uliofanywa nchini humo unaonesha kuwa kwa mwaka 2011–2013 pekee, takribani raia 6,000 wa Armenia walisafiri nje ya nchi yao kutokana na aina fulani ya unyanyaswaji. Jamii ya watu wasioweza kuwachukulia wengine inaweza kuwwa sababu kuu ya kumuathiri mtu mwingine isaikolojia.

Hata kupata msaada kutoka kwa wataalamu wa saikolojia ni jambo gumu, kwani wanasaikolojia wanaowatazama mabasha kwa hali ya uchanya na walio uelelewa wa changamoto za mabasha wenye mahitaji tofauti ni wa nadra sana.

“Nnatambua kuwa ninazo harakati halisi sana ndani mwangu. Pengine ninapaswa niendelee kuwepo hapana kujaribu kuibadilisha jamii yangu au kwa kuwa nina nafasi moja tu ya kuishi, niende mahali salama ili niwe na maisha ya kesho yaliyo ya furaha?”

Homofobia: Kifaa cha kisiasa kilicho vitani

Pich: Anna Nikoghosyan kwa ajili ya OC Media

Eva anaamini kwamba unyanyasaji dhidi ya watu wa mapenzi ya jinsia hvi karibuni imekuwa ni jambo lilishika kasi sana nchini Armenia, nchi iliyo ya kijeshi inayoongozwa na hofu ya wakati wote ya kuingia vitani na jirani yake Azerbaijan. Hata wale ambao katika hali ya kawaida hawakupaswa kuwa na tatizo na mabasha wanaonesha chuki, mtazamo ya ubaguzi dhidi ya watu wajinsia moja kwa kuwa tu ni jambo la kawaida kufanya hivyo.

Zaidi, mabasha mara kwa mara wamejikuta wakiwa wahanga kwenye michezo ya kisiasa. Pale siasa za ndani zinapokuwa kwenye mnyukano mkali, katika nchi inayozidi kudidimia kiuchumi, katika hali isiyotarajiwa makala kuhusu mabasha zinaanza kujitokeza kwa wingi na kisha watu wanahamisha mjadala kutoka kwenye mikwamo ya serikali hadi kwenye ‘kulinda tunu na tamaduni za raia wa Armenia’.

Miongoni mwa mifano iliypo ya hili ni shambulio la arson kwenye ukumbi rafiki kwa mabasha siku mbili mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2012 na harakati dhidi ya ‘utambulisho wa jinsia” mwaka 2013, mambo yaliyoibuka pale Armenia ilipokuwa na mcchakato wa kuchagua kati ya kuingia makubaliano ya ushirika na Umoja wa Ulaya na kujinga na Umoja wa Kiuchumi wa Eurasia unaoongozwa na Urusi.

Kwa maana hii, mabasha nchini Armenia wanachorwa kama ‘maadaui’ na vyombo vvya habari vya nchini humo. Katika mazingira haya, wanawake mabasha ndio haswa wanaolengwa.

Eva anafikiri kuwa kwa nchi changa iliyo katika janga la vita, kama ilivyo kwa Armenia, ambapo maisha ya watu yanagubikwa na harakati zao za kutafuta kuishi, haki za wanawake na haki za mabasha siyo kipaumbele.

“Kama kwa leo hakuna mtu aliyepoteza maisha, kila kitu ni chema” anasema Eva. “Kwa hiyo, kwa kuwa Armenia ipo kwenye wimbi zito la vita na ni moja ya nchi iliyo na misingi ya kijeshi ulimwenguni, kuna uwezekano mdogo sana wa kupata mabadiliko tunayoyahitaji” anahitimisha na kuwasha sigara yake ya mwisho iliyokuwa imesalia.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.