Watumiaji wa Mitandao ya Kijamii wa Trinidad & Tobago Wamjibu Mshauri wa Trump kwa Kuja na ‘Ukweli Mbadala’

"Soldiers and Airmen from the Florida National Guard look on as President Donald Trump takes the oath of office during the 2017 Presidential Inauguration." Photo taken from The National Guard flickr page, CC BY 2.0.

“Wanajeshi na Wanaanga kutoka Kikosi cha Taifa Florida wakimtazama Rais Donald Trump akila kiapo cha kukabidhiwa madaraka wakati wa tukio la kuapishwa kwa Rais mwaka 2017.” Picha imechukuliwa kutoka kwenye ukurasa wa mtandao wa Flickr wa National Guard, CC BY 2.0.

Katika enzi za habari za kupikwa, ambapo wakati mwingine watumiaji wa mtandao hulazimika kufanya kazi ya ziada kupembua habari sahihi na propaganda, kuna maneno mapya, yaliyoanzishwa na mshauri wa Rais Donald Trump aitwaye Kellyanne Conway: “ukweli mbadala”.

Maneno hayo yalitamkwa wakati mahojiano na kipindi cha televisheni kinachoendeshwa na kituo cha NBC kiitwacho Meet the Press, ambapo alikuwa akitetea madai yasiyo na ushahidi wowote ya mwandishi wa habari wa Ikulu ya nchi hiyo, Sean Spicer, kwamba “huu ulikuwa ni umati mkubwa kuwahi kushuhudia tukio la kuapishwa kwa rais — bila swali — iwe ni kwa mahudhurio au kutazwa duniani kote”.

Inaripotiwa na vyombo vikuu vya habari —na kuenezwa na mitandao ya kijamii —kwamba umati uliojitokeza kushuhudia kuapishwa kwa Trump haukuwa mkubwa kama ule wa Obama mwaka 2009:

Ulinganisho wa idadi ya watu waliojitokeza kushuhudia kuapishwa kwa Donald trump na Barack obama

Dakika hiyo hiyo ambapo Conway alisema kuwa Spice alikuwa akitoa “ukweli mbadala” na kwamba “hapakuwa na namna ya kujua idadi halsii ya wahudhuriaji”, mwandishi Chuck Todd aliyaelezea matamshi hayo kama “uongo unaoweza kuthibishwa”. Alisema kwamba kama Spice anaweza kudanganya kwa jambo dogo kama hili, tafsiri yake ni kuwa “anadhalilisha uhalali wa idara ya mawasiliano ya Ikulu ya nchi hiyo”. Conway alimtuhumu Todd “kupiga siasa nyepesi”.

Awe amefanya siasa nyepesi au hapana, watumiaji wa mtandao wa Trinidad na Tobago — kama wenzao wa duniani kote — waligeuza maneno hayo kuwa alama ishara ya vichekesho kwenye mtandao wa Twita.

Mtumiaji wa facebook Keith Francis alisema:

Ringling Brothers imefungwa kuotea mashindano yanayoendeshwa na serikali ya Marekani.
#alternativefacts

Msanii Christopher Cozier alishangazwa, na kubandika andiko hili:

Kwa hiyo…mtazamo wangu unatengenezwa na ‘ukweli mbadala’

Raia wa Trinidadi David Rudder, ambaye mara nyingi huwafurahisha wafuasi wake kwenye mtandao wa Facebook kwa maoni yake yaliyojaa werevu, aliweka bandiko hili zuri, ambapo alijifananisha na nyota maarufu wa muziki wa soca Machel Montano:

shoo yangu ilikuwa na watu kumi zaidi ya wale wa shoo ya machel, lakini vyombo vya habari vinavyopendelea haviwezi kusema hivyo.
Nilipoanza kuhesabu kiasi cha wanawake pekee waliohudhuria nilifikia elfu saba, kisha nikachoka. Lakini vyombo vya habari haviwezi kusema hivyo. Mwuulize msemaji wangu Kelly Ann Converse, nyota wangu anayeweza kuwa tayari kufanya lolote kwa ajili yangu, atakwambia

Mtumiaji wa Facebook Nigel Thompson alitumia dhana ya “ukweli mbadala” kuhalalisha ongezeko kubwa la uhalifu nchini Trinidad na Tobago:

siku 20 watu 35 wamekufa.
COP [Kamishna wa Polisi]: uhalifu mkubwa umepungua.
#alternativefacts

Laura Dowrich-Phillips, ambaye ni mweusi, aliamua kutania kwenye alama habari hiyo kwa mambo binafsi:

Mimi ni msichana mwekundu [mweupe] lakini mweusi #alternativefacts

Franka Philip, wakati huo huo, alichekesha:

Kellyanne Conway alikuwa anatumia uhusika upi kwenye riwaya za Harry Potter? Au ndio alikuwa horcrux?

Watumiaji wa mitandao ya kijamii walikuwa na wasiwasi zaidi ya kushangazwa, hata hivyo. Kama mtumiaji mmoja wa raia wa Trinadadi waishio nje ya nchi alivyoliweka jambo hili:

ukweli mbadala… (?!)
orodha ya kusoma kwa lazima kwa 2017 – kazi zote za george orwell.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.