Mazungumzo ya GV: Global Voices Kutangaza Habari za Uchaguzi wa Marekani (MUBASHARA mnamo Desemba 26, Saa 11 Jioni GMT)

Trump, Hillary au Stein? Hata kama waandishi wetu wengi wa Global Voices hawataweza kupiga kura nchini Marekani, tunajisikia kuguswa kwenye uchaguzi huu wa Urais kama ilivyokuwa kwenye chaguzi nyinginezo.

Maswali yanayotujia akili: Je, Marekani itakuwa na ushirikiano zaidi na mataifa mengine au itajitenga? Je, rais mwanamke wa Marekani atabadili hali ya mambo kwa wanawake duniani? Je, Marekani itakuwa mahali magumu zaidi kwa wahamiaji au makundi ya wachache kuishi?

Ili kupata maoni na mtazamo wetu kila Jumatano, kuanzia Oktoba 26 mpaka Novemba 9, waandishi wetu wanne wa Global Voices watakutana na kuzungumzia habari zitakazokuwa zikijiri kutoka katika uchaguzi huo, kile ambacho watu wa nje ya Marekani wanakifikiri, na namna gani waandishi wetu wa ki-Marekani –wanaosafiri duniani kote na wenye uelewa wa michakacho mbalimbali ya kisiasa katika nchi nyingine –wanavyouona uchaguzi huu.

Kipindi chetu cha kwanza kati mfululizo wa vipindi vitatu kitakuwa na mazungumzo makali na mazuri kati ya mhariri wetu wa mitandao ya jamii anayeishi Beirut Zuhour Mahmoud, mhariri wetu wa Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini Joey Ayoub, mpiga kura wa Marekani anayeishi Amsterdam na mwandishi wa Iran Tori Egherman, na Sahar Ghazi, mpiga kura wa Marekani anayeishi San Francisco na mhariri mtendaji wa Global Voices.

Ungana nasi na tutumie maswali kupitia zana (app) ya Q and A.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.