Masaa yaliyopita, mdahalo wa tatu na wa mwisho wa urais nchini Marekani ulimalizika, na kumaliza majibizano makali kati ya Hillary Clinton na Donald Trump ambayo kwa mara nyingine uliitaja Urusi na rais wake, Vladimir Putin, mara nyingi sana. Mradi wa RuNet unaoangazia habari za Urusi unapitia twiti zilizoandikwa usiku wa mdahalo huo na shirika kubwa la habari la Urusi ili kupata picha ya kile kilichoendelea jijini Moscow.
Likiwa na zaidi ya wafuatiliaji milioni tatu kwenye mtandao wa Twita, RIA Novosti lilikuwa shirika kubwa zaidi la habari lililokuwa likitoa habari mubashara wakati wa mdahalo huo. Twiti zifuatazo zilizoonekana kwa mpangilio wa muda wa kuonekana kwake.
Twiti ya kwanza ilionekana kama dakika ya 30, wakati Hillary Clinton alipotaja madai ya serikali ya Marekani kuwa Urusi inaipeleleza nchi hiyo:
Клинтон заявила что Россия “шпионит” за американцамиhttps://t.co/ufZJlThpAX pic.twitter.com/pb8DVOu0tg
— РИА Новости (@rianru) October 20, 2016
Clinton anatangaza kwamba Urusi “inawapeleleza” Wamerekani.
Matumizi ya maneno ya shirika hilo la RIA yalionekana kulenga kuwafurahisha wasomaji wa Urusi, ambao Kremlin amekuwa akidai wako hatarini kupelelezwa na serikali ya Marekani, akitumia taarifa zilizotolewa na watu kama Edward Snowden na wengineo.
Трамп рассказал, почему Клинтон “не любит Путина” https://t.co/5gpzxwDTlZ pic.twitter.com/F8sug6wlNt
— РИА Новости (@rianru) October 20, 2016
Trump anatoa sababu kwa nini Clinton “hampendi Putin”
Путин хочет использовать Трампа как марионетку на посту президента США, считает Клинтон: https://t.co/HcgjfJfjql pic.twitter.com/eD4ppRGdiA
— РИА Новости (@rianru) October 20, 2016
Putin anataka kumtumia Trump kama kikaragosi kwenye serikali ya Marekani, ndivyo anavyoamini Clinton.
Трамп заявил, что благотворительный фонд семьи Клинтон является “преступной организацией” https://t.co/NURKLw6GwI pic.twitter.com/552cE6tJFa
— РИА Новости (@rianru) October 20, 2016
Trump anatangaza kwamba Taasisi ya misaada ya Clinton ni “Shirika la Kihalifu.”
Трамп заявил, что Асад намного умнее Клинтон и Обамы https://t.co/kzuBsKGIuo pic.twitter.com/74isHq8CAF
— РИА Новости (@rianru) October 20, 2016
Trump anatangaza kuwa Assad ana akili zaidi kuliko hata Clinton na Obama.
Трамп пообещал отменить реформу здравоохранения Обамы https://t.co/bflsAw5ctl pic.twitter.com/4ZY5FFoDRU
— РИА Новости (@rianru) October 20, 2016
Trump anaahidi kufutilia mbali mpango wa mabadiliko ya huduma za afya nchini humo.
Kwa ujumla, shirika la habari la RIA lilichagua kuweka mkazo ziaid kwenye matamshi ya Trump, kwa lengo la kupata ufuatiliwaji zaidi kwenye mitandao ya kijamii. Kwa asili, shirika hili la habari lilijikita zaidi kwenye maeneo ambayo Urusi ilitajwa kwenye mdahalo huo, ingawa hakuna kilichoandikwa wakati mazungumzo marefu yakifanyika kuhusu Urusi na Syria kupiga mabomu yhuko Aleppo, hali ambayo kwa mujibu wa maafisa wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Marekani, lazima uchunguzi wa uhalifu wa kivita ufanyike.
Kuhusu kusambazwa na ‘kupendwa’ kwa twiti hizo na wafuatiliaji wake, twiti iliongozwa ni ile ambayo Trump alidai kuwa Rais wa Syria Bashar al-Assad ana “msimamo na akili zaidi kuliko [Clinton] na Obama.”