‘Uganda ni Chungu Kinachotokota': Kukamatwa, Udanganyifu na Kufungwa kwa Mitandao ya Kijamii Vyatawala Uchaguzi

Ugandans take to the polls, February 2016. Photo by Flickr user Commonwealth Secretariat. CC BY-NC 2.0

Waganda wakiwa kwenye mistari tayari kwa kupiga kura, Februari 2016. Picha na mtumiaji wa Flickr sekretarieti ya Jumuia ya Madola. CC BY-NC 2.0

Tarehe 18 Februari, raia wa Uganda walipiga kura kumchagua Rais, wabunge na viongozi wa serikali za vijiji, uchaguzi uliogubikwa na machafuko, maandamano, kutiwa nguvuni pamoja na kuwepo kwa taarifa za uchakachuzi wa matokeo.

Raia wa Uganda na waangalizi wa kimataifa wamekuwa na maoni tofauti kuhusiana na uhalali wa upigaji kura, hata hivyo, asasi moja ya nchini Uganda, ‘Waangalizi wa Uchaguzi wa Uganda’, wamesema kuwa, zoezi zima la uchaguzi lilikuwa ni  batili.

Matokeo ya awali yanaonesha kuwa Rais aliyemaliza muda wake, Yoweri Museveni, ambaye anawania Urais kwa mara ya tano na anayekamilisha miaka 30 akiwa madarakani, anaongoza kwa takribani asilimia 62  ya kura.

Kizza Besigye, kiongozi mkuu wa upinzani anayewakilisha chama cha Forum For Democratic Change (FDC), alitiwa nguvuni yeye pamoja na maafisa wengine wa chama chake pale polisi walipovamia makao makuu ya chama chake , na kufyatua mabomu ya machozi pamoja na milipuko isiyo na madhara iliyokuwa na lengo la kuwatawanya watu. Waandishi wa habari waliokuwa wakipasha habari kutoka katika eneo la tukio nao walitiwa nguvuni. Kwa ujumla, kwa wiki hii pekee, Besigye amekamatwa mara tatu .

Siku ya Ijumaa, kulikuwa na maandamano nje ya makao makuu ya chama (cha FDCT) na pia kuripotiwa kuwepo kwa machafuko ya hapa na pale baina ya wafuasi wa vyama katika maeneo mbalimbali nchini Uganda yaliyochangiwa na kuchelewesha kutangazwa kwa matokeo.

Chaguzi za Urais za mwaka 2006 na 2011 pia ziligubikwa na machafuko pamoja na wananchi kuandamana.

Siku ya uchaguzi, Tume ya Mawasiliano ya Uganda ilizuia kutumiwa kwa mitandao ya kijamii kama Facebook, Twitter, na WhatsApp saa moja mara baada ya zoezi la uchaguzi kuanza, lengo la hatua hii likisemwa kuwa ni kwa minajili ya ulinzi wa Taifa. Huduma hizi bado zimesitishwa.

Baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii waliweza kukwepa kikwazo hiki kwa kutumia mfumo siri wa intaneti (VPNs), na pale walipopata namna ya kutumia mitandao ya kijamii, wengi walichapisha taarifa ya yale waliyokuwa wakiyashuhudia.

Mtumiaji mmoja wa Twitter alituma ujumbe mfupi uliokuwa umetumwa kwa watumiaji na kampuni moja ya simu kuhusiana na kusitishwa kwa huduma:

Mtumiaji mwingine, ‘PeacifulTransitionUg’, alichapisha picha iliyoonesha matairi yakichomwa jijini Kampala:

Kwa upande mwingine, mtumiaji wa Twitter, Lucy alichapisha picha iliyowaonesha wanajeshi wakiweka doria katika maeneo ambayo yalionekana yakiwa tulivu:

‘Uganda ni chungu kinachotokota!’

siku chache kabla ya uchaguzi, waandamanaji walio wafuasi wa Besigye na polisi walikabiliana vikali jijjini Kampala. Mtu mmoja aliuaw kwa risasi na pia polisi walitupa mabomu ya machozi moja baada ya jingine kwa ajili ya kutawanya watu waliokuwa wamekusanyika katika makundi.

Watumiaji wa mitanao ya kijamii walijadili namna walivyokasirishwa na hali ya mambo ilivyokuwa. Akiibua hoja ya nmna polisi na wanajeshi walivyokuw wakikabiliana wagombea wa upinzani pamoja na wafuasi wao, ‘Cane cutter’ aliandika:

Daniel Kawuma, mwanafamasia raia wa Uganda alitoa tahadhari:

Melissa Sibihwana alisali:

Mtumiaji wa Twitter'kmarkusk96′ alilalama:

Nimrod Taabu, mtangazaji wa televisheni, alisema:

Raia mwingine wa Uganda aliweka bayana kuwa:

‘Wewe ni nani unayeweka pingamizi?’

Akihoji kuhusu matumizi y mali ya umma kuhujumu raia, Ashaba Godfrey, ambaye nni mwanafunzi, alisema:

Kwenye mada hiyo hiyo, Stuart alihoji:

Davido, mwanabaolojia wa viwandani alitaka kufahamu kama kulikuwa na sababu yoyote ya kufanyika kwa uchaguzi:

Akirejelea jina la chama tawala, National Resistance Movement (NRM), Melissa Sibihwana alitanabaisha:

Matokeo ya jumla yanategemewa kutangazwa Jumamosi Februari 20.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.