
Picha ya angani ya makazi duni ya Kibera Nairobi, Kenya. Picha imeruhusiwa kutumika chini ya leseni ya Creative Commons na PSchreibkraft.
Kuna tovuti ya picha inayoitwa wanadamu wa New York (Humans of New York) ambayo imehamasisha kuweko kwa wanadamu wa Kibera ama (Humans of Kibera). Huu ni mradi wa Mtandao wa Habari wa Kibera (KNN), kikundi cha waandishi vijana wa habari kutoka Kibera, Nairobi, Kenya. Mradi huu unatuonyesha vyema maisha ya wakazi wa Kibera—makazi duni yaliyo kubwa zaidi Kenya—kwa mtandao wa Tumblr.
Hizi ni picha kadhaa zinazosimulia maisha ya Wanadamu wa Kibera:
Mnamo mwaka wa 2012 katika Mkutano wa Mkuu wa Global Voices Nairobi, Rising Voices ikishirikiana na Mfuko wa Kibera na Mtandao wa Habari wa Kibera iliwakutanisha waandishi wa Global Voices na wanajamii wa Kibera kujaribu kushiriki shughuli za uandishi wa kiraia katika eneo la Kibera.

Washiriki wa jamii ya Global Voices na Map Mathare