Habari kutoka Muhtasari wa Habari na Maandamano
Venezuela: Utata na Mashambulizi Wajadiliwa kwenye Mtandao wa Twita
Wakitumia alama ashiria #UcabCaracas na #SOSColectivosDelTerrorAtacanUCAB [SOS vikundi vya kigaidi vya mashambulizi UCAB], maoni na picha ya mashambulizi kwa wanafunzi kwenye maandamano ambayo inaonekana yalitokea katika Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Andrés Bello [es] mjini Caracas zimeonyeshwa sana. Miongoni mwa wale wanao twiti ndani ya chuo kikuu hicho, kilchosimamisha shughuli...
Naijeria: Kampeni ya #Bringourgirlsback
Katikati ya mwezi Aprili, zaidi ya wasichana 200 wa shule walitekwa nyara kutoka shule ya sekondari iliyoko eneo la Chibok, Naijeria, kitendo kinachodaiwa kufanywa na Boko Haram, kundi la kigaidi lililoko katika eneo la kaskazini mwa nchi hiyo. Ingawa baadhi ya wasichana 57 wameweza kutoroka, bado wengine wengi wako...
Hedhi Sio Siri ya Aibu. Tuzungumzie Siku Zetu kwa Uwazi
“Kwa nini wanawake hawapendi kuzungumzia hedhi?” anauliza Sourav Kumar Panda kwenye tovuti ya Youth Ki Awaaz na anaendelea kujadili/a> kuwa kwenye siku hizi na zama za leo, kuendelea kuifanya hedhi kuwa suala la kuficha haina maana -wakati umefika kwetu kuvunja kimya na kuacha woga wa mila za jamii zetu kuhusiana...
Wito wa Kuacha Ujenzi Nchini Taiwan Ili Kuwalinda Chui
Chui wameorodheshwa kama wanyama wanaoishi kwenye mazingira magumu [zh] nchini Taiwan. Kwa kuwa chui wakubwa huishi misituni na mwituni katika maeneo tambarare na yale yenye milima na makazi yao ni aina tofauti sana. Makazi yao nchini Taiwan yanasumbuliwa kwa sababu ya miradi mipya ya ujenzi. Kamati ya tathmini ya mazingira...
PICHA: Maandamano mjini Caracas, Aprili 1
Tovuti ya PRODAVINCI inachapisha picha nne za Andrés Kerese zilizopigwa wakati wa maandamano yaliyotokea Chacao, moja ya mitaa ya wilaya ya Caracas, Jumanne, Aprili 1, 2014.
Amnesty International: ‘Mfululizo wa Ghasia ni Tishio la Utawala wa Sheria Nchini Venezuela’
Shirika la kutetea haki za binadamu, Amnesty International limetoa taarifa inayo weka kumbukumbu sawa “kuhusu madai ya uvunjifu wa haki za bindamu na unyanyasaji uliofanywa katika mukhtadha wa maadamano makubwa ya umma tangu mwezi Februari.” “Nchi hiyo iko kwenye hatari ya kuwa na mfululizo wa matukio ya ghasia kama hatua...
Ufisadi Nchini Nepal: Umeanza Kuwa Tabia Inayokubalika Kijamii?
Watu wana hasira na wamechoka, na mashirika ya habari mara nyingi huchapisha habari kuhusu uhusiano kati ya viongozi wa kisiasa na wezi wa mali za umma lakini hakuna anayezungumzia kuingia mtaani kuandamana kupinga ufisadi -hali isiyotarajiwa kwenye nchi ambayo watu hugomea kila kisichokwenda sawa Siromani Dhungana anaandika uchambuzi kwenye blogu...
Machafuko Nchini Burundi kabla ya Uchaguzi wa Rais
Angalau kumekuwa na makala 19 ya matukio ya vurugu tangu mwanzo wa 2014 nchini Burundi kabla ya uchaguzi wa rais vituo vya machafuko juu ya marekebisho ya katiba iliyopendekezwa na rais Nkurunziza ambayo inaweza kumruhusu kugombea kwa awamu ya tatu. CNDD-FDD chama tawala na tawi lake la vijana ni watuhumiwa...
Video: Usambazaji Vyakula katika Kambi ya Yarmouk-Syria
Shirika la habari la FAJER liliweka mtandaoni video ya kambi ya wakimbizi ya Yarmouk mjini Damascus wakati wa kupokea mgawo wa chakula cha kuwalisha wakazi 18,000 wa kambi waliobaki, ambao wamelazimishwa kula wanyama waliopotea ili kuokoa maisha yao wakati huu ambapo kuna uhaba mkubwa wa chakula. Video ni ya tarehe...
Kwa nini Maandamano Hayatasababisha ‘Mapinduzi ya Cambodia’
Faine Greenwood anaandika kuhusu mhadhara wa Stanford uliotolewa na mwanaharakati wa haki za binadamu wa Cambodia Ou Virak. Aliuliza kuhusu maandamano ya kupinga serikali yanayoendelea nchini Cambodia, Ou Virak alieleza kwa nini hayatasababisha ‘mapinduzi ya kisiasa': Sidhani kuwa mapinduzi ya Cambondia yatatokea, na wala sidhani yanahitajika…Hatuna hata neno muafaka kwa...