Habari kutoka na

Ramani Hizi Zaonesha Mahali Walipotesewa na Kuuawa Wanahabari wa Kambodia

  2 Juni 2015

Kituo cha Haki za Binadamu cha kambodia kimezindua jarida linaloelezea ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa kwa waandishi wa habari nchini Kambodia. Katiba ya nchini Kambodia inatoa uhuru wa kupashana habari lakini wanahabari wanazidi kunyanyaswa na kuuawa, hususani kwa waandishi wanaopasha habari kuhusiana na ukiukwaji wa maadili unaofanywa na maafisa...

Wanawake wa Kichina Waandamana Kupinga Kombe la Dunia

  13 Julai 2014

Offbeat China alieleza kwa nini wanawake hao wana hasira na jinsi Kombe la Dunia linavyoharibu mahusiano ya kifamilia nchini China. Wanapinga mambo mawili makubwa: 1) wapenzi wao kupuuza majukumu yao ya kifamilia kwa sababu ya kuangalia mpira usiku wa manane; 2) tabia za kucheza kamari kwa mashindano hayo.

Maandamano Makubwa Yafanyika huko Guangzhou, China

  12 Juni 2014

Mamia ya wakazi wa Guangzhou jana mchana walikusanyika huko Sanyuanli kupinga hatua ya polisi ya kutaifisha mali binafsi za watu kwenye bohari kama sehemu ya harakati za kukabiliana na majanga ya moto. Waandamanaji walijikuta wakikabiliana vikali na polisi, na baadae, wakati wa vurugu hizo, waandamanaji walifikia hatua ya kupindua magari...

Madai ya Ukiukaji wa Haki za Binadamu Wakati wa Mgomo wa Kilimo Nchini Colombia

  9 Mei 2014

Tovuti ya ‘kongamano la watu’ imeshutumu hadharani [es] uvunjifu wa haki za binadamu unayoendelea katika mgomo wa kilimo [es] nchini Colombia. Wanaripoti madai ya ukiukaji wa haki za binadamu katika mikoa mbalimbali: Catatumbo na Cucuta, San Pablo-Bolívar, Sogamoso – Boyaca, Kaskazini Santander-Hacarí, Yopal-Casanare, Boyaca, Berlin – Santander, Pinchote – Santander...

Caribbean Yajiunga na Kampeni ya #BringBackOurGirls

  7 Mei 2014

Kama watoto wetu wangetoweka tungelipenda dunia yote kusimama na kuja kutusaidia kuwatafuta wao. Sisi … tunauliza kwamba … kwa nini mara nyingi miili ya wanawake huwa uwanja wa vita ambapo vita hupiganiwa. Hili si tatizo ambalo linahusisha mji mdogo nchini Nigeria, ni tatizo la wasichana wote kila mahali. Tillah Willah...