Serikali ya Angola Yafungia Kituo cha Runinga cha Kibrazili kwa Madai ya ‘Kukiuka Taratibu’

Picha iliyopigwa kutoka kwenye video ya Kituo cha Runinga cha Serikali ya Angola/YouTube

Mapema tarehe 19 Aprili, serikali ya Angola ilisimamisha matangazo ya Record TV África, kituo cha kibrazili cha Runinga kinachomilikiwa na kampuni ya Grupo Record, kwa kile kinachoaminika kuwa ni ukiukwaji wa taratibu.

Taarifa rasmi iliyotolewa na Wizara ya Mawasilino, Teknolojia ya Habari na Media ya Angola (MINTTICS)ilieleza kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Record TV África hakuwa mzawa wa Angola. Wizara iliongeza kuwa, wanahabari wa kigeni katika kituo hicho cha runinga hawakuwa na vibali rasmi vya kufanya kazi nchini Angola.

Kwa mujibu wa taarifa ya wizara, shughuli za kituo hiki zilisitishwa rasmi tarehe 21 Aprili, hadi hapo taarifa nyingine itakapotolewa.

Tarehe 30 Aprili, Record TV África ilieleza kuwa ingemadilisha Mkurugenzi Mtendaji, ndugu Fernando Teixeira, ambaye ni raia wa Brazili na kumuweka ndugu Simeão Mundula, ambaye ni raia wa Angola. Kituo hiki cha Runinga kiliweka bayana pia kuwa, hakikuwa kimewaajiri waandishi wa habari ambao hawakuwa raia wa Angola.

Wakati kituo kiki kinasimamishwa, Record ilikiambia kituo kimoja cha utangazaji cha kibrazili kuwa kilishangazwa na maamuzi haya. Kilisema:

Em 19/04/2021, a Record TV Africa foi surpreendida com um comunicado da Direção Nacional de Informação e Comunicação do Ministério das Telecomunicações, Tecnologias de Informação e Comunicação Social (“MINTTICS”).

A Record TV Africa exerce a sua atividade em Angola desde 2005 e conta com atualmente 73 colaboradores diretos e indiretos.
A Record TV Africa, no estrito respeito da Constituição e da lei Angolana, informa o público, parceiros comerciais e, em particular, as suas centenas de milhares de telespectadores diários.
A Record TV Africa, pauta e sempre pautou pela legalidade nos mais de 15 anos presentes em Angola e em todo continente Africano, e irá juntos aos órgãos de tutela buscar o esclarecimentos referente as supostas irregularidades alegadas.

tarehe 19 Aprili, Record TV Africa kilishangazwa na taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mawasilino, Teknolojia ya Habari na Media ya Angola (MINTTICS).

Record TV África imekuwepo Angola tangu mwaka 2005 na hadi sasa inafanya kazi na watu 73 wa kudumu na wasio wa kudumu.

Record TV África, inawahabarisha raia, washiriki wake na kwa upekee mamia ya maelfu ya watazamaji wake kwa kuzingatia matakwa ya katiba na sheria za nchini Angola

Kwa kipindi cha miaka 15 ambacho Record TV África imekuwa ikifanya kazi nchini Angola na katika maeneo mengine barani Afrika, imekuwa ikizingatia matakwa ya kisheria ya nchi husika na itaendelea kushirikiana na mamlaka husika za serikali ili kupata ufafanuzi wa tuhuma zinazotukabili.

Uamuzi wa serikali unakuja wakati ambako kumezuka hali ya kuhojiwa kwa kanisa la Universal Church of the Kingdom of God), ambalo ndio mmiliki wa kitu cha runinga cha Kibrazili cha Grupo Record, kinachofanya kazi zake katika maeneo mbalimbali ya Afrika ikwemo Angola.

Tangu 2017, makasisi wazawa wa Angola wamekuwa wakiwatuhumu wasimamizi wa Kanisa la Universal Church wenye asili ya Brazili kwa makosa ya rushwa, uonevu na ubaguzi wa rangi . Mapema mwezi Agusti, 2020, waendesha mashtaka wa nchini Angola waliyashikilia majengo saba yanayomilikiwa na kanisa hili kama sehemu ya uchunguzi wa makosa ya jinai yanayolikabili kanisa hili. Baadhi ya makasisi nchini Angola wanatazamia kuwa na mwanzo mpya wa kanisa la Universal Church la nchini Angola.


Makala haya yanatokana na tafsiri ya makala ambayo kwa mara ya kwanza ilichapishwa kwa kireno tarehe 22 Aprili, 2021, na kisha kuboreshwa zaidi baada ya kuchapishwa na hivyo kuifanya kuwa na utofauti na chapisho la kwanza.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.