Maandamano Nchini Angola Yakitaka Haki Itendeke Kwa Silvio Dala, Daktari Aliyefariki Akiwa Mikononi Mwa Polisi

Maandamano dhidi ya kifo cha daktari Silvio Dala huko Luanda. Picha na Simão Hossi, CC-BY 3.0

Mamia ya Waangola waliingia mitaani kuandamana hapo Septemba 12 huko Luanda, Benguela na miji mingine 15 wakipinga ukatili wa polisi. 

Maandamano hayo yalianza baada ya habari za kushtusha kutolewa kuhusu kifo cha daktari Silvio Dala, mwenye miaka 35, aliyepoteza maisha Septemba 1 akiwa chini ya uangalizi wa polisi. 

Kulingana na taarifa za mamlaka, Dala aliondoka kwa gari yake kutoka hospitali ya  Watoto ya David Bernardino huko Luanda, ambapo ndiko hufanya kazi kama Mkurugenzi wa kliniki na alisimamishwa na polisi kwa sababu hakuvaa barakoa. 

Daktari huyo alipelekwa katika kituo cha polisi cha Catotes katika mji jirani wa Rocha Pinto, na “alipoonesha dalili za kuishiwa nguvu na kuanza kuzimia, alianguka vibaya na kugonga kichwa na kusababisha jeraha dogo kichwani mwake” ilisema taarifa rasmi ya polisi. Pia ilisema kwamba Dala alifariki wakati maofisa wa polisi wakimpeleka hospitali.

Chama cha Madaktari kiliipinga taarifa hiyo. Raisi wa chama hicho Adriano Manuel, aliiambia  Sauti ya Amerika (VOA) kwamba kuna utata katika maelezo ya mamlaka ambapo inaonesha kwamba daktari alisulubiwa. 

Manuel aliiambia  Sauti ya Ujerumani (DW) kwamba ” chanzo cha kifo kilichoelezwa na polisi sio halisi. Mtu yeyote ambaye ni daktari na amesomea udaktari atajua kuwa hiki sicho kilichomuua Silvio”. Kulingana na DW, chanzo cha habari kutoka wizara ya mambo ya ndani kinasema kuwa uchunguzi ulifanyika mbele ya familia na mwendesha mashtaka na ikathibitika kwamba daktari hakuwa mhanga wa kipigo. 

Chama kimesema kuwa kitalichukulia jeshi la polisi hatua za kisheria. Wakati huo huo serikali ya Angola imeunda tume itakayoshirikiana na Wizara ya Afya kufanya uchunguzi wa tukio hilo. 

Waandanaji hawaiamini taarifa ya polisi kuhusu kifo cha Dala. Mabango yaliyotumiwa na waandamanaji katika maeneo mbalimbali ya mji wa Luanda yalisema: “Kusiwepo tena Mauaji,” “Mnalipwa kutulinda, hamlipwi kutuua,” “Mimi ni Silvio Dala,” “Wamemuua Silvio Dala.” Pia kuna waliomtaka waziri wa Mambo ya Ndani Eugénio Laborinho ajiuzulu.

Maandamano yaliaandaliwa na Chama cha Madaktari wakishirikiana na mashirika na Taasisi za kiraia. 

Maandamano dhidi ya kifo cha daktari Silvio Dala huko Luanda. Picha na Simão Hossi, CC-BY 3.0

Maandamano dhidi ya kifo cha daktari Silvio Dala hiko  Luanda. Picha na  Simão Hossi, CC-BY 3.0

Tangu kuanza kwa janga la korona nchini Angola, vimeripotiwa visa kadhaa vya polisi kutumia nguvu kubwa wakati wakifanya ukaguzi  na wakati mwingine husababisha vifo vya raia. 

Akiongea na  Lusa, mwanamuziki wa kufokafoka  “Brigadeiro 10 Pacotes”, ambaye jina lake halisi ni  Bruno Santos, alimtaka Lugarinho ajiuzulu na pia akiitaka shule ya polisi iboreshe muundo wake wa mafunzo. 

“Jeshi la polisi ni taasisi ambayo inapaswa kuwapa wananchi ujasiri, lakini leo wananchi wanakosa ujasiri, yaani wanaogopa wanapokutana na polisi,” alimalizia kusema.

Maandamano dhidi ya kifo cha daktari Silvio Dala huko  Luanda. Picha na  Simão Hossi, CC-BY 3.0

Wengi waliyahamishia maandamano haya katika kurasa za Facebook na WhatsApp kupinga tukio hilo. Mwanaharakati na mwanazuoni  Nuno Álvaro Dala aliandika huko  Facebook:

A POLÍCIA NACIONAL É A RESPONSÁVEL PELA MORTE DO MÉDICO SÍLVIO DALA

As imagens são fortes e muito esclarecedoras. Temos todos de exigir que a justiça seja feita. A Polícia Nacional tem de pagar pelo crime que cometeu. Isto não deve ficar assim.

POLISI WA NCHI HII WANAHUSIKA NA KIFO CHA DAKTARI SILVIO DALA

Picha zina nguvu sana na ziko sawia. Lazima wote tudai haki itendeke. Polisi wa nchi hii lazima walipe kwa uhalifu waliotenda. Mambo hayawezi kuendelea kuwa hivi.

Huko Twitter, Isabel dos Santos, mwenyekiti wa zamani wa bodi ya wakurugenzi wa kamapuni ya mafuta ya Sonangol, binti wa rais wa zamani José Eduardo dos Santos, alisema:

#MimiNiSilvioDala. Siku ya Jumamosi Chama cha Madaktari wa Angola (SINMEA) kilitangaza “mgomo wa kimya na wa amani” wakiwataka wafanyakazi wa afya, vyama vingine na taasisi za kiraia kupinga ukatili wa polisi ikiwa ni ishara ya kumkumbuka daktari Silvio Dala, mnamo saa 6:30 mchana huko  Largo da Mutamba

Kichwa cha habari: waAngola waingia mitaani wakipinga ukatili wa polisi na wakitaka mauaji yakomeshwe. 

Wakati huo huo,  pia  huko Tweeter Alejandro alihoji ushiriki wa wahamasishaji wa mitandaoni nchini Angola katika tukio hili:

Wakati  George Floyd alipouawa hao wanaojiita “wahamasishaji wa ki-Angola” mitandaoni walionesha kuunga mkono mchakato wa Maisha ya Weusi Yana Thamani, lakini katika kifo cha daktari wa ki-Angola Silvio Dala, hawa ndugu hawafanyi chochote kuhusu janga hili!

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.