Salamu ya Siku ya Wajinga Kutoka Ubalozi wa Urusi

Picha. Chanzo: YouTube.

Tarehe 1 Aprili, siku ya wajinga duniani “ni siku ya kucheka” kwa utamaduni wa jamii ya watu wa Urusi— Wizara ya Mambo ya nje ya Urusi(MFA) imetumia vyema siku hii kwa kutayarisha kichekesho cha namna Urusi inavyohusiana kisiasa na mataifa ya nje, na kwa sasa ikitumia tukio lililoifanya Urusi kufuatiliwa sana mwaka 2016 baadaa ya kuingilia mchakato wa uchaguzi Mkuu wa Marekani.

Asubuhi ya leo katika ukurasa wa Facebook wa Ubalozi wa Urusi, Wizara ya mambo ya Nje ilipakia video ya mzaha katika mfumo wa sauti yenye kichwa cha habari, “Wizara ya mambo ya Nje ya Urusi imeandaa maelezo ya sauti yanayoweka bayana mipango yote ya mahusiano ya Kimataifa.”

Добрый день! Вы позвонили в посольстве России. Если Вы хотите заказать звонок российского дипломата Вашем политическим конкурентам, нажмите 1. Чтобы воспользоваться услугами русских хакеров, нажмите 2. По вопросам вмешательства в выборы, нажмите 3 и ждите начала избирательной кампании. В целях повышения качества услуг все разговоры записываются.

“Uwe na siku nzuri! Huu ni Ubalozi wa Urusi. Simu yako ni ya muhimu sana kwetu. Ili kuwasiliana na mpinzani wako wa kisiasa kutokea Ubalozi wa Urusi, bonyeza 1. Kuwatumia wataalam wa udukuzi wa Kirusi, bonyeza 2. Ili kuvamia chaguzi, bonyeza 3 na kisha subiri hadi wakati wa kampeni. Tafadhali, ni vizuri ukafahamu kuwa simu zote zinakaguliwa kwa ajili ya ubora wa uendeshaji na utoaji mafunzo.”

Usikilize mzaha huu hapa (Ujumbe wa sauti kwa lugha ya Kiingereza unaanza sekunde ya 0:29):

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.