Habari kutoka Muhtasari wa Habari na Trinidad na Tobago
Barbados, Trinidad & Tobago:Plastiki na Uchafuzi wa Mazingira
“Fanya matembezi kwenye pwani yoyote nchini Barbados – na utaona uchafu wa plastiki uliosukumwa ufukweni”: Barbados Free Press anauliza kama uuzaji wa chupa za plastiki za maji uwekewe vikwazo, wakati Mtrinidadi Keith Francis pia anaguswa na suala la uchafuzi wa mazingira kwa plastiki ulimwenguni.
Trinidad & Tobago: Kampeni ya 350
“Trinidad na Tobago ni kisiwa tajiri na nchi inayoendelea tajiri kwa mafuta na gesi asilia. Lakini pia tunashuhudia madhara mabaya ya maendeleo ya haraka kwenye nyanja za viwanda katika visiwa vyetu. Hii ni fursa ya sauti za wanawake kusikika”: Attillah Springer anajihusisha na kampeni ya hali ya hewa 350.
Trinidad & Tobago: Mtrini Mpaka Kwenye Mifupa?
“Kila siku ambayo ninapitia habari ninazidi kushawishika kuwa ninataka kuachana na klabu ya ‘Mimi ni Mtrini’ na kwenda sehemu nyingine”: Coffeewallah ameshachoka na kila kitu kuanzia uhalifu mpaka kodi.