Habari Kuu kuhusu Guadeloupe
Habari kuhusu Guadeloupe
Karibea: Tuzo za Fasihi ya Kifaransa
Wiki hii, waandishi wawili wenye asili ya Kiafrika wanaoandika kwa Kifaransa walipewa tuzo mbili zenye kuheshimika sana katika fasihi ya Kifaransa: Ulimwengu wa blogu za wanaozungumza Kifaransa katika Karibea umekuwa ukinguruma juu ya kutosheka kwao mara mbili kwa mpigo, katika makala hii kutoka Haiti, na hii kutoka Guadeloupe na hii...
Martinique: Uhuru na “Ubeberu” wa Kifaransa
Wakati harakati za wafanyakazi zinaendelea huko Martinique na Guadeloupe, wanablogu wa Martinique wanapima uhuru wa Idara za Ng'ambo utamaanisha nini. Le blog de [moi] anaona dhana ya kuwa Martinique haiwezi kujitegemea ni dhana inayotusi na ya kibeberu. Wasomaji wake wanadhani kuwa ukweli wa kisiwa chochote kidogo ni kuwa kila siku kitakuwa katika kivuli cha wengine.
Karibeani Ya Kifaransa: Tamasha la Kanivali 2009 Lazinduliwa
Kanavali ni utamaduni, sehemu ya uhai wa kila Muhindi wa Magharibi bila kuwaacha wale wa Karibeani ya Kifaransa. Ufuatao ni muhtasari wa blogu kutoka Martiniki, Guyana ya Kifaransa, Haiti na Guadalupe, ambao unaelezea mambo yanavyokuwa kwenye Kanivali.