Habari kutoka Muhtasari wa Habari na Vyombo na Uandishi wa Habari
Baada ya Maandamano Burkina Faso na Burundi, Naija na Togo Zinafuata?
Wanaija 20,000 wameingia mitaani mjini Niamey, Naija mnamo Juni, 6. Kuna ababu nyingi za maandamano hayo: umaskini uliokithiri, utawala mbovu na kubanwa kwa uhuru wa kujieleza yakiwa ni moja wapo ya malalamiko ya asasi za kiraia nchini humo. Maandamano kama haya yalitokea katika nchi za Burkina Faso, Burundi na Togo....
Ramani Hizi Zaonesha Mahali Walipotesewa na Kuuawa Wanahabari wa Kambodia
Kituo cha Haki za Binadamu cha kambodia kimezindua jarida linaloelezea ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa kwa waandishi wa habari nchini Kambodia. Katiba ya nchini Kambodia inatoa uhuru wa kupashana habari lakini wanahabari wanazidi kunyanyaswa na kuuawa, hususani kwa waandishi wanaopasha habari kuhusiana na ukiukwaji wa maadili unaofanywa na maafisa...
Je, Blogu Zinaelekea Kutoweka?
Makala haya ni sehemu ya 46 ya #LunesDeBlogsGV (#JumatatuYaBloguGlobalVoices) siku ya Machi 23, 2015. Kwenye #LunesDeBlogsGV (#JumatatuyaBloguGlobalVoices), tunajitahidi kuzitunza blogu mithili ya “viumbe wanaoelekea kutoweka”, kwa kushughulikia changamto zinazokabili uwepo wa blogu kwenye ulimwengu wa kidijitali. Jitihada kama hizi zinamfanya mwanablogu Iván Lasso kuchambua mustakabali wa kublogu na matatizo yanayowakabili wanablogu leo,...
Uhuru wa Vyombo vya Habari nchini Liberia Wawekwa Shakani Kufuatia Vita Dhidi ya Ebola
Umoja wa wanahabari wa Liberia wasikitishwa na hali ya kukosekana kwa uhuru wa upashanaji habari kufuatia hatua ya serikali ya kuzuia kuenea kwa virusi vya ebola. Umoja huu ulimwandikia barua Waziri wa sheria kumtaka kutafakari upya madhila wanayokabiliana nayo waandishi wa vyombo vya habari. Ufuatao ni muhtasari wa barua yenyewe:...
Jinsi Wanablogu Walifikia Gerezani kwa Kuandika Kuhusu Haki za Binadamu Nchini Ethiopia
Melody Sundberg anachambua uhuru wa kujieleza nchini Ethiopia baada ya wanablogu wa Ethiopia waliokamatwa kukaa siku 100 gerezani: Ethiopia ina idadi ya watu 94,000,000 na ni nchi ya pili yenye wakazi wengi katika bara la Afrika. Hata hivyo, hailingani na mahojiano ya Endalkhachew Chala kupitia Global Voices, kuwa na gazeti...
Majadiliano na Picha za Mkutano wa Highway Africa 2014
Mkutano wa Highway Africa 2014 ulifanyika kuanzia tarehe 7-8 Septemba, 2014 kwenye Chuo Kikuu cha Rhodes, Grahamstown, Afrika Kusini. Maudhui ya mkutano huo yalikuwa Mitandao ya Kijamii -kutoka pembezoni kwenda kwenda kwenye vyombo vikuu vy habari. Angalia picha na mzungumzo kuhusiana na mkutano huo hapa.
Highway Africa 2014 Yasogeza Mbele Tarehe ya Mwisho ya Kujiandikisha
Tarehe ya mwisho ya kujiandikisha kwa ajili ya Mkutano wa 18 wa mwaka wa Highway Africaimesogezwa mbele mpaka Ijumaa, Agosti 08 2014: Kutokana na kuongezeka kwa shauku ya watu kuhudhuria mkutano wa mwaka wa 18 wa Highway Africa, tarehe ya mwisho ya kujiandikisha imesogezwa mbele mpaka Ijumaa, 08 Agosti 2014....
Kuongozeka kwa Vitendo vya Kujichukulia Sheria Mkononi Nchini Senegali
Sada Tangara, mpiga kura na mwanablogu anayeishi Dakar, nchini Senegali aliweka picha-habari inayohusu kuongezeka kwa matukio ya kujichukulia sheria mkononi kwenye mitaa ya Dakar, mji mkuu wa Senegali. Anaeleza mwanzo wa mradi wake na kwa nini aina hii maarufu ya haki imeshika kasi jijini Dakar [fr] : Il faut savoir...
Umuhimu wa Haki kwa Wanablogu wa Ethiopia
Justice Matters ni blogu inayoripoti kuhusu kesi ya wanablogu wa Zone9 waliokamatwa na waandishi wa habari nchini Ethiopia kwa ajili ya kutoa maoni yao: Blogu hii ina habari zaidi za hivi karibuni kuhusu jitihada za utetezi, ripoti za vyombo vya habari, na hadhi ya kisheria ya wanablogu wa Zone9 nchini...
Tovuti 50 Zilizotembelewa Zaidi Nchini Kenya
Je, unajua ni tovuti gani maarufu zinazotembelewa zaidi nchini Kenya? Soka posti ya James Wamathai kwenye blogu yake kufahamu zaidi: Mengi yamebadilika tangu mwezi Januari, wakati nilipotoa orodha ya tovuti maarufu zaidi nchini Kenya. Tovti ya Budget airline Jambo Jet ilizinduliwa, gazeti linalomilikiwa na kampuni ya NMG liitwalo Nairobi News...