Sada Tangara, mpiga kura na mwanablogu anayeishi Dakar, nchini Senegali aliweka picha-habari inayohusu kuongezeka kwa matukio ya kujichukulia sheria mkononi kwenye mitaa ya Dakar, mji mkuu wa Senegali. Anaeleza mwanzo wa mradi wake na kwa nini aina hii maarufu ya haki imeshika kasi jijini Dakar [fr] :
Il faut savoir qu’à Dakar, quand un délinquant se fait attraper par une foule alors qu’il vient de commettre un crime ou un délit, il est systématiquement tabassé, grièvement blessé et meurt parfois des suites de ces coups. J’ai donc voulu comprendre ce cycle de violence et montrer la vengeance disproportionnée que subissent parfois les délinquants en retour de leurs actes [..] Pour les Dakarois, cette justice populaire est un moyen d’effrayer les agresseurs et d’essayer de les dissuader de revenir dans leur quartier.
Jijini Dakar, wakati kundi la watu wenye hasira linafanikiwa kumkamata kibaka ambaye ametoka kufanya uhalifu, mtu huyo hupingwa kwa mfululizo, na wakati mwingine hujeruhiwa sana na hata kufa. Nilitaka kuelewa mduara huu wa matumizi ya nguvu na kuonyesha namna matumizi haya ya nguvu kupita kiasi yanavyowaathiri vibaka shauri tu ya matendo yao yasiyokubalika […] kwa watu wa Dakar, na jinsi ambavyo adhabu za namna hii zinavyochukuliwa kuwa namna ya kuwaogofya waendelezaji wa vitendo hivi na kuwafanya wasirudi majumbani kwao.