Habari kutoka Muhtasari wa Habari na Mahusiano ya Kimataifa
Video Inayoonyesha jinsi Marekani Iliangusha Mabomu ya Tani Milioni 2.5 Nchini Laos
Mother Jones alipakia video ambayo inaiga utupaji mabomu 600 uliofanywa na Marekani nchini Laos kati ya mwaka wa 1965 hadi 1973 wakati wa zama za Vita ya Vietnam.
Kwa nini Rwanda Inaituhumu Ufaransa Kusaidia Mauaji ya Kimbari ya 1994
Wakati Rwanda ikiwakumbuka waathirika wa mauaji ya kimbari yalitokea miaka 20 iliyopita, Rais Kagame anasema tena kuwa Ufaransa lazima “ikabiliane na ukweli mgumu” wa kukiri kushiriki kwenye mauaji hayo ya mwaka 1994 [fr]. Kama matokeo ya matamshi hayo, serikali ya Ufaransa imesusia matukio yote ya kukumbuka mauaji hayo na waziri...
Jiunge na IGF Japan Kujadili Utawala wa Mtandao
IGF Japan, hatua ya maendeleo nchini Japani ya Jukwaa la Utawala Mtandao, ambapo watu wanaojihusisha mtandaoni huja pamoja kujadili changamoto za utawala wa mtandao, ulifanyika Machi 14, 2014
Kurudisha Mabaki ya Miili ya Binadamu tu Haitoshi, Ombeni Radhi, Namibia Yaiambia Ujerumani
Mabaki ya watu waliouawa wakati wa vita vya kikoloni (kwenye karne ya 20) yalirudishwa Namibia na Ujerumani mwezi Machi. Hata hivyo, Wanamibia bado wanadai tamko rasmi ya kuomba radhi kutoka kwa serikali ya Ujerumani kama Tendai Marima, mwanazuoni mtafiti wa fasihi za Afrika , aliandika kwenye tovuti ya Think Africa Press:...
Korea Kaskazini: Ni Lini Itaanguka?
Ingawa Korea Kusini inaonekana kutengeneza mahusiano na Korea ya Kaskazini, wataalamu wana wasiwasi kidogo kuhusu kubashiri kuanguka kwa Korea Kaskazini. NKnews.org ilichapisha posti nzuri kuhusu uwezekano wa kutawanyika kwa utawala wa kidikteta, akihitimisha kuwa ‘mageuzi ya kiuchumi ya Pyongyang yanaongeza uwezekano wa tukio la kuanguka vibaya’.
Matukio ya Ghasia Zinazofanywa na Majeshi ya Urusi nchini Ukraine
Blogu maarufu ya “Tafsiri za Maida ilichapisha bandiko la mtandao wa Facebook la Dmitry Tymchuk, Mkuu wa Kituo cha Ukraine cha Stadi za Siasa za Kijeshi, linaloeleza matukio ya ghasia za kimataifa zinazodaiwa kufanyika na “matendo yasiyo ya kawaida” tangu Februari 2014. Tymchuk anaanza uchambuzi huu kwa kusema: Kwa mfano,...
Mkutano wa Wanawake wa Nchi Zizungumzao Kifaransa 2014 Wafunguliwa Kinshasa, DRC
Mkutano wa wanawake wa nchi zizuingumzao Kifaransa 2014 [fr] Unafunguliwa leo jijini Kinshasa, DRC. Huu ni mkutano wa pili kufuatia ule uliofanyika Paris mwaka 2013. Wakati ule wa kwanza ulijikita katika kupunguza vitendo vya kudhalilisha wanawake katika maeneo yenye migogoro, lengo la mkutano huu wa 2014 litakuwa ni wajibu wa wanawake...
Caribian: Namna Vyombo vya Habari Vinavyoathiri Mitazamo
Venezuela na Haiti zimekuwa zikikabiliwa na maandamano ya kupinga serikali. Hata hivyo, ukuzaji wa mgogoro wa Venezuela unaofanywa na vyombo vya habari vya kimataifa na ukimya wake kwa mgogoro wa Haiti, unaibua maswali muhimu kuhusu kuyumba kwa Marekani katika kuimaisha tunu ya haki za binadamu na demokrasia. Kevin Edmonds anatoa...
Pakistan, Usiingilie Vita vya Ndani ya Syria
Siku moja baada ya dondoo ndogo ya habari yenye kichwa cha habari, “Saudi Arabia ‘inatafuta uungwaji mkono kwa waasi wa” ilipoonekana kwenye magazeti ya Pakistani, mwanablogu wa siasa Ahsan Butt aliposti tahadhari kali kwa watunga sera ya mambo ya Kimataifa wa nchi ya Pakstani kuachana na mambo ya ndani ya...
Picha Mpya ya Korea Kaskazini ya Shirika la Anga la Marekani
Wasomaji wa kimataifa wanaofuatilia masuala ya Korea Kaskazini labda wangekutana angalau mara moja na picha hii maarufu ya rasi ya Korea kutoka Shirika la Anga la Marekani (NASA) kuonesha tofauti kubwa ya taa zinazoangaza usiku kwenye nchi hizo mbili za Korea. NASA hatimaye walihuisha picha zao za Satelaiti na ‘ina mwonekano mzuri kuliko picha ya...