Kurudisha Mabaki ya Miili ya Binadamu tu Haitoshi, Ombeni Radhi, Namibia Yaiambia Ujerumani

Mabaki ya watu waliouawa wakati wa vita vya kikoloni (kwenye karne ya 20) yalirudishwa Namibia na Ujerumani mwezi Machi. Hata hivyo, Wanamibia bado wanadai tamko rasmi ya kuomba radhi kutoka kwa serikali ya Ujerumani kama  Tendai Marima,  mwanazuoni mtafiti wa fasihi za Afrika , aliandika kwenye tovuti ya Think Africa Press:

Mafuvu na mifupa yaliyorudishwa nyumbani mwezi huu yalichukuliwa na Ujerumani wakati Namibia -wakati huo ikiitwa ‘Ujerumani ya Kusini Magharibi ya Afrika’ -ikiwa ni moja la koloni lake. Namibia ilitawaliwa kwanza na mabeberu wa kizungu mwaka 1884, na 1904, watu wakabila la Waherero na Wanama − walionyang'anywa ardhi yao na mifugo -waliazimia kwa pamoja kupambana ili  kujaribu kuwafukuza Wajerumani.

Katika maasi hayo ya mwanzo, zaidi ya makabaila 100 wa Kijerumani na askari waliuawa, lakini juhudi za kupambana na mapinduzi hayo zilikuwa za kikatili na kinyama. Baada ya miaka mitatu ya kujaribu kuzima mapinduzi hayo, kadri ya watu wa kabila la Waherero na Wanama 10,000 waliuawa, hiyo ikiwa ni asilimia 80 na 50 ya makabila yao. Inasemekana kuwa hayo ndiyo yalikuwa mauaji ya kwanza ya kimbari katika karne ya 20.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.