Habari kuhusu Lugha
Twita Kutoka Beirut: Siku ya Pili ya Warsha ya Wanablogu wa Uarabuni
Siku ya pili ya Warsha ya Wanablogu wa Kiarabu ilianza na mada inayohusu Mtandao wa Herdict, tovuti inayotumia vyanzo vya watumiaji kukusanya taarifa za uchujaji wa habari kwenye intaneti kutoka kwa watumiaji duniani kote. Mshiriki wa warsha kutoka Qatar Muhammad Basheer alituma picha kutoka kwenye mada hiyo katika ujumbe wa...
Karibea: Tuzo za Fasihi ya Kifaransa
Wiki hii, waandishi wawili wenye asili ya Kiafrika wanaoandika kwa Kifaransa walipewa tuzo mbili zenye kuheshimika sana katika fasihi ya Kifaransa: Ulimwengu wa blogu za wanaozungumza Kifaransa katika Karibea umekuwa ukinguruma juu ya kutosheka kwao mara mbili kwa mpigo, katika makala hii kutoka Haiti, na hii kutoka Guadeloupe na hii...
Finland: Suala la Lugha
Nordic Voices anaandika kuhusu ‘suala la lugha” huko Finland.
Afrika Kusini: Wimbo wa Taifa kwa Wanaoongea Kiingereza
Wimbo wa Taifa wa Afrika Kusini kwa wanaoongea Kiingereza: Ni njia kuu iliyoje ya kufafanua kwa kuonyesha Wimbo wa taifa wa Afrika Kusini kwa wale kati yetu ambao kwanza hatuufahamu mpaka sasa, pili tunaoufahamu lakini pengine hatujui jinsi ya kutamka maneno yake na tatu ambao hatuongei lugha iliyo kwenye wimbo...
Dunia Nzima: Lugha 2,500 Zinapotea
Ramani shirikishi ya lugha zinazopotea, inayoonyesha lugha 2,500 kati ya 6,000 ambazo ziko hatarini, imezinduliwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO). Shirika hilo la kimataifa linawaomba watumiaji wachangie kwa kutuma maoni kwenye mradi huo ambao unawatia mashaka wanablogu wengi wenye nia ya kuhifadhi tamaduni.
Jamaika: Miziki Yenye Maneno Machafu Yazuiwa
Utata wa muda mrefu juu ya usahihi wa kurushwa hewani kwa miziki fulani umezuka tena nchini Jamaika. Wanablogu wa Jamaika wanapaza sauti zao.
Msumbiji: 2038?
Msumbiji itakuwaje katika miaka 30 ijayo? Mwana sosiolojia Carlos Serra [pt] anatoa mitizamamo tisa ya falme zilizokufa za Kirumi yaani (Byzantine) na anawakaribisha wasomaji wake kurekebisha mitizamo hivyo kwa kadri ya wanavyoona ni sawa: 1. Lugha ya kireno itakuwa ni mabaki, itazidiwa na lugha ya kiingereza, itakayokuwa ikitumika kiufasaha katika...