Uzbekistan: Mchezo wa Siasa katika Facebook

Facebook inaonekana kuanza kuchukua jukumu muhimu katika siasa za Uzbek. Hata hivyo , facebook ni imekuwa ni zaidi kwa ajili ya michezo na akaunti za kugushi kuliko chombo kuwa chombo cha harakati za kiraia.

Je habari hii ya kujiua ni ya kupandikizwa?

Mnamo tarehe 6 Disemba, 2011, Redio Free Europe/Redio Liberty ilitoa taarifa ya kujiua kwa msichana huko kwenye mji wa magharibi ya Uzbek uitwao Andijan. Baada ya kurudi nyumbani kutoka mapumzikoni, Gulsumoi Abdujalilova, mwenye umri wa miaka 32 mwanafunzi wa chuo kikuu nchini Ujerumani, inasemekana alihojiwa na polisi kwa muda wa siku nne.

Kwa mujibu wa Shirika Lisilo la Kiserikali la Haki za Binadamu (Uzbek NGO Human Rights Alliance), Abdujalilova alipigwa akiwa kituo cha polisi na kushinikizwa kuandika maelezo dhidi ya Muhammad Salih, kiongozi wa upinzani wa People's Movement of Uzbekistan (PMU) aliye ukimbizini. Harakati hizi zilianzishwa mnamo Mei 2011 na vikundi mbalimbali vilivyo nje ya Uzbek vyenye msimamo wa kuipinga serikali kwa lengo la kuhakikisha kuwa utawala wa Rais Islam Karimov unaangushwa.

Picha ya utambulisho wa Gulsumoy Abdujalilova katika ukuta wake wa Facebook, ambayo kiuhalisia ni picha ya mwanamitindo wa Uturuki Armine Eşarpları

Kwa Mujibu wa akaunti yake ya Facebook, AAbdujalilova alikuwa ni mfuasi wa harakati hizo, na mtu aliyejitambulisha kwa jina Muhammad Salih alikuwa mmoja kati ya rafiki zake wa kwenye Facebook.Wanahabari wa mtandaoni na watumiaji wengine wa wavuti wanaamini kuwa hiyo ndio sababu iliyofanya binti huyu kuanza kutupiwa macho na mamlaka za Uzbek. Hata hivyo, tovuti ya PMU imeeleza [uz] kwamba Abdujalilova hakuwahi kamwe kuwa mwanchama wa harakati hizo.

Ni vyema pia kueleza kuwa maafisa wa Wizara ya Mambo ya Ndani mjini Andijan hawajatoa maoni yoyote. Ndugu zake Abdujalilova (kwa mujibu wa maelezo yake ya utambulisho kwenye Facebook ameolewa, na Asasi ya Haki za Binadamu imemtaja dada yake Abdujalilova ambaye ndiye aliyeuona ujumbe wa kujiua ulioachwa na mdogo wake) nae pia amekaa kimya.

Habari hii ilizidi kuwa na utata siku mbili baadaye, mnamo tarehe 8 desemba, pale tovuti ya upinzani Uzmetronom.com ilipochapisha [ru] makala yenye matokeo ya uanahabari wa kipelelezi uliofanywa na tovuti hiyo. Mwandishi wa makala hiyo ambaye hakujifahamisha, alihitimisha kuwa habari hii yote ni uchochezi ulioandaliwa na Muhammad Salih ili kutikisa jamii ya Uzbek na kutafuta kujulikana kimataifa.

Habari hii imewavuta watumiaji wa wavuti. Mmoja wao ametoa maoni juu ya dhana kuwa inawezekana kuwa jambo hili limepandikizwa na upinzani wa kuichafua serikali ya Uzbek. Mwingine akasema kwamba hii imefanywa na kitengo cha usalama wa taifa ili kuwaonesha raia hatari za kushirikiana na wapinzani wa serikali.

Bado haijawa wazi nani atafaidika katokana na habari hii ya kutungwa na p ngine hilo halitajulikana kamwe. Sarah Kendzior wa Registan.net anakamilisha:

[…] inaweka wazi ni kwa kiasi gani uvumi unavyofanya kazi katika mtandaoni wa siasa wa Uzbek. Dhana ya kwamba taarifa zote si za kuaminika, na kuwa vyanzo vyote hupendelea upande fulani, imeweza kuwa na madhara ya makusudi ili kuhakikisha kwamba kila uvumi unachukuliwa maanani.

Akaunti ya uongo ya Waziri Mkuu katika Facebook

Mada nyingine ambayo imeleta utata mkubwa kati ya wanablogu wa Uzbek ni akaunti ya Facebook ya Waziri Mkuu wa Uzbekistan Shavkat Mirziyoyev. Akaunti hii ilianzishwa mapema mwezi Mei mwaka huu, ina takribani marafiki 2,000 na inamtambulisha yeye kama Muislamu kwa asilimia 100 mwenye mtazamo wa siasa za kihafidhina, aneyependelea wanawake na ameoa.

Catherine A. Fitzpatrick wa Eurasianet.org anasema:

[…] unaweza kuona kuwa Mirziyoyev ametiwa moyo na Nicolas Sarkozy, Lee Myung-bak, Barack Obama, Vladimir Putin and […] Islam Karimov.

Anuani yake ya barua pepe ya gmail imewekwa, kwa hiyo mwandikie na uulize swali lolote! Hata hivyo usitarajie picha za paka au mbwa.

Wengine wanajiuliza kwa nini Waziri Mkuu hana ukurasa katika mtandao ya kijamii nchini humo Muloqot.uz wanakisia kuwa lengo la ukurasa wake wa facebook ni kuvutia watu wa Magharibi

Hata hivyo, baada ya tamko lisilo rasmi kutoka kwenye ofisi ya Waziri Mkuu kuhusu kuwasiliana na uongozi Facebook wakiwa na ombi la kuufuta ukurasa huo, ndipo ilipojulikana wazi kuwa akaunti hiyo haikuwa halisi

Hatari ya kuwa hadharani sana

Hii sio mara ya kwanza kwa majina ya viongozi wa ngazi ya juu sana nchini Uzbek kutumika kwenye akaunti zenye utata kwenye mitandao ya kijamii. Mapema Mei wanablogu walizijadili akaunti mbili za twita ambazo zilihusishwa na binti wa Rais, Gulnara Karimova.Ya kwanza, @GuliKarimova, haipo tena kwa sasa. Hata hivyo, @GulnaraKarimova [ru], inafanya kazi na inawafuatiliaji zaidi ya 1,800

Kama tunavyoona , mitandao ya kijamii nchini Uzbekistan inatumika sana katika michezo yenye siasa ndani yake. Kwa sababu hiyo Hugh Raiser kutoka Eurasianet.org anaonya:

[…] hoja zinazohusu hatari za kujiweka hadharani sana na kuwa wazi juu ya mahusiano yako kwenye mitandao yakijamii bado ina nguvu.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.