Habari kutoka na

Filamu: ‘Sanaa ya Ama Ata Aidoo’

The Art of Ama Ata Aidoo ni filamu iliyotayarishwa na mtayarishaji wa filamu Yaba Badoe: The Art of Ama Ata Aidoo, inasaili mchango wa kisanii wa mmoja wa waandishi wanawake mashuhuri barani Afrika, anayeongoza kizazi hiki kwa kipaji kipya cha pekee. Dokumentari hii inasaili safari ya ubunifu ya Ama Ata...

Trinidad na Tobago: Washindi wa Tuzo za Hollick Arvon

  20 Machi 2014

Blogu ya Bocas Lit Fest imewatangaza waandishi chipukizi kutoka Jamaica, Grenada, St. Vincent na Trinidad na Tobago kuwa washindi wa Tuzo zinazovuta watu wengi za Waandishi wa nchi za Karibiani za Hollick Arvon kwa mwaka 2014, ambazo kwa mwaka huu zilifanyika kwa mara ya pili.

Uajemi: Washairi Wawili Watiwa Nguvuni

Washairi Mehdi Mousavi na Fatemeh Ekhtesari wametokomea nchini Uajemi. Kwa mujibu wa taarifa za habari, washairi hao wamewekwa kizuizini tangu mwanzoni wa mwezi Desemba. Zaidi ya watu mia mbili wametia saini hati ya malalamiko mtandaoni na kutoa wito kwa Umoja wa Mataifa kuchukua hatua kuhusiana na hali za wanaharakati wa...

Vijiwe Vya Usomaji Gazeti Mjini Mumbai Vyazorota

  8 Juni 2013

Vachanalays (vituo vya kusoma magazeti) ni jambo la kawaida katika vitongoji vingi mjini Bombay ambapo wenyeji husoma magazeti na kujadili habari zilizotokea siku husika. Sans Serif anaripoti jinsi vituo hivyo vinavyozidi kupitwa na wakati pole pole. Blogu hiyo pia inaonyesha picha nzuri inayojieleza ya mwanablogu wa picha M.S. Gopal juu ya maudhui hayo...

Peru: Kampeni ya Kuzuia Kufungwa kwa Maktaba ya Amazon

  11 Novemba 2010

Juan Arellano wa Globalizado [es] anaripoti juu ya kampeni ya kuzuia kufungwa kwa maktaba huko Iquitos, Peru , maktaba ambayo inatilia mkazo vitabu na masuala yanayohusu Amazon. Maktaba hiyo ni ya pili kwa umuhimu katika masuala ya Amazon huko Marekani ya Latini.

Karibea: Tuzo za Fasihi ya Kifaransa

Wiki hii, waandishi wawili wenye asili ya Kiafrika wanaoandika kwa Kifaransa walipewa tuzo mbili zenye kuheshimika sana katika fasihi ya Kifaransa: Ulimwengu wa blogu za wanaozungumza Kifaransa katika Karibea umekuwa ukinguruma juu ya kutosheka kwao mara mbili kwa mpigo, katika makala hii kutoka Haiti, na hii kutoka Guadeloupe na hii...