Habari kutoka Muhtasari wa Habari na Mwitikio wa Kihisani
Kimbunga Haiyan: Hadithi ya Ujasiri Kupitia Filamu Fupi
Kimbunga Haiyan, filamu fupi kwa hisani ya Janssen Powers, inaonyesha hali baada ya dhoruba ambayo mapema mwezi Novemba iliua zaidi ya watu 6,000 katika jimbo la Philippine la Leyte. “Kwa kawaida, mimi nia yangu ilikuwa kupata habari za uharibifu huo, “Powers aliandika katika maelezo ya kazi yake. “Nilicho pata hata...
Kuwasaidia Waathirika wa Tetemeko la Balochistan
Zaidi ya watu 300,000 wameathirika kufuatia tetemeko la hivi karibuni katika wilaya sita za Jimbo la Balochistan nchini Pakistan. Kashif Aziz wa mtandao wa Chowrangi anatoa habari za namna ya kutoa msaada kwa waathirika wa tetemeko la Balochistan.
Katika Jamhuri ya Afrika, ”Bado Tuna Matumaini ya Kuishi Pamoja kwa Amani”
Kama mapigano baina ya waasi wa Sékéla na jeshi la taifa la Jamhuri ya Afrika ya Kati vinaendelea, mvutano katika mji wa Bossangoa. Wenyeji wanahofia kwamba migogoro inaweza kumwagika katika mapigano ya wazi kati ya jumuiya ya kikristo na Waislamu. Baadhi bado kushikilia tumaini kwa upatanisho angalau, kama Iman wa msikiti wa mji wa...
Udhaifu wa Watawala wa Afrika unajionesha Mali?
Ousmane Gueye katika tovuti ya Mondoblog anaandika [fr] kuhusu kuchelewa kupeleka vikosi vya kijeshi kasikazini mwa Mali: Kama tungekuwa tunasaiili matokeo ya watu wenye amani na huru kuingilia kati hali ya mambo nchini Mali, basi ni wazi kuwa kwa kuchelewa kupeleka vikosi vya ulinzi, nchi za Afrika zimewakosea wananchi wa Mali...
Watu 60 Wauawa kwa Msongamano nchini Abidjan
Magogo ya miti yaliyokuwa yameanguka barabarani yanaonekana kusababisha msongamano mkubwa na ulioua watu 60 na kujeruhi wengine 49 wakati wa sherehe za kuukaribisha mwaka mpya mjini Abidjan, Côte d'Ivoire. Kutokana na ukweli kuwa eneo hilo halikuwa na mwanga wa kutosha inawezekana ndio sababu iliyochangia tukio hilo la msongamano ulisababisha mkanyagano...
Je, Una Swali Lolote kwa Jimmy Carter?
Rais wa zamani wa Marekani Jimmy Carter anapokea maswali kupitia mitandao ya kijamii ya Facebook na Twita (#CarterQA) kama sehemu ya kuadhimisha miaka 30 ya Kituo cha Carter (Carter Center) kinachojishughulisha na “kupigania masuala ya amani na kupambana na magonjwa duniani kote”. Rais Carter atakuwa anayajibu maswali hayo kwa njia...
Haiti: Kuokoa Maisha
“Idadi ya wagonjwa waliotibiwa katika siku 10 zilizopita ni 227″: matumaini ya kweli kwa haiti wanaeleza uzoefu wao wakati wanasaidia kupambana na ugonjwa wa kipindupindu.
Naijeria: Uzoma Okere ashinda kesi dhidi ya jeshi
Nigerian curiosity anaandika kuhusu kesi ya Uzoma Okere huko Naijeria: “Uzoma Okere ni msichana wa Kinaijeria ambaye kipigo alichopata kutoka kwa maafisa wa jeshi kiliondokea kuwa video iliyosambazwa sana na kuamsha hasira za wengi.”
Haiti: Kituo Cha Habari Chazinduliwa Kwa Ajili Ya Uanahabari wa Haiti
Réseau Citadelle anatangaza kuzinduliwa kwa Kituo Cha Habari, mradi unaotoka kwa Wanahabari Wasio Na Mipaka pamoja na Quebecor, wenye lengo la kuwezesha kazi za wanahabari wa ndani na wa nje ambao wako nchini Haiti, na pia kuunda ubia kati ya Asasi Zisizo za Kiserikali na Vyombo vya Habari.