Iran, Kama Inavyoelezewa na Kuandikwa na Waandishi wa Habari wa Ki-Irani

The image of the leader of the Iranian Revolution Imam Khomeini on the wall of a building in Sanandaj, in the capital of Iranian Kurdistan Province, as seen through an open window. Photo by Jordi Boixareu. Copyright Demotix

Picha ya kiongozi wa Mapinduzi ya Irani Imamu Khomeini ikiwa katika ukuta wa jengo huko Sanandaj, katika Mjii mkuu wa Irani kitongoji cha Kurdistan inavyoonekana kupitia dirishani.  Picha na  Jordi Boixareu. Hakimiliki Demotix

Muanzishaji mwenza wa Global Voices  Ethan Zuckerman amewaelezea kuwa “mfano wa daraja” watu ambao wanapenda kuelezea utamaduni wa nyumbani kwao kwa watu wanaotoka katika jamii nyingine. Wazo hiki lilitengenezwa kupitia mfumo ulioota mizizi ndani ya Global voices na unaelezea kazi kubwa na utamaduni wa jamii.  Kwa kuwa kazi yetu imelenga “kuunga” utengano uliopo kati ya mitazamo ya nje juu ya Irani na ile halisi ndani ya nchi yenyewe,  Global Voices Iran imeanza mfululizo wa mahojiani na mwanadishi wa Kiirani na waandishi ambao watafanya hivyo.

Mahojiano haya yatafanyika ili kuelewa kwa jinsi gani na kwa namna gani watu hawa waliofanya kazi zao kupitia kuielezea jamii iliyo nje ya Irani kuhusu Irani pamoja na ugumu na utata uliopo katika kuelezea.

Golnaz Esfandiari: “Nafikiri matumizi ya mitandao ya kijamii nchini Irani na manufaa yake yanaongezeka”

Golnaz Esfandiari ni mtangazaji mwandamizi katika  Redio Free Europe/Radio Liberty, na mmoja wa waandishi wa habari wachache ambao wamejikita nje ya Irani wakiandika kwa lugha ya Kiingereza kuhusu usumbufu na changamoto za jamii na siasa za Wairani.

Golnaz Esfandiari spoke to us about her experiences reporting Iran. Photo was taken at the Sixt Al Jazeera Forum in March, 2011. Used with permission from Golnaz.

Picha imetumika kwa ruhusa ya Golnaz Esfandiari.

Soma zaidi: Mazungumzo na Golnaz Esfandiari, Daraja la uhandishi wa habari kwa lugha ya Kiingerreza

Katika mahojiano na Global Voices, alisema:

Nafikiri matumizi ya mitandao ya kijamii nchini Irani yameongezeka na manufaa yake pia yameongezeka. Maafisa wa serikali wanakiri hilo nami pia ninaona watu wengi ndani ya nchi wakitumia mitandao ya jamii. Ninafikiri kuwa tangu mwaka 2009, matumizi ya mitandao ya kijamii imeongezeka kwa kiwango kikubwa.  Baadhi ya Wairani wameniambia kuwa wamejiunga na mtandao wa Twitter baada ya kusoma kuhusu yale madai ya “Mapinduzi ya Twitter” nchini Irani.  Mitandao ya kijamii inasaidia mazungumzo na kushirikishana maudhui ambayo yamekatazwa au yanayoonekana kama ya aibu na watu wanajadiliana kwa uwazi. Pia mara nyingi watu wanakosoa sera na mitazamo ya serikali katika mitandao ya jamii.

Kelly Golnoush Niknejad: “Unapaswa kuwa mwandishi wa habari,  mwanasaikolojia, profesa na msoma mawazo ya watu kwa wakati mmoja”

Mwekezaji katika tasnia ya habari nchini Irani Kelly Golnoush Niknejad, ni mwanzilishi wa ‘Taasisi ya Tehran’ chanzo cha habari kinachosaidizana na The Guardian ambapo huandika kuhusu Irani na Wairani walio ughaibuni. Mradi wake ni mmoja kati ya chanzo kinachoongoza kinachotoa mtazamo ‘tofauti’ kuhusu nchi hiyi katika masuala ya kisiasa, utamaduni na watu.

Niknejad akijipiga picha mwenyewe akiwa nyumbani kwake Boston kabla ya kongamano. Picha kwa hisani ya Niknejad, na imetumika kwa ruhusa.

Picha na Kelly Golnoush Niknejad na imetumika kwa ruhusa.

Soma zaidi: Jinsi  ‘Taasisi ya Tehran ‘ ya Kelly Golnoush Niknejad inavyounganisha Irani na ulimwengu wa Magharibi.

Katika mtazamo mbaya walio nao watu wasio wa-Irani dhidi ya Irani, alifafanua:

Linapokuja suala la Irani, huwa ninajikuta mara zote nikirudi nyuma mpaka mwaka 1979 kisha naelezea mabadiliko yaliyofanyika muongo baada ya muongo ili kuleta maana ya wakati huu wa sasa. Mara nyingine inakuwa vigumu sana hata kwa wa-Irani wenyewe kuelewa kinachoendelea Irani kwa sasa sembuse wasio wa-Irani. Hii inaonesha jinsi ilivyo muhimu kuifunika Irani “gubigubi,” tukiyaweka katika mtiririko maalum maisha ya watu wa kawaida. Tukiifikia nchini kwa kutoa taarifa za wasomi ma wenye mamlaka pekee hilo sio jambo la msingi au muhimu sana kwetu kama wanahabari. Ndio maana hata watu makini sana wanaofuatilia habari hawaelewi mambo ya msingi yanayotokea nchini Irani. Ni kweli kama watafuatilia taarifa za kutoka Taasisi ya Tehran basi watapata mtazamo tofauti sana.

Nina Ansary: “Ninaamini wanawake watakuwa mstari wa mbele katika mabadiliko yoyote nchini Irani”

Nina Ansary ni mtunzi wa “Johari za Mwenyenzi Mungu: Yasiyosimuliwa Kuhusu Wanawake Wa Irani,” kitabu cha kwanza kabisa kuandika kuhusu mtazamo wa haki sawa kwa wanawake katika siasa kuanzia mwishoni mwa karne ya 19 mpaka sasa.

Jalada la Johari za Mwenyenzi Mungu

“Jalada la kitabu cha Johari za Mwenyenzi Mungu

Kitabu kinafafanua jinsi wanawake wameweza kuijenga historia ya sasa ya Irani na wanavyoendelea kufanya hivyo, wakati wakiendelea kushughulika na kusimamisha misingi ya haki zao na usawa katika jamii ambazo zimekuwa zikiwakandamiza kwa asili.

Soma zaidi: Mazungumzo na Mwandishi Mpigania Usawa wa wanawake wa Kiirani Nina Ansary katika Mkesha wa usiku wa mabadiliko nchini

Ansary alisema kuwa “alikuwa na mtazamo chanya” kuhusu kesho ya Irani na nafasi ya mwanamke ndani yake:

…na ni kwa sababu niliona urejesho wao. Na hii ni kwa sababu wanaharakati wa kike hawakupata majibu ya uhakika: wanawake hawakuwa wakiruhusiwa kuwa majaji lakini sasa wanatumika kama majaji wapelelezi. Wanawake walikuwa hawaruhusiwi kusoma baadhi ya fani, lakini kwa miaka kadhaa wameweza kupenya hadi ndani ya fani ambazo zilitawaliwa na wanaume zaidi kama vile utabibu na uhandisi. Kwa tahadhari kubwa ninatazamia yaliyo chanya, lakini ninaamini wanawake watakuwa mstari wa mbele katika mabadiliko yoyote nchini Irani.

Saeed Kamali Dehghan: “Wanaiona Irani kama picha ya rangi nyeusi na nyeupe lakini Irani haiko hivyo. Ipo kama Upinde wa Mvua uliosambaa.”

Akiwa na makala zaidi ya 800 zinazohusiana na Irani, Saeed Kamali Dehghan ndiye mwandishi mkuu wa kwanza kwanza wa The Guardian aliyejitolea kuandika kuhusu Irani na ni mmoja wa wa-Irani wachache walioajiriwa na kampuni kubwa ya habari za lugha ya Kiingereza.

Picha imetumika kwa ruhusa ya Saeed Kamali Dehghan.

Taarifa zake nyingi zinahusiana na uvunjaji wa haki za binadamu nchini Irani, lakini kama alivyosema katika mahojiano kwa njia ya simu, “tatizo kubwa kwa vyombo vya habari vya Magharini ni kuwa wao huiona Irani kama picha ya rangi nyeusi na nyeupe lakini Irani haiko hivyo. Irani ni kama Upinde wa Mvua, imeenea rangi”

Soma zaidi: Saeed Kamali Dehghan anayeiandikia Irani katika gazeti la The Guardian

Katika magumu ya kuiandikia nchi ambayo anafungamana nayo kihisia, Saeed anafafanua kwamba:

Kama mu-Irani nina hisia zangu juu ya nchi, lakini ninapoandika habari zake huwa ninajaribu kukaa pembeni kidogo ili kuondoa upendeleo. Lakini ninaruhusiwa kuelezea mawazo yangu wakati nikiandika habari za kinyume na nimekuwa nikifanya kitu kama hicho. Niliandika kuhusu ni kwa nini Canada waliielewa Irani vibaya na hii ilipelekea waziri wa mambo ya nje wa wakati huo kunituhumu kupitia ukurasa wake wa Tweeter kuwa natumiwa na mamlaka za Irani. Nimekuwa nikishambuliwa na baadhi ya watu ambao wamekuwa wakinituhumu kuwa natumikishwa na wa-Irani na wengine wamekuwa wakinituhumu kuitumikia Uingereza. Ninaamini hii ni ishara ya kuwa ninaifanya kazi yangu ipasavyo.

Omid Memarian: “Kuigeuza hasira yako kuwa kitu cha kujenga na kutokuyachukulia mambo kibinafsi ni sanaa”

Omid Memarian, mwanahabari wa ki-Irani anayeishi New York.

Omid Memarian ni mwandishi wa zamani aliyesomwa sana huko Irani na sasa anafanya kazi Marekani na amekuwa akiandika habari za Irani kwa watumiaji wa lugha zote za Kiingereza na Kiajemi. Mahojiano yetu yalitaka kufahamu utofauti katika kuandika habari kuhusu Irani kwa watumiaji wa lugha tofauti tofauti na uzoefu wake kama mwanahabari wa ndani na nje ya Irani.

Soma zaidi: Mwanahabari wa ki-Irani Omid Memarian

Memarian anaelezea uzoefu wake wa kuandika na kuripotia katika jumuiya ya kijamii nchini Irani kama ifuatavyo:

Kulikuwapo na bado wapo watu ndani ya Irani ambao wanaamini kuziwezesha jumuiya za kijamii,vyama vya siasa na uhuru wa habari, serikali ya kiislamu inaweza kubadilika polepole kwa kuanzia ndani. Kwa upande mwingine kuna nguvu nyingine zinazopambana kuthibitisha kuwa hilo haliwezekani na njia mojawapo ni kuyafanya mazingira kuwa hatarishi kiasi kwamba hakuna mtu atadhubutu kubaki akifanya alichokuwa anakifanya. Niliposisitiza kuendelea kufanya nilichokuwa nafanya, kuandika nankuhamasisha kuhusu vitu nilivyokuwa naamini nilikamatwa na kutupwa gerezani.

Hooman Majd: “Irani haina utofauti wa kipekee: upekee hapa ni kuwa watu wengi hawafahamu mengi kuhusu Irani.”

Sasa tupo katika hatua za marejeo ya sera za nje za nchi ya Marekani. Majuma kadhaa kuelekea ukingoni mwa utawala wa Obama, kuna uwezekano mkubwa Marekani ikaachana na mradi wake mkubwa wa muda mrefu wa maelewano na adui yake wa muda mrefu, jamuhuri ya Kiislamu ya Irani. Katika mawio ya Uraisi wa Donald Trump yanayoonesha yatakuwa ya kipekee yenye uvuli wa magumu na jamuhuri ya kikatili, ninafikiri ni wakati wa kukaa chini na wanahabari na mtunzi Hooman Majd. Vitabu vyake, makala na machapisho yake yanafafanua “kitendawili cha Irani” ambayo kwa upana yameonekana katika vyombo vikubwa vya habari vya Marekani katika kipindi cha Bush, wakati wa ukatili dhidi ya serikali ya Irani ilipogeuka kuwa alama kuu mwanzoni mwa miaka ya 2000 katika sera za nje na mtazamo wa vyombo vya habari dhidi ya Irani.

Hooman Majd amekuwa akijulikana kama “sauti ya Irani” kwa nchi za Magharibi. Picha ya Majd ilipigwa na Ken Browar, imetumika kwa ruhusa.

Soma zaidi: Mazungumzo na Hooman Majd, daraja baina ya vyombo vya habari vya Irani na Marekani.

Kama mtazamo mbaya dhidi ya Irani umeleta somo tangu kutoka kwa kitabu chake mwaka 2008 kilicholenga kupinga mitazamo mibaya kuhusu jamii ya wa-Irani kwa wasomaji wa Marekani:

Ahmadinejad ndiye alikuwa wa kwanza kuwa wazi kwa vyombo vya habari, ambavyo ndio chanzo cha kwanza kabisa cha habari hasi. Lakini wa-Irani wenye asili ya Marekani na wa-Irani wenye asili ya Ulaya wameandika sana kuhusu utamaduni wao katika siku za hivi karibuni, na pia kuna safari nyingi sana kati ya Irani na Marekani baina na wa-Irani wenye asili ya Marekani na wa-Irani asilia. Kwa sasa wanauelewa mzuri kidogo na kuna vitabu vingi kidogo. Irani sio kitendawili cha kipekee: lakini kilicho cha pekee ni kuwa watu wengi hawafahamu mengi kuhusu Irani.