Dunia Yasimama na Palestina: Maandamano Yafanyika Kila Bara

Siku kadhaa tangu Israeli iivamie Gaza, maandamano yamemiminika katika miji kadhaa duniani kote kuwaunga mkono wa-Palestina na kutoa mwito wa kumalizwa kwa mashambulizi yanayoendelea. Kwa kutambua hitaji la kuonyesha mshikamano, mtandao wa Tumblr ulitengeneza mfumo wa kutunza kumbukumbu za maandamano haya. Akaunti hiyo, ambayo haina jina, inasema kuwa lengo ni kukusanya ‘Picha, video, na taarifa kutoka kwenye maandamano ya mshikamano na wa-Palestina wakati wa mashambulizi yanayoendelezwa na Israeli yenye sura ya adhabu ya umma.” Picha hizi zinatoka kwenye baadhi tu ya maandamano ambayo yamefanyika kwenye nchi nyingi duniani kote.

"World Cup protests in Brazil become Gaza protests."

“Maandamano ya kupinga Kombe la Dunia huko Brazil yageuka maandamano ya kupinga kinachofanyika Gaza.” – July 12, 2014.”

Kabul, Afghanistan – 13 Julai, 2014.

Hyderabad, India – 13 Julai, 2014.

Helsinki, Ufini – 12 Julai, 2014.

Istanbul, Uturuki – 12 Julai, 2014.

San Francisco, Califonia Marekani – 12 Julai, 2014.

Seoul, Korea Kusini – 12 Julai, 2014.

The Hague, Uholanzi – 12 Julai, 2014.

Japan – 12 Julai, 2014.

“Leo, watu wa Afrika Kusini wameandamana kuwaunga mkono wa-Palestina kwa kuteseka na Uvamizi huo. Nelson Mandela aliwahi kusema “Tunajua vizuri kuwa uhuru wetu haujakamilika bila uhuru wa wa-Palestina.” Kwa hiyo leo tumesimama kuwa sauti ya wasio na sauti.” – 13 Julai, 2014.

Indonesia – 12 Julai, 2014.

“Waandamanaji wa Montreal wakibeba bendera ndefu ya wa-Palestina kuwahi kuonekana duniani wakati wa maandamano ya Mshikamano na Gaza Ijumaa, Julai 11, 2014.”

Maldives – 12 Julai, 2014.

Tunis, Tunisia – 13 Julai, 2014.

Valparaiso, Chile – 12 Julai, 2014.

Berlin, Ujerumani – 12 Julai, 2014.

Canberra, Australia – 18 Julai, 2014.

“Siku ya tarehe 12 Julai kundi la watu kadhaa lilitayarisha maandamano ya kimya kimya mjini Krakow – kushikamana na Gaza. Waandamanaji walichapisha majina ya watoto waliouawa kwenye operesheni “kujilinda” inayoendelea Gaza.”

Exit mobile version