Kwa mara ya kwanza, wananchi wa Costa Rica waishio nje ya nchi wamepata fursa ya kupiga kura kwenye uchaguzi wa Rais. kutoka pande zote za dunia, raia wa Costa Rica wamekuwa wakiripoti kupita mtandao wa twita kuhusiana na upigaji kura katika nchi walizopo.
Esta vez los ticos 15,000 en el extranjero somos claves, nuestros votos pueden evitar una segunda ronda..#EleccionesCR #votoCR #vivomivoto
— carolina palma (@Carolpalma54) tarehe 2, Februari 2014
Kipindi hiki, sisi raia 15,000 tunaoishi nje ya nchi, ni ufunguo, kura zetu lazima zizuie kufungana katika kura.
Kutoka kwa Raia wa Costa Rica wanaoishi nchini Australia, ambao ndio waliokuwa wa kwanza kupiga kura, wakifuatiwa na wale wanaoishi Japan, Ufaransa, Marekani na kwingineko, raia wanaota taarifa huku wakionesha hisia zilizojaa hamaki.
Stephanie anataarifu kutoka Washington:
#VivoMiVoto @ Washington, DC pic.twitter.com/eftYI5MXGR
— Stephanie (@stephbrealey) Tarehe 2 Februari, 2014
Nimepiga kura yangu Washington, DC.
Francisco alisafiri kutoka Boston hadi New York ili kutimiza haki yake ya kupiga kura.
#VivoMiVoto Francisco Delgado estudia en Boston y viajó a Nueva York para votar pic.twitter.com/qcxQh6WPiI
— ameliarueda (@ameliarueda) Tarehe 2 Februari , 2014
Francisco Delgado anayesoma huko Boston alisafiri hadi New York ili apige kura yake .
Pia kutoka Marekani, Diego Rivera aweka picha hii:
Yo ya voté!! #VivoMiVoto #Voto2014 (Consulado de Costa Rica en Miami!) pic.twitter.com/FEt8Uq7Zzk
— Diego Rivera (@driverag) tarehe 2, Februari 2014
Tayari nimeshapiga kura yangu!!! (Ubalozi mdogo wa Costa Rica huko Miami!)
Kutoka Brussels, Silvia Muñoz na Alexander Molina washerehekea baada y kupiga kura:
#VivoMiVoto En Bruselas, la capital administrativa de Europa, votaron Silvia Muñoz Solano y Alexander Molina López pic.twitter.com/pMW5SJa5im
— ameliarueda (@ameliarueda) tarehe 2, Februari 2014
Huko Brussels, ambao ni mji mkuu wa kiutawala wa Ulaya, Silvia Muñoz Solano na Alexander Molina López , walipiga kura.
Moja kwa moja hadi China, msichana mmoja kutoka Cartago ataarifu kuhusiana na kupiga kura kwake:
#VivoMiVoto Sofía Hernández, de Cartago, votó en China. Ya la mesa de Beijing cerró la jornada (vía @maviru) pic.twitter.com/I1nFYyrKmE
— ameliarueda (@ameliarueda) tarehe 2, Februari 2014
Sofía Hernández, kutoka Cartago alipiga kura yake akiwa China. Kituo cha kupigia kura kilichopo Beijing tayari kilishafungwa.
Na pia, Adolfo Chaves anataarifu kutoka The Hague, Netherlands:
Mi voto en La Haya #EleccionesCR #VotoExteriorCR pic.twitter.com/DUETPV6GYe
— Adolfo Chaves J. (@adolfochaves) tarehe 2, Februari 2014
Kura yangu nikiwa The Hague.
Picha zaidi na taarifa zinapatikana kwa kufuata viungo habari #VotoExteriorCR [piga kura ukiwa nje ya Costa Rica], #EleccionesCR [Chaguzi Costa Rica] na #VivoMiVoto [Ninapiga kura yangu].