(…) kuna nafasi ambayo mpaka sasa haijatumiwa ipasavyo na vyama vya siasa nchini Msumbiji, iwe ni kwa ajili ya kueneza propaganda za kisiasa au kufanya kampeni za uchaguzi: nalo ni mtandao wa intaneti.
Jukwaa la Msumbiji liitwalo Olho Cidadão (Jicho la Wananchi) lilizindua blogu mpya tarhe 2 Aprili, 2013, kwa uchambuzi wa uwepo wa vyama vya siasa mtandaoni [pt]. Msumbiji itafanya uchaguzi wa manispaa tarehe 20 Novemba mwaka huu.