PICHA: Maandamano ya Pamoja ya Watu wa Shia Nchini kote Pakistan Yamalizika Kwa Amani.

Maandamano ya mshikamano ya watu wa Shia yaliyoendeshwa kwenye takribani majiji 100 katika maeneo mbalimbali ya Pakistan hatimaye yamefikia tamati. Maandamano yalichochewa mara baada ya milipuko ya mabomu iliyowaua watu zaidi ya 100 wa jamii ya Hazara ya Shia katika jiji lililopo Kusini Magharibi mwa jiji la Quetta mnamo Januari 10, 2013.

Milipuko hiyo ya mabomu iliweka kumbukumbu ya miongoni mwa siku mbaya ya umwagaji damu katika historia ya jimbo la kusini Magharibi la Balochistan. Wanachama wa kikundi cha kijeshi kilichofutwa cha Laskher-e-Jhangvi walidai kuhusika na ukatili huo.
Kufuatia mashambulizi hayo, watu wa jamii ya Hazara wa kutoka Quetta walikutana katika barabara ya Alamdar na kisha kuanzisha maandamano ya amani ya kukaa mahali pamoja na kuishinikiza serikali kusikiliza madai yao. Wakati picha zao zikisambazwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii zikiwaonesha wakiwa wamekaa huku wakinyeshewa na mvua iliyoambatana na barafu sambamba na majeneza ya ndugu zao, maandamano ya mshikamano kwa mtindo wa maandamano ya amani ya kukusanyika sehemu moja yalisambaa kama moto katika sehemu mbalimbali za nchi. Watu wa Pakistan kutoka katika makundi makuu ya dini pamoja na makabila yaliungana kupinga ugaidi katika jina la Uislam

Waandamanaji katika jiji la Quetta walikuwa na agenda moja tu:

“Jiji la Quetta liwekwe chini ya uangalizi wa Jeshi na iwe kama sheria ya utawala.”

Iliichukua serikali siku nne kujadili jambo hili; hatimaye ilituma ujumbe kuashiria kusitishwa kwa maandamano ya siku nne ya kukaa mahali pamoja. Zaidi, ndugu wa marehemu walikataa kuzika miili ya ndugu zao waliofariki mpaka pale madai yao yatakapotatuliwa. Kwa kuwa maandamano yameshasitiswa, waliofariki sasa wanazikwa.

Raia walipanga maandamano ya kuishinikiza serikali kutatua madai yao katika maeneo yote ya nchi ya Pakistan. Maandamano yalifanyikia katika barabara kuu za treni na katika barabra kuu za magari. Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa, maandamano yalianzishwa kwenye zaidi ya majiji 100 na katika miji kadhaa. Maandamano pia yalianzishwa katika jiji la Skardu, ambapo jotoridi wakati wa usiku lilifikia nyuzijoto hasi 14. Lengo lilikuwa rahisi:

Kubaliana na matakwa ya waandamanaji wa Quetta.

Kinachofuata ni muonekano katika picha wa baadhi ya maandamano katika miji mikuu ya Pakistan:

Karachi

Maandamano mbele ya nyumba ya Bilawal ya kupinga mauaji ya Shia. Chanzo: ‏@ArsalanMKhan

Maandamano mbele ya nyumba ya Bilawal ya kupinga mauaji ya Shia. Haki miliki: FacebookSyed Sabih Abbass Rizvi. Used with permission

Maandamano katika klabu ya vyombo vya habari ya KarachiProtest at Karachi Press Club. Chanzo: @‏faisalkapadia

Mtoto wakati wa maandamano ya mshikamano wa waShia karibu na Numaish Chowrangi. Chanzo: @arifaBatool

Ifuatayo ni video maandamano ya Numaish, Karachi.

Hyderabad

Maandamanno karibu na barabara ndogo ya Hyderabad. Chanzo: ‏@ImZeesh

Lahore

# Sisi sote ni waandamanaji wa Hazara katika Lahore. Muda: saa nane usiku. Chanzo: ‏@XumarShirazi

Maandamano mbele ya nyumba ya Gavana wa Lahore. Muda: 5:30 usiku. Chanzo: Qurrat-ul -in Haider (‏@mojesma)

Msichana mdogo wa Shia akiwaomba “kaka zake wa Sunni” kujiunga na maandamano. Chanzo: ‏@annyzaidi

Maandamano ya kukusanyika sehemu moja yaendelea usiku kucha. Chanzo: FaceBookTaimour Mubashar

Islamabad

Wanawake na watoto wakati wa maandamano ya pamoja ya kuishinikiza serikali kusikiliza matakwa yao. Chanzo: ‏@Zulfi25

Wanajitahidi kwa kadiri wawezavyo kukabiliana na hali ya hewa ya baridi kali. Chanzo: ‏@Mehr_Shah

Peshawar

Mtoto mdogo akishiriki katika maandamano. Chanzo: ‏@Khushal

Maandamano ya Peshawar. Chanzo: Hassan Turi (‏@spin_ghar)

Quetta

Watu wakiwa wamekaa na maiti za wapendwa wao huko Quetta. Chanzo: Humayoun Behzad (‏@behzadjee)

Maandamano makubwa yaliyoanzishwa na Chama cha Maendeleo cha Hazara (HDP) huko Quetta. Chanzo: Humayoun Behzad (‏@behzadjee)

Watu wakiwa imara. Jotoridi wakati wa usiku huko Quetta likiwa bado ni chini ya nyuzijoto sifuri. Chanzo: Humayoun Behzad (‏@behzadjee)

Exit mobile version